chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,982
Kunga'ra duniani na kung'ra locally vitu tofauti kabisa...Tanzania inaweza kuwa na amani ikilinganishwa na nchi zinazoizunguka, kwa dunia haipoIking'ara Afrika Mashariki ama duniani si ni kung'aa tu. La muhimu imeng'aa ama unataka tuwe tunanunua nyama kwenye mabucha ya Ulaya wakati nyama ni ile ile?
Kipimo cha amani nchini mwako wewe unakipimaje? Au unasubiri ripoti ya nje?Inang'ara kwa amani Duniani au Afrika Mashariki?
Kunga'ra duniani na kung'ra locally vitu tofauti kabisa...Tanzania inaweza kuwa na amani ikilinganishwa na nchi zinazoizunguka, ila kwa dunia haipo
Hao wanaowasifia kwa amani si ndio waliwakosoa kwa mauaji ya watu juzi mkawap
Na wakikosoa watu kama nyinyi huja mbio mkifurahi na vi screen shot vyenu mnapongezana ila wakisifia sasa povu jingiiiii kama hivi...tulishawazoea pingapinga kila kitu hata maendeleo.Hawa "wanaume" wakiwasifia mnafurahi ila wakiwapa ukweli wenu mnawaita mabeberu, wanyonyaji, waizi...
Kwa hiyo unaamini kwamba serikali ya magufuli ni kigeugeu?Na wakikosoa watu kama nyinyi huja mbio mkifurahi na vi screen shot vyenu mnapongezana ila wakisifia sasa povu jingiiiii kama hivi...tulishawazoea pingapinga kila kitu hata maendeleo.
sio govt naongelea nyie pingapinga kila kitu...hasa ikisifiwa ..ila ikosolewa tu mnakuja mbio ...hahahahaha mama Tanzania..Kwa hiyo unaamini kwamba serikali ya magufuli ni kigeugeu?
sio govt ..
Umeuliza kwa niaba yangu mumuUtulivu wa namna gani huo?!
Pongezi kwa wananchi wanaokataa kudanganywa na wanasiasa wanaosaka kikiHongera pekee iende kwa vyama vya upinzani manake mengine yote yanayopoteza amani nchi zingine na Wapinzani wa Tanzania wanafanyiwa; lakini for the sake of amani yetu, wanaamua kutumia busara ili kutoivuruga nchi!
Maalim Seif amenyang'anywa ushindi mchana kweupe lakini badala ya kuwahamasisha wafuasi wa CUF kupigania ushindi wao; ndo kwanza akawahamasisha watulie!
Ni nani asiyejua hicho ni moja ya vyanzo vya uvurugikaji wa amani Africa?
Mbowe akaitisha UKUTA na watu wakahamasika! Lakini kwa kuchelea UKUTA ungevuruga amani; Mbowe aka-call off dakika za mwisho!!
Tanzania ni moja ya nchi chache sana Africa ambako, moja ya viongozi waandamizi nchini wanaponea chupuchupu kuuawa lakini bado viongozi wakuu wanawapoza wafuasi!!
Hongereni Vyama vya Upinzani na Wafuasi wenu manake pamoja na kwamba serikali imeoonesha dalili zote za kidhalimu na kupenda damu za raia wasio na hatia; nyie kwa busara zenu mmeepusha kutoa kafara ya damu za wanadamu kwa Mazimwi yala watu!
God bless Tanzania!
Kweli kabisa ndugu yangu... hoja yako naiunga mkono! Na pongezi zaidi hususani kwa wananchi wa MKIRU ambao, pamoja na ndugu na jamaa zao kupotea katika mazingira yakutatanisha huku ikihofiwa wameuawa na maafisa wa serikali lakini bado wananchi hao wameamua kuvuta subira!Pongezi kwa wananchi wanaokataa kudanganywa na wanasiasa wanaosaka kiki