Tanzania’s President John Magufuli bans Opposition Politicians from Politics

Suala la Nyerere kufunga watu liongelee kwa ushahidi na mifano.
Good step in the right direction, at least umenyoosha maelezo kwamba huhitaji "mix" kuweza kuongoza.

Wewe umetoa ushahidi na mifano ya unyenyekevu wa Nyerere? Kama hujui kwamba watu walifungwa kisiasa wakati wa Nyerere basi sidhani kama tutafika mbali kimjadala.
 
First things first.

Niliandika hivi.

Hana mix ya humility na intelligence inayotakiwa kuongoza nchi.

Sijaandika kwamba unahitaji mix kuweza kuongoza. Hivyo siwezi kunyoosha kitu ambacho hakikupinda tangu mwanzo. Unaweza kuwa huna mix ila umeipita hiyo mix kwa mbali sana na ukaweza kuongoza.

Kama kuna kitu kinachonyooka hapa ni uelewa wako wa kitu kile kile nilichokiandika tangu awali.

Inawezekana ukiwa na shaba huwezi kuongoza kabisa, ukiwa na dhahabu unaweza kuongoza kidogo, ukiwa na platinum unafaa kuongoza kabisa.

Mtu akisema "huyu hana dhahabu inayotakiwa kuongoza nchi", kwa maana ya kwamba hana the bare minimum threshold, haina maana kwamba aliye na platinum, maximum qualification possible, hawezi kuongoza.
 
Magufuli ni mtu asiye na upeo wa kuongoza nchi. Ni mtu wa kuongozwa tu.

Hana mix ya humility na intelligence inayotakiwa kuongoza nchi.

Ukiwa na humility kubwa na intelligence kubwa, hiyo ni best mix (Nyerere).

Ukiwa na humility kubwa na intelligence ya wastani, unaweza kusaidiwa kuongoza nchi (Mwinyi)

Ukiwa na humility ya wastani na intelligence ya wastani,pia unaweza kusaidiwa kuendesha nchi vizuri (Kikwete)

Ukiwa huna humility na una intelligence, unaweza kuendesha nchi (Mkapa)

Ukiwa huna humility wala intelligence, tena uko conceited, hata kusaidiwa kuendesha nchi ni kazi nzito sana, maana utawatukana mpaka wanaokusaidia kuendesha nchi kwa kujiona wewe zaidi wakati huna lolote (Magufuli)
 
Nimependa description ya watawala wetu (maana hakuna kiongozi, except Nyerere), umeni impress sana! Kumbe kuna watu can think!
 
But since Magufuli was elected in October 2015, the list of human rights complaints has been growing.

Although Magufuli has managed to restore public accountability, “he has not succeeded in promoting human rights, especially people and political rights,” said Helen Kijo-Bisimba, who leads Tanzania’s Legal and Human Rights Center.

Huyu Mama kumbe bado anawashwa washwa

Hivi ameshaenda kumtembelea Lissu?
 
Mtu akisema "huyu hana dhahabu inayotakiwa kuongoza nchi", kwa maana ya kwamba hana the bare minimum threshold, haina maana kwamba aliye na platinum, maximum qualification possible, hawezi kuongoza.

kwani nani kasema aliye na platinum hawezi kuongoza nchi?
 
kwani nani kasema aliye na platinum hawezi kuongoza nchi?
Kama hakuna swali juu ya aliye na platinum kuweza kuongoza nchi, kwa nini ambaye hana hata gold kumsema huyu hana gold inayotakiwa kuongoza nchi kuzushe suala la mbona huyu ana platinum hana gold na kaongoza nchi?
 
Umenichekesha sana mkuu.

Ila umeniacha kwa msamiati, hilo fogong'o ni kitu gani? Ni neno la Kiswahili rasmi, kilugha za makabila au kati ya maneno ya Kiswahili cha mtaani tu?

Niko mbali kidogo na kamusi zangu hapa lasivyo ningelitafuta.
Fogong'o ni Jumuia zinazoundwa na watu wa jamii ya kisukuma ambao zinalenga kutatua shida mbali mbali kwanzia ngazi ya familia mpaka kijiji kwa ujumla. Na mara nyingi makutano yao ni kila baada ya mwezi.

Mimi nimewahi kuudhuria fogong'o nikajionea ni jinsi gani viongozi wanavyoendesha mambo kwa utaratibu, kwa vitu ambavyo hawajui wanawaachia wajuzi hata kama ni kijana mdogo tu ila shariti awe ameoa.

Sasa raisi magufuli hakuna asichokifahamu wakati ukweli ni kwamba kuna vingi hasivyovifahamu.
 
Asante sana mkuu. Mimi Msukuma wa Dar, Kisukuma napenda na najua cha hapa na pale. Ila najifunza bado.

Nimeongeza msamiati.

Ong'wene oyo ateho nolo kobeja ha fogong'o. Kongono ate na masala gete. Wetaga mamihayo nya chilochilo gete.

Kokaya obise tole mamnho ga kobeja mamihayo nyalali getegete. Ong'wene oyo wobiza ntemi sagala gete.

Wabeja namhala.
 
Jirani wakikutangaza kuwa wewe ni mchawi na ukidharau bila kuliweka sawa hilo basi we we ni mchawi kweli
Hii sio habari njema, wale jamaa huanza kukuchokonoa kwa jani mwishowe wanakukata na panga
 
This should be the basis of deleting this thread. Siyo kila kinachoandikwa na mzungu mmoja ndiyo maono ya wazungu walio wengi ambao wanampenda sana rais wetu: ushahidi ukiwa ni jinsi wanavyo miminika kuja kumuona ikulu na kumpa support ya hali na mali, hadi akina Bill Gate na rais wa benki ya dunia!! Support ya namna hii haijawahi kutokea huko miaka ya nyuma. Tuliona marais wetu miaka ya nyuma walivyokuwa wanadharirika kutembea nchi za wazungu kila kukicha wakitembeza bakuli la kuomba misaada hadi tukafikia kuwaita ma Vasco Dagama. Leo rais wetu katulia nyumbani akinyoosha nchi, watu hawa wanamfuata wenyewe, kumpongeza na kumpa support!

1.Demokrasia si kufanya maandamano kila kukicha. Hata huko kwa wazungu hawafanyi hivyo.

2.Demokrasia si kuonesha mikutano ya bunge live. Hata huko kwa wazungu hawafanyi hivyo.

3. Demokrasia si maseneta (kwetu tunawaita wabunge) wa jimbo fulani kwenda kufanya mikutano ya kisiasa kwenye majimbo ambalo siyo ya kwao isipokuwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu au mdogo kwa utaratibu uliowekwa na tume ya uchaguzi.

4. Demokrasia siyo kwamba gazeti au chombo cha habari cho chote kinaweza kuandika au kusema au kuropoka anything bila kuzingatia maadili ya uanahabari na sheria za nchi. Hata huko kwa wazungu hawafanyi hivyo.

5. Demokrasia si kwamba unaweza kutumia mawasiliano ya kimtandao kama unavyotaka hata kama unavunja sheria, mila na utamaduni wa nchi yako na hata huko kwa wazungu hawafanyi hivyo.

6. Demokrasia siyo kwamba wale ambao chama chao kilishindwa uchaguzi (wapinzani) ndiyo mawazo yao walazimishe yaendeshe nchi na kufanya choko choko. Hata huko kwa wazungu hawafanyi hivyo.

7. Democracy is the government of the people by the people and for the people through their elected government. The word people here means the majority of the people and not the minority (wapinzanj) who had failed in the elections. Hawa minority hawapaswi hata kusikilizwa bali wanaruhusiwa kusema wakiwa bungeni kwa utaratibu na kanuni za bunge. Na hata huko kwa wazungu hali iko hivyo.

8. Demokrasia si kama wanavyotaka akina Mbowe na wenzake tuamini. Ni kinyume chake kabisa na hao wazungu wanajua hivyo.

10. Demokrasia siyo wabunge wa upinzani kwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za nchi wawe bungeni au nje ya bunge. Wakifanya hivyo kama ambavyo wanaendelea kufanya, basi kila kukicha tutaendelea kushuhudia wakikamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani hadi pale watakapokoma tabia hiyo au watakapokuwa wamenyooka. Haya ndiyo mabadiliko ya kweli watanzania waliyoyataka na kuyapigia kura mwaka 2015. Tusubiri hadi 2020 kuona kama watayabadilisha. Sasa hivi povu za nini?
Kwa hiyo democrasia ni kumpiga risasi mtu anaesema maovu ya serikali
 
Walale mbele hakuna madini hapa

Hii post ifutwe usimuweke mello matatizoni
Umesoma na kuielewa lakini. Post imetulia sana hiyo na inaeleza ukweli mtupu labda kwakuwa tupo katika awamu ya kutotaka kuambiwa ukweli katika utendaji wetu mbovu. Ndiyo yale yale mtu anatoa taarifaya ubovu fulani badala ya kushukuriwa anakamatwa. Baada ya hapo wanakubali kuwa kuwa nyufa zipo ktk expansion joints!
 
Back
Top Bottom