Tanzania yashuka nafasi moja katika viwango vya Fifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yashuka nafasi moja katika viwango vya Fifa

Discussion in 'Sports' started by Ngongo, Sep 3, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,056
  Likes Received: 3,416
  Trophy Points: 280
  ANZANIA imeshuka kwa nafasi moja katika viwango vya ubora wa Shirikisho la Kimataifa la Soka, Fifa, kwa mujibu wa viwango vya ubora kwa mwezi uliopita.

  Tanzania ilipanda hadi nafasi ya 93 miezi miwili iliyopita, baada ya kuifunga New Zealand mabao 2-1, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Dar es Salaam mapema Juni. Timu hiyo ilikuwa ikienda Afrika Kusini kushiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho.

  Kwa mujibu wa tovuti ya Fifa, Tanzania imeshuka kwa nafasi moja kutoka 93 hadi 94 licha ya kubakia kwenye nafasi yake ya 23 ya ubora wa soka Afrika.

  Kabla ya kushika nafasi ya 93, Taifa Stars ilipanda kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 97 hadi 93 katika viwango hivyo vya FIFA.

  Baada ya mechi ya Rwanda iliyofanyika kwenye mji wa Kigali, timu hiyo iliichapa mabao 2-1 katika mecghi zinazoandaliwa na Fifa, lakini matokeo hayo yamekuwa tofauti na matarajio ya wengi kuwa Tanzania ingepanda zaidi.

  Mtandao huo wa viwango unaonyesha kuwa, kwa nchi za Afrika Mashariki, Uganda ndiyo inayoongoza baada ya kupanda kutoka nafasi ya 75 hadi 72 na inashika nafasi ya 15 kwa ubora wa soka Afrika.

  Katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Tanzania iko juu ya mataifa ya Kenya, Rwanda na Burundi. Kenya pia imepanda kwa nafasi moja kutoka 105 hadi 104 na imepanda kwa nafasi moja kutoka 28 hadi 27 katika viwango vya CAF.

  Rwanda, ambayo ipo Afrika ya Mashariki pia, haijapanda wala kushuka katika viwango vya FIFA na kubakia katika nafasi ya 117, lakini imepanda katika viwango vya CAF kwa nafasi moja kutoka 31 mpaka 30.

  Timu nyingine ambayo inapatikana katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki ni Burundi ambayo imepanda kwa nafasi tatu kutoka 128 mpaka 125 katika viwango vya FIFA, lakini imebaki katika nafasi ya 35 katika viwango vya CAF.

  Tangu Fifa iamue kutoa viwango mwaka 1993, nchi mbali mbali zimekuwa zikifuatilia taarifa hizo kwa kuangalia nchi zao zinasimama vipi katika msimamo huo wa viwango na zinaendelea vipi kisoka.

  Brazil ndiyo inayoongoza kwa ubora duniani ikifuatiwa na Hispania na Uholanzi inayoshika nafasi ya tatu.
   
Loading...