Duh! uchumi wenyewe wa kupigana vita ukowapi? vita ya Uganda tu zaidi ya miaka 30 na bado tunadaiwa na akina Ghadafi ingawaje wameshakufa...
Kwani Ghadafi alikuwa double agent wakati wa vita vya kagera...? Ninavyokumbuka ni kuwa alikuwa mshirika wa Amini...hadi wanajeshi wake walitekwa na akina mzee mti mkavu...wakafungwa vitambaa...busara ya Mwl Nyerere ilitoa msamaha...wale mamluki wakarudishwa kwao... Sasa iweze tuwe na Deni kwa Ghadafi??
Ujinga mtupu hakuna sababu ya kuwashitaki wamalawi, Tanzania inatakiwa ku-develop kwa nguvu ukanda wa ziwa upande wetu na kuweka vitega uchumi vya kukata na shoka kama vile usafiri wa majini katika vijiji husika, uvuaji wa kisasa kwenye eneo letu na kuweka kituo cha manoari za kivita kwenye eneo letu then tuone huyo kimburu anayetaka kuleta chokochoko. Actions speaks louder.
Wakati umefika kuondoa mizoga ya CCM.
Mkuu hatuwezi kushindwa. Kesi hii iko wazi mno ndo maana membe anakimbilia huko, wewe unafikiri yeye mjinga. Wote wanaozungumzia kesi hii wanasema Tanzania imesimamia kwenye sheria ya kimataifa, kwa maana kuwa ikiwa sheria ya kimataifa itatumika ushindi wa Tanzania uko wazi.
Malawi ndo maana wanakataa sheria ya kimataifa na kung'ang'ania wakoloni. Maana yake ni kuwa Malawi wameshapima nguvu ya kesi yao kwenye sheria za kimataifa wakaona haiwezi kushinda. Ndo maana hawataki kwenda huko na hawataki majadiriano. Wanasema ziwa ni lao, full stop. Wanasema hivyo sababu baba yao wa Taifa, Kamuzu Banda alishawaambia hivyo. Na walipooneshwa mkataba wanaodhani umewapa ziwa lote wakagundua kuwa kumbe mkataba ule hauwapi ziwa ndo kabisa wamezidi kuchanganyikiwa.
Ila wanasiasa wa Malawi wanajua kitu kimoja; atakayewaambia wamalawi kuwa ziwa lote si la kwao, yaani wamelichangia na Tanzania na Msumbiji, atakuwa amejinyima kura. Na siasa za malawi unazijua. Ndo maana kina Chiume baada ya kuona hoja zao ni dhaifu wameamua kugomea majadiriano. Kwa ujumla suala hili linachukua uzito mno kwenye siasa za Malawi. Hakuna mwanasiasa aliye tayari kuwaambia wamalawi kuwa msimamo wa Banda si sahihi.
you are contradicting yourself,do you realy understand the gravity of the words membe spoke during his budgetary presentation in the parliament?what about now?huko sio kumeza moto?Nahisi wewe ndo umemeza moto tena kaa la moto kwani unafikiri kwa kukurupuka na unaitaka nchi nayo ikurupuke. Membe fanya kazi, kila taasisi inamfumo, fuata mfumo unaokuongoza baba, tumekutuma kazi sio kukurupuka
Duh! uchumi wenyewe wa kupigana vita ukowapi? vita ya Uganda tu zaidi ya miaka 30 na bado tunadaiwa na akina Ghadafi ingawaje wameshakufa, yaani uchumi wa kuexport kahawa, tumbaku na chai tena ghafi wala sio processed ndio unajigamba kwamba utapigana vita? Hao wanajeshi tu wenyewe, mabuti na kombati zina viraka hamna hela ya kununua zingine itakuwa vifaru!
Sahau mambo ya vita hatuwezi, tumechoka sana tena sana, kwangu mimi bora hata walichukue hilo Ziwa kama ikibidi kuliko kuingia vitani, hailipi kabisa bado tuna mengine mengi tu akina Ziwa Rukwa, Natron, Tanganyika, Nyanza na hayo yote yana utajiri wa kufa mtu, ukienda Natron hapo kuna Magadi (soda Ash) ya kufa mtu, Tanganyika Mafuta ya kufa mtu, Ziwa Nyanza nao maji na samaki wa kufa mtu mito mikubwa ambayo karibu yote ipo ndani ya mipaka yetu kabisa mingine haikauki mwaka mzima akina Ruaha, Rufiji, Pangani n.k
Kushindwa kupigana vita hakuna maana kuwa tutoe sehemu ya nchi yetu kwa watu wanaosema kuwa hapo ni kwao! Huo ni woga usiokuwa na msingi tena ni kukosa uzalendo wa kuwajali watanzania wenzio. Hivi unafikiri hatima ya watanzania wapatao milioni moja wanaoishi mwambao wa ziwa hilo itakuwaje ikiwa watanzania kama wewe wataingia Ikulu? You can't be a coward, because you are poor!!
Vita ya Uganda ilitugharim sana, lakini unafikiria Maisha ya Watanzania waliouawa na Majeshi ya idd amin kule Kagera?? Hiyo gharama ni kitu gani kwa uhai uliopotea? Hiyo gharama ni kitu gani kwa uhai ambao ungepotea ikiwa tusingepigana ile vita? Tunacholipia hadi leo ni gharama ya uhuru na haki, na siku zote vitu hivyo vitapiganiwa na si kupewa bure.
Kwa kifupi tu ni kuwa Banda alishawaaminisha watu wa Malawi kuwa hata Ardhi yote ya Tanzania na Msumbiji iliyoko mwambao wa ziwa lile ni sehemu ya Malawi (Wilaya zote zinazozunguka ziwa Nyasa). Huwezi uka-give in kwa madai ya kipuuzi kama hayo eti tu kwa kuwa Tanzania tuna maeneo kibao - huko ni kukosa uzalendo. Kaangalie ukubwa wa China halafu ukaangalie kile kisiwa wanachogombania na Japan!!
Tatizo la mpaka ni tatizo la mpaka. Halina uhusiano na mlolongo huo wa mambo mengi tuliyoshindwa uliyoorodhesha. Vita haishabikiwi na hakuna anayeshabikia vita. Toka mwanzo nimesema approach ya Membe ni nzuri. Kama Malawi wanaamini wana "just cause" kwa nini wanaepa usuluhishi wa kimataifa? Vita ni silaha ya mwisho "when all fail" na huwezi kulalama tu eti kwa kuwa tumeshindwa hiki na kile kwa hiyo na hilo la mpaka hatuliwezi!!! No.
Malawi wamegomea majadiriano kwa sababu wameona hawawezi kushinda kwa majadiriano. Usuluhisho wa kimataifa hawataki. Kwa hiyo tuwaachie tu kwa sababu wanataka na kwa sababu tumeshindwa mengine mengi!!!
Kama wamegomea majadiliano huwezi jua ni nini kinawasukuma kwa nini hizi chokochoko zianze sasa hivi?
Raisi wa JMT ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na ambaye anajua hali ya nchi yetu vizuri kuliko mimi na wewe ameshasema hatuna uwezo wa kuingia vitani kwa sasa, na huo ndio ukweli mengine yote yanabaki kuwa hisia na hasira ambazo hazitusaidii, kwa hiyo kama unapinga hilo basi jipange umpindue Raisi upeleke majeshi vitani, vinginevyo kila kitu kinabaki kilivyo hatuna UWEZO WA KUPIGANA VITA
Hakukuwa na njia mbadala hasa baada ya wenzetu kususia kikao kilichopangwa kufanyika Dar 10-14 mwezi wa tisa.
Maadhimio ya Mzuzu yalikuwa ni kama hatutaelewana/kufikia mwafaka, basi kwa pamoja tungetafuta msuluhishi (nchi yoyote ya jirani Afrika) kisha nae akishindwa ndipo twende UN.
Sasa wao wamesusa hasa baada ya ujumbe wetu makini ulioongozwa na Mh B. Membe na Prof A. Tibaijuka kuwamwagia vielelezo lukuki kiasi chakuwaacha midomo wazi.
Sasa naamini haki ya kila mmoja itaamuliwa na jicho la dunia.