Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,560
Mkapa, unasema, hakuwa na "mix" lakini aliweza kuongoza nchi. Kwa hiyo kumbe "mix" si lazima.
By the way, Nyerere alikuwa dikteta, hawezi kusemwa ana humility. Watu walifungwa kwa kuwa na mawazo tofauti, unyenyekevu gani unoongelea?
Inawezekana juu kabisa ya jedwali la kuweza kuongoza kuna intelligence tupu isiyo na humility inaweza kuongoza, katikati kuna aina tofauti za mix za intelligence na humility zinazoweza kuongoza, chini kabisa huku ambako hakuwezi kuongoza hakuna mix yoyote ya intelligence na humility. Ni ujinga na kujiona bab kubwa tu.
Sasa hapo unaweza kuambiwa huyu Magufuli hajafikia mix ya intelligence na humility ya kuweza kuongoza, yupo chini kabisa.
Suala la Nyerere kufunga watu liongelee kwa ushahidi na mifano. Sijakwambia Nyerere alikuwa doormat, nimekwambia Nyerere alikuwa na mix ya intelligence na humility. Kama alitumia katiba kufunga wapinzani wake huwezi kusema alikuwa dikteta kwa sababu dikteta anatumia neno lake tu, si sheria.