Tanzania yenye mafuta na gesi, watanzania tuwe makini na vibaraka wa wazungu

kanone

JF-Expert Member
Oct 10, 2013
6,188
1,576
Historia inaonyesha kuwa nchi zote zenye rasilimali nyingi pamoja na mafuta na gesi hazina amani, zimejaa machafuko na wanaoangaika ni wazee, watoto na wakina mama,

Pia uko ushaidi wa kitakwimu mataifa ya ulaya wamekuwa yakitumia nafasi hiyo kuwavuruga kuwachonganisha ili hali wao wapate nafasi ya kuuza sihara na kuwaibia.

Ushauri wangu: Ktk kipindi hiki, SERIKALI na vyombo vya Dola wanapaswa kuwa makini na kufatilia mienendo ya viongozi wa serikali na KISIASA WOTE wanaoonekana wako karibu na wazungu na kuwageuza vibaraka wao ili kutimiza Malengo YAO.

VYOMBO vya Dola sio wakati wa kulala ni wakati wa kufatilia kila mienendo ya wanasiasa na watu binafsi kujilizisha ukaribu na misaada wanayopewa ni ya malengo gani?

Maana kila MTU anajua wazungu kila nchi yenye machafuko Afrika ukitoa Burundi ambayo sijafanya tafiti kujilizisha uko mkono wa wakoloni wazungu KUPITIA vibaraka wao waafrika wenzetu,

So vyombo vya Dola timiza dhamana zenu na wajibu kwa kujilizisha na kila mwanasiasa awe anaishi Tanzania au nje ya nchi ili vizaze vujavyo viikute aman hii watawakumbuka,
 
Kimsingi nchi nyingi zimeingia penye machafuko kutokana na rasilimali walizobarikiwa na mwenyezimungu tamaa ya vibaraka wachache wenye uchu wa kujilimbikizia mali.

Mpaka kuna wakati mtu unajiuliza kuwa na rasilimali hizo sio baraka tena ila ni laana tumeona jinsi savimbi na kundi lake la UNITA walivyoiharibu Angola au Sierra Leone na fodei sankho ni mambo ya kuchukiwa kwa kweli.

Na hapo ndipo tunapopaswa kupaza sauti zetu kulipigia kelele kwa ustawi wa vizazi vijavyo.
 
Fafanua, serikali na vyombo vya dola ni kina nani hasa na viwafuatilie viongozi wa serikali na siasa kina nani? Kama rais na mkuu wa majeshi wakiwa karibu na "wazungu" watafuatiliwa na nani serikalini na kwenye vyombo vya dola? Kubwa zaidi, unaamini kweli serikali yetu, kuanzia rais hadi watendaji, ina ubavu wa kukaa mbali na "wazungu"?
 
Back
Top Bottom