Tanzania ya Viwanda - mchawi ni mamlaka za serikali

Tanzania ya Viwanda - mchawi ni mamlaka za serikali

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Kwa viongozi wetu wa juu nchini watendaji serikalini na wanasiasa kwa jumla, msemo wa viwanda hauwatoki midomoni kila wanapopata fursa katika majukwaa.

Kimsingi msemo huo hauwezi kuwatoka kwa sababu wao ndio wadau wa kwanza kama watoa dira kuelekea Tanzania ya viwanda.

Hata hivyo ili tufikie kwenye maono hayo ya viongozi wetu kuhusu viwanda, tunahitaji kubadili fikra kutoka kuwa Taifa la walaji na wachuuzi hadi Taifa la waanzisha viwanda wa kutengeneza bidhaa.

Viwanda tunavyovipigia debe kuwa vijengwe kwa mamia na hata kwa maelfu kila kona ya nchi havitatokana na wawekezaji wa nje pekee.

Utahitajika mchango na ushiriki madhubuti wa Watanzaia wenyewe katika kuanzisha viwanda vya aina mbalimbali. Viwanda hivi havitaanzishwa kama mtazamo utaendelea kuwa uleule utokanao na fursa za kuwa walaji na wachuuzi pekee.

Kwa mfano kwa nini Watanzania wengi waishie kuuza matunda magengeni na sokoni lakini washindwe kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vya kusindika matunda hayo wakajihakikishia tija zaidi?



Tuna mfano mzuri wa namna hivi sasa Watanzania kwa makundi wanavyochangamkia fursa kwenye kilimo lakini wengi utakuta ama wanalima au ni wauzaji wa bidhaa zitokanazo na kilimo.

Tunachokosa ni ule uthubutu wa kuongeza thamani kwa bidhaa hizo na mwishowe kuzipeleka sokoni kama bidhaa tofauti na zilivyokuwa awali.

Tunaamini kama Watanzania tutaukumbatia uthubutu wa kuongeza thamani kwenye bidhaa mbalimbali za kilimo na ufugaji tutapiga hatua kubwa katika mchakato wa uanzishwaji wa aina mbalimbali za viwanda nchini.

Hata hivyo, tunapopiga chapuo mabadiliko haya ya kimtazamo na kifikra kwa Watanzania hatuna budi kuzipa neno Mamlaka kama Wizara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Mamlaka nyingine za Serikali

Uzoefu unaonesha baadhi ya vyombo hivi zinarudisha nyuma juhudi za Watanzania wanaojaribu kujijongeza. Hii ni kwa sbabu ya kuwapo kwa taratibu na masharti yasiyo rafiki.

Kwa mfano leo ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuanzisha kiwanda kidogo cha kusindikiza matunda. Anayejaribu atakumbana na mlolongo wa masharti ambayo mwishowe yatamkatisha tamaa.

Bado Mamlaka zetu zina mtazamo wa kiwanda kwa kuangalia ukubwa wa ardhi anayomiliki mwekezaji au jingo linalitumika kuzalisha bidhaa.

Ni kosa kwa mtu kuanzisha kiwanda kidogo ndani ya ua wake kwa sababu tumejiaminisha kuwa kiwanda hakiwezi kuwa ndani ya nyumba ya mtu.

Lazima tukubali kuwa miaka mingi ya uhuru Watanzania hatuna budi kuwa watu tunaoweza kujitafutia chakula, kukipika na kukiandaa mezani. Vinginevyo kuendelea kuwa walaji na wachuuzi wa bidhaa zinazotengenezwa na wengne, tukubali kuwa wategemezi wa kudumu wa maendeleo katika dunia hii ya ushindani.

Kuna katazo tena la kimaandishi kama ifuatavyo:-
1. Ni kosa kutangaza bidhaa yoyote kwa njia yoyote ile pasipo kusajiliwa na mamlaka husika. Jiulize bila kutangaza bidhaa yangu kwenye hatua za awali nitakuwaje na msukumo wa kuiendeleza na kuisajili?

Mfano mdogo tu; mtoto wangu aliugua upele ambao ulikuwa haumuwashi, niliangaika kwenye hospitali, maduka ya dawa pasipo kupata suluhisho. Nikakutana na mama mmoja mmasai nikamweleza tatizo la mtoto wangu, akanipatia mafuta ya atermisia. Haikupita hata wiki mtoto akapona kabisa.
Nawiwa kutangaza hayo mafuta ya atermisia lakini NI KOSA KUTANGAZA. Hivi huyo Mmasai ni lini atamiliki kiwanda cha mafuta ya atermisia kama hawezi kutangaza ili apate wateja wa mafuta hayo?
TAFAKARI.
 
Back
Top Bottom