Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,510
- 7,755
Bila shaka sasa Tanzania mpya iliyokuwa inameremeta kwa ujenzi wa viwanda kila kona ya nchi, sasa imegeuka kuwa Tanzania ya ujenzi wa vituo vya mafuta kiholela na kila sehemu!
Sheria inataka ujenzi wa kituo cha mafuta uwe mita 500 kutoka kimoja hadi kingine lakini sheria hii haifuatwi tena. Kuanzia mwaka 2021 vituo vya mafuta vinaota kama uyoga kwenye nchi yetu. Swali la kujiuliza kimetokea nini?
Mkoa wa Pwani ulikuwa unaongoza kwa ujenzi wa viwanda vingi sana lakini sasa hivi wakifanya utafiti upya watakuta unaongoza kwa ujenzi holela wa vituo vya mafuta.