Tanzania yongoza kwa ughali wa simu kutoka ughaibuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yongoza kwa ughali wa simu kutoka ughaibuni

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Nov 6, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  BAADHI ya Watanzania wanaoishi Ulaya na Marekani wamesema Tanzania inakosa mapato mengi kutokana na gharama za kupiga simu nchini kuwa ghali karibu mara tatu ya viwango vya nchi zote za Afrika Mashariki.


  Wamesema kuwa inawabidi kutumia ujanja wa kupiga simu nchini kupitia nchi jirani kama vile Kenya na Uganda ili kukwepa mzigo wa gharama za kuunganishwa ili kuwasiliana moja kwa moja na ndugu zao nchini.


  "Sisi kama Watanzania tunaopenda kuisaidia ndugu na nchi yetu kwa ujumla kwa sasa tunaona kero kupiga simu za moja kwa moja kwa sababu gharaa za uunganishaji simu zinazoingia Tanzania moja kwa moja kutoka hapa (Ulaya) ni ghali sana," alisema mmoja wa watanzania anayeishi nchini Marekani.


  Alielezea mtindo wa Watanzania wengi wanaoishi ugaibuni kuona njia rahisi ni kuunganishwa simu kwa kupitia kampuni za simu za Kenya au Uganda zinaipunguzia mapato Tanzania na kunufaisha nchi jirani.


  "Katika hili nani anapoteza?" Alihoji Mtanzania huyo na kujibu: "Tanzania kama nchi ndiyo inayoathirika kwa sababu tu ya gharama kubwa za uunganishaji simu za ughaibuni. Kwa sasa simu zinazopigwa kuja huko Tanzania zinapitishiwa Kenya na Uganda, hivyo mapato yanaenda kwa nchi hizo."


  Alifafanua kuwa nchi hizo jirani zinafaidika mara mbili, kwanza kwa kuunganisha simu kuingia nchini kwao na pili kuzielekeza tena kwenda Tanzania.


  Pamoja na mzunguko huo, Watanzania hao wanadai ni njia yenye gharama nafuu zaidi kuliko kupiga simu za moja kwa moja nchini.


  Akizungumza kwa kuwawakilisha Watanzania wenzake wa huko Ughaibuni ambao wamekuwa wakisononeshwa na jambo hilo, waliitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuingilia kati suala hilo ili uchumi wa nchi usiendelee kuhujumiwa.


  Alisema mara kadhaa wamewasiliana na TCRA bila mafanikio na uchunguzi wao wa awali ulibaini kuwa kampuni za simu nchini zinapewa uhuru wa kujipangia viwango vya gharama za kuunganisha simu zinazoingia nchini.


  Gharama za simu
  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kupitia kampuni za simu nchini Marekani za Rebtel, Wisecalling na VIP, umedhihirisha wazi kuwa malalamiko ya Watanzania hao yana hoja ambayo serikali kupitia TCRA inapaswa kuingilia kati.


  Kwenye mtandao wa kompyuta wa kampuni hizo ulionyesha wazi viwango vya gharama za kuunganisha simu Tanzania ni aghali kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki.


  Gharama hizo ambazo zimo kwa kiwango cha senti za dola za Marekani kwa kila sekunde ambayo muongeaji anatumia wakati anaunganishwa na simu kwa ukanda wa Afrika Mashariki ziliainishwa kama ifuatavyo.


  Kampuni ya Rebtel kupiga simu Tanzania kupitia simu za mezani na mkononi ni 25, Kenya 8 kwa simu za mezani na 10 kwa simu za mkononi, Uganda 12 simu za mezani na 13 za mkononi, Rwanda 15 mezani na mkononi wakati Burundi mezani na mkononi ni 14.


  Kampuni ya VIP kwa Tanzania simu za mezani 24 na mkononi 25 wakati Kenya ni 9 kwa mezani na mkononi ni 12, Uganda ni 13 kwa mezani na mkononi, Rwanda 16 mezani na 18 mkononi wakati Burundi 12 mezani na 18 mkononi.


  Kampuni ya Wisecalling kwa Tanzania ni 14 mezani na 24 mkononi wakati Kenya ni 6 mezani na 10 mkononi, Uganda 6 mezani na 17 mkononi, Rwanda 16 mezani na 13 mkononi na Burundi 7 mezani na 13 mkononi.


  Meneja Uhusiano wa TCRA, Innocent Mungy alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema mamlaka hiyo haina uwezo wa kudhibiti gharama zinazotozwa kwa simu zinazoingia kwenye mitandao ya hapa nchini.


  “Sisi (TCRA) tuulizeni gharama za viwango vya kupiga simu kwa kampuni zetu za ndani, maana kisheria ndiko mamlaka yaetu yanakoishia, lakini kuhusu simu zinazoingia kutoka nje sisi hatuna mamlaka ya kuziingilia,”alisema Mungy na kuongeza:


  “Kuna kampuni kubwa tano zilizopewa leseni gateway (kupokea simu za kimataifa) na kuziingiza kwenye mtandao wa hapa nchini, sasa TCRA haiwezi kufahamu ni kiwango gani zinachotozwa kampuni za simu za ndani katika kupata huduma hiyo, na wao wanawatoza vipi wateja wa huko”.


  Maelezo hayo ya Mungy yanamaanisha kwamba TCRA wana uwezo wa kisheria wa kudhibiti viwango vinavyotozwa kwa simu zinazopigwa kutoka nchini pekee, lakini gharama ya simu zinazoingia kutoka nje ya nchi zimeachwa mikononi mwa kampuni za simu husika.

  chanzo. Gazeti la Mwananchi
   
 2. Mageuzi

  Mageuzi Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi sheria iliyounda TCCRA inasemaje?nilidhani mawasiliano ni ya ndani ya nchi na yale yanayoingia kutoka nje ya nchi.Mungi inabidi uwape ushauri viongozi wako wafanye review ya majukumu yao.ukizingatia wameshapewa kashfa ya kutumia bilioni za TZS kutoa elimu kwwa wafanyakazi wachache.sometime natamani kumwambia JK afute hii Taasisi.ila Mr.Mungi unafanya kazi nzuri kwa mwajiri wako,nakupongeza kwa kazi zako katika online media.
   
Loading...