Tanzania ya viwanda kwa watanzania material

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
388
Reaction score
666
aa994d2f8f265b9b1747ebf99acb3923.jpg

Hii Tanzania mpya ya ndugu Charles Mwijage
Tanzania inayo pewa sifa kedekede yakujikomboa kutoka nchi Maskini nakuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati

Tanzania ambayo watu wake hawajawa tayari kuwa sehem ya uchumi endelevu

Tanzania ambayo huvithamini vitu vilivyotengenenzwa nje ya Tanzania nakuvibeza vitu vilivyotengenezwa na wananchi wake,

Tanzania ambayo viongozi wake hujiona nadhifu kwa kuvaa suti kutoka London na kuyadharau mavazi yenye ulua wa kitanzania

Tanzania ambayo budget yake ya ujenzi hutumika kwa kulipia 70% wakandarasi wa nje ya Tanzania kama China, Japan, Italy, Misri, Turkey, South Africa n.k huku makampuni ya ujenzi ya Tanzania yakikosa Tender nono ambazo serikali yao huzitoa kwa makampuni hayo ya kigeni

Tanzania ambayo huzalisha pamba kwa wingi lakini bandari yake ikitumika kusafirisha pamba hiyo India

Tanzania ambayo inasifika kwa idadi kubwa ya mifugo lakini ikiwa haina machinjio za kisasa katika miji yake mikubwa

Tanzania ambayo huzalisha ngozi kwa wingi kutokana na idadi kubwa ya mifugo iliopo lakini haina viwanda vya kisasa vyenye uwezo wakuzalisha bidhaa zenye ubora kutokana na ngozi

Tanzania ambayo viongozi wake nao huishi kwa kulalamika katika majukwaa huku hali ya maisha ya watanzania walio wengi yakizidi kuwa duni kutokana na Sera za viongozi wao kutokuwa na mwarubaini wakuwatoa katika umasikini uliobobea

Tanzania ambayo husifika kila mahara kwa ushiriki wake katika ukombozi wa Africa lakini ikishindwa kumkomboa mtanzania kutokana na umaskini, maradhi, elimu duni, utawala bora,

Tanzania ambayo huwasifia viongozi wake kwa uchapa Kazi huku rai wakawaida akiteseka kwa kukosa Huduma Muhimu katika maisha ya kila siku huku vyombo vya Dora vikishindana kuwafurahisha watawala badala ya kuwalinda raia wa hali ya chini

Tanzania ambayo wasomi wake hujikita zaidi katika mambo ya siasa kuliko uvumbuzi mbalimbali kutokana na fani zao.

Tanzania ambayo wananchi wake hawana uhakika na uhai wao kutokana na Huduma za afya kuwa duni na ukosefu wa madaktari katika hospital za uma huku viongozi wao wakiwatoa sadaka madaktari katika nchi jirani za Kenya, Uganda, na Botswana

Tanzania ambayo hujisifu kuwa na viwanda huku bidhaa zake nyingi zikikosa ubora ambao unahitajika katika soko

Tanzania ambayo bidhaa bora ni bidhaa za Mitumba kutoka ulaya huku nchi ikikosa sheria yakuzuia bidhaa zilizotumika kuingizwa nchini matokeo yake kila mtanzania nikuvaa nguo chakavu viatu chakavu, boxer chakavu, bukta chakavu, kila kitu kuwa chakavu hadi mambo Muhimu kama pembejeo za kilimo kuletwa zikiwa chakavu

Tanzania ambayo viongozi wake hujigawia Mali za uma kama Mali za urithi wa baba zao, Hujigawia ardhi huku wakiwaacha raia maskini wakikosa ardhi zenye rutuba, hujigawia nyumba zilizojengwa na serikali huku raia maskini nyumba zao zikibomolewa kwa kupisha ujenzi wa mabarabara ambayo hayana tija na raia wakawaida

Hii ndio Tanzania yangu niipendayo.
 
Sasa tufanye nini,maana umeniacha kwenye muning'inio wa mada.
 
Kwa kuyaona haya, utagundua watanzania wenyewe ndio chanzo cha hali zao ngumu
 
Back
Top Bottom