Tanzania yakaribia kufunga kambi zote za wakimbizi nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yakaribia kufunga kambi zote za wakimbizi nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanaFalsafa1, Jun 21, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Na Jackson Odoyo
  SHIRIKA la kimataifa la kuhudumia wakimbizi nchini (UNHCR) linajiandaa kufunga ofisi zake nchini baada ya wakimbizi wote kuondoka katika kambi za kuhifadhi wakimbizi.

  Shirika hilo limefikia hatua hiyo baada ya zoezi la kurejesha wakimbizi katika nchi zao kuendelea vizuri.

  Akizungumza na Mwaandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya wakimbizi dunia inayoadhimishwa Juni 20 kila mwaka Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Yacoub El hillo alisema kambi hiyo itafungwa mara baada ya wakimbizi kuondoka.

  Maadhisho hayo yatatanguliwa na matembezi yatakayoanzia viwanja vya Mnazi mmoja hadi ukumbi wa Kareem Jee na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Laurence Masha.

  Mwakilishi huyo wa UNHCR nchini alisema baada ya kambi zote kufungwa ofisi pamoja na vifaa vyote vya kuhudumia wakimbizi zitakabidhiwa serikali ya Tanzania.

  Alisema kambi hizo zitafungwa kwa sababu suala la wakimbizi si la kudumu na wala haifahamiki ni lini wakimbizi watapatikana.

  “Hatuwezi kuendelea na kambi hizi wakati wakimbizi wamerudi kwao wala hatuwezi kusema kwamba huo ndiyo mwisho wa kuhudumia wakimbizi kwa sababu suala la wakimbizi linatokana na vurugu za kisiasa hivyo siku ya kupatikana kwao haifahamiki”alisema El Hillo.

  Alisema mwanzoni mwa mwaka 2007 kulikuwa na wakimbizi 300,000 kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na walihifadhiwa katika kambi 11 za Mikoa ya Kigoma na Kagera.

  “Leo hii tumebakiza wakimbizi 100,000 wanaohifadhiwa kwenye kambi tatu Mkoani Kigoma ambazo ni Mtabila ambapo kuna wakimbizi wa Burundi, Lugufu na Nyarugusu zenye wakimbizi kutoka Congo” aliongeza El Hillo .

  Kuhusu wakimbizi 220,000 waliokimbilia nchini mwaka 1972 na kuishi katika kambi za Ulyankulu, Katumba na mishamo katika mikoa ya Tabora na Rukwa, aliasema 40,000 kati yao walisaidiwa na UNHCR kurejea Burundi kwa hiyari mwaka 2008.

  “Mbali na jitihada hizo za UNHCR kurejesha wakimbizi hao nchini Burundi tumeandaa mikakati ya kurejesha wakimbizi wengine 15,000 ifikapo Oktoba Mwaka huu" El Hillo aliendelea kufafa zidi.
  Source:Mwananchi
   
Loading...