Tanzania yapanda katika viwango ya FIFA

Tanzania yapanda katika viwango ya FIFA

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
Tanzania yapanda FIFA: Tanzania ni ya 106-yapanda kwa nafasi 7 katika orodha ya Fifa iliyotolewa leo. Kenya ya 95, Uganda 87. Germany yaongoza, Spain yashuka hadi 8.

====
UBORA DUNIANI: GERMANY SASA
NAMBA MOJA, SPAIN YATUPWA YA
8, TANZANIA YAPANDA 7!




MABINGWA WAPYA DUNIANI, Germany, leo wamewapindua Spain toka namba moja duniani na kukamata nafasi hiyo katika orodha ya Ubora Duniani iliyotolewa leo hii na FIFA.

Argentina, ambao walifungwa Bao 1-0 na Germany kwenye Fainali ya Kombe la Dunia huko Maracana, Rio de Janeiro, Brazil Jumapili iliyopita, wameshika Nafasi ya Pili. Spain, ambao walikuwa Mabingwa Watetezi wa Kombe la Dunia walilotwaa huko Afrika Kusini Mwaka 2010 na kushikilia Namba 1 tangu wakati huo, wametupwa Nafasi ya 8. Kwa Nchi za Afrika, Nchi ya Juu kabisa ni Algeria ambao walitolewa Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia na Germany kwa kufungwa kwa taabu Bao 2-1 na sasa wamekamata Nafasi ya 24 kwa Ubora Duniani. Tanzania ipo nafasi ya 106 baada kupanda Nafasi 7.


Netherlands wamenufaika sana kwa mafanikio yao huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa kupanda nafasi 12 na kushika Nafasi ya 3. England imeporomoka Nafasi 10 na sasa wako Nafasi ya 20.

Nchi nyingine zilizotolewa 10 Bora ni Italy na Portugal na zilizoingia humo, pamoja na Netherlands, ni Belgium na France.

Orodha nyingine ya Ubora Duniani itatolewa Agosti 14.



TIMU ZA JUU 30:
1 Germany [Imepanda Nafasi 1]
2 Argentina [Imepanda 3]
3 Netherlands [Imepanda 12]
4 Colombia [Imepanda 4]
5 Belgium [Imepanda 6]
6 Uruguay [Imeshuka 4]
7 Brazil [Imeshuka 4]
8 Spain [Imeshuka 7]
9 Switzerland [Imeshuka 3]
10 France [Imepanda 7]
11 Portugal
12 Chile
13 Greece
14 Italy
15 USA
16 Costa Rica
17 Croatia
18 Mexico
19 Bosnia and Herzegovina
20 England
21 Ecuador
22 Ukraine
23 Russia
24 Algeria
25 Côte d'Ivoire
26 Denmark
27 Scotland
28 Romania
29 Sweden
30 Venezuela



TANZANIA NA JIRANI ZAKE:
101 New Zealand
102 Moldova
103 Latvia
104 Lithuania
105 Bahrain
106 Tanzania [Imepanda Nafasi 7]
107 Kuwait
108 Luxembourg
109 Rwanda
110 Ethiopia
111 Equatorial Guinea
112 Namibia
113 Haiti
114 Mozambique
115 Sudan

Zaidi: http://www.fifa.com/worldranking/rankingtable/
 
Dah sasa hapo lini tutafika top 100
 
Tanzania kila sehemu tumefeli. Soka tupo mkiani, elimu ndio kabisa hoi, huduma za afya bwaaaa, kote hoi labda chini ya kitovu
 
Hakuna siri ya mafanikio zaidi ya kushinda mechi za majaribio na zile za mashindano...

Tutegemee kupanda tena kama tukiwafunga Msumbiji mechi zote mbili...
 
Kufuatia kutwaa kombe la dunia,Ujerumani sasa yaongoza katika viwango vya soka ulimwenguni ikifuatiwa na Argentina pamoja na Uholanzi katika nafasi za pili na tatu. Nafasi ya nne ni Colombia ikifuatiwa na Ubelgiji,Uruguay,Brazil,Hispania,Uswisi na Ufaransa.

Orodha hiyo inaonyesha kuwa Algeria inaongoza Afrika ikishika nafasi ya 24 kidunia Ivory Coast iko nafasi ya 25 kidunia. Nigeria imepaa kwa nafasi kumi hadi 34 kidunia.

Costa Rica imechumpa hadi nafasi ya 16 nafasi moja nyuma ya Marekani iliyo nafasi ya 15...
 
hizi ranks za FIFA ni siasa tu. sasa USA ana ubora gani wa kuwa kwenye nafasi hiyo!
 
hizi ranks za FIFA ni siasa tu. sasa USA ana ubora gani wa kuwa kwenye nafasi hiyo!

Nakushauri jaribu kuangalia usa huwa anafika wapi kwenye mashindano mbali mbali .. USA ni wazuri sana . Usiendeshwe kwa hisia angalia ranks na matokeo yao
 
Kichwa cha thread kigugumizi, hebu waombe uongozi wakusaidie kurekebisha!
 
Mkia wa ma.ma yako? Mijitu mingine imezoea kukosoa tu.
wa baba yako...peleka matusi yako kwa wajinga wenzio huko...watu wengine mtakufa na matress yenu...kapeti kama mkeka weee..
 
Kenya nafasi ya 95, Uganda 87. Yaani hadi Palestina wametupita eti.
New Zealand, Montenegro, Moldova, Lithuania, Latvia, wote hao wametupita.
kina Usain Bolt, Jamaica wala kush nao wapo mbali yetu.
Ila nashangaa imekuwaje tumewapita Sudan na Ethiopia wakati wao wanakaza sana kuliko hawa wauza samaki huku feri.

"Nlikuwepo":bolt:
 
Back
Top Bottom