Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,141
- 1,982
Heshima Kwenu,
Serikali yetu imejiapiza kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda itakayosababisha tuwe na uchumi wa kati.Ni malengo mazuri.Lakini fikiria haya;
Kiwanda cha Viuadudu Kibaha kilichojengwa kwa mkopo wa dola za Kimarekani milioni 22.307 na gharama za mkopo asilimia 11 kwa miaka kumi, hakijapata kuuzia serikali bidhaa hii muhimu. Serikali imetoa Sh. 2.1 bilioni kwa kiwanda na kimekopa toka mabenki Sh. 4.55.
Kiwanda hiki kimezalisha lita za dawa 100,000 mpaka Februari mwaka 2017 ambazo zimeuzwa Niger kwa Sh. 1.012 bilioni. Wizara ya afya haijatenga fedha kwa ajili ya kununua dawa ya kuulia mbu wanaoeneza malaria inayoongoza kwa kuua watu wengi. Kiwanda hakijapata soko Tanzania. Kitajiendesha vipi?
Kiwanda cha TANELEC cha Arusha kinazalisha transfoma ambazo mtumiaji wake mkubwa ni TANESCO. Ni ajabu kuwa Shirika letu la umeme linanunua transfoma zinazozalishwa hapa nchini nje ya nchi! Sababu, taratibu za manunuzi. Wateja wa transfoma zetu ni Kenya, Uganda, Zambia na Msumbiji.
Serikali inatakiwa kuhakikisha viwanda vya ndani vinapata fursa katika soko la ndani. Ikifaulu hapo ndio ijikite kuanzisha viwanda vipya.