Tanzania yaanza kujenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro

elbarik

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
576
395
Rais wa Tanzania John Magufuli leo hii ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa awamu ya kwanza ya mradi mkubwa wa reli ya kisasa ya Standard Gauge ambayo hapo baadae itaunganisha nchi za Rwanda na Burundi pia.

Lakini katika awamu hii ya kwanza, ujenzi utakuwa wa reli yenye urefu wa kilomita takribani 300, ambayo itatoka jijini Dar es Salaam na kuishia mkoa wa jirani wa Morogoro.

Ni reli ya kisasa, na ya kwanza Afrika Mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nguvu ya umeme.

Reli hiyo itajengwa kwa awamu ya kwanza na kampuni kutoka nchi mbili, uturuki na Ureno kwa gharama ya takriban dola bilioni 1.2 za Kimarekani.

Reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba treni yenye kuvuta mabehewa 100 na kubeba mzigo wa mpaka tani 10000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa Malori 500 ya mizigo.

Mradi huu utaleta ahueni kwa wasafiri wa Dar es Salaam mpaka Morogoro ambpo wataweza kusafiri kwa mwendo kasi kwa saa 2 na dakika 50 pekee

Rais wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli katika sherehe hizo amesema kuwa Tanzania itanufaika kutokana na Mradi huu kwa maendeleo ya uchumi,

Hivi sasa Serikali ya Tanzania inaelekeza jitihada zake za ujenzi wa reli wa awamu ya pili yenye urefu wa kilometa 336 kutoka Morogoro mpaka Dodoma yalipo makao makuu ya nchi na tayari serikali ya Uturuki imeonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania kujenga sehemu hiyo.

Chanzo: BBC
 
Viashiria vya ufisadi hivi.....Reli ya Dar-moro ya nn wkt tayari kuna reli nyingine na kuna usafiri wa uhakikwa kwa njia ya barabara?
Kwa nn asifufue mashamba ya mkonge pale moro na kujenga kiwanda kwanza?
KWA NN HII SERIKALI NA VIONGOZI KUANZIA KIONGOZI MKUU HAWAJUI PRINCIPLE HATA MOJA YA UCHUMI? TUMEROGWA NA NANI?
 
Icho ni kitu tofauti kabsa unazungumzia apa...
 
Viashiria vya ufisadi hivi.....Reli ya Dar-moro ya nn wkt tayari kuna reli nyingine na kuna usafiri wa uhakikwa kwa njia ya barabara?
Kwa nn asifufue mashamba ya mkonge pale moro na kujenga kiwanda kwanza?
KWA NN HII SERIKALI NA VIONGOZI KUANZIA KIONGOZI MKUU HAWAJUI PRINCIPLE HATA MOJA YA UCHUMI? TUMEROGWA NA NANI?
Principle ya uchumi c ndio hyo ya kukuza uchukuzi( infrastructure development)
Hayo mambo ya viwanda na mashamba yabaki private sector.
 
Viashiria vya ufisadi hivi.....Reli ya Dar-moro ya nn wkt tayari kuna reli nyingine na kuna usafiri wa uhakikwa kwa njia ya barabara?
Kwa nn asifufue mashamba ya mkonge pale moro na kujenga kiwanda kwanza?
KWA NN HII SERIKALI NA VIONGOZI KUANZIA KIONGOZI MKUU HAWAJUI PRINCIPLE HATA MOJA YA UCHUMI? TUMEROGWA NA NANI?
Anasema yeye anajiamini na hapangiwi nini cha kufanya, alafu huwa najiuliza tumewahi kua na Rais aliyekuwa anapangiwa kitu cha kufanya? au tumewahi kuwa na Marais wanaopokea ushauri na kuufanyia kazi?
 
Back
Top Bottom