Tanzania ya uchumi wa kati yaanza kunukia

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
“TANZANIA ya Magufuli, itakuwa ya viwanda,” hiyo ni kauli aliyokuwa akiisema mara kwa mara Rais John Magufuli, wakati akijinadi wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Watanzania baada ya kumchagua Magufuli kuongoza nchi yetu, serikali yake imeanza kuweka mipango thabiti ya kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati. Hayo tumeyaona kwenye bajeti zinazoendelea kuwasilishwa bungeni mjini Dodoma. Moja ya vitu vinavyoonesha nia hiyo ya serikali ni Bajeti ya Nishati na Madini kujielekeza zaidi katika umeme pamoja na Mpango wa Pili wa Maendeleo ambao ni sehemu ya Mpango elekezi wa miaka 15 unaolenga kuifikisha nchi yetu kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji nayo imetoa picha namna nchi inavyohamasisha sekta binafsi kuchukua hatamu za kupeleka viwanda vikubwa na vidogo katika kila sehemu ya nchi yetu.

Moja ya changamoto zinazofanyiwa kazi na Serikali kwa upande wa viwanda ni baadhi ya viwanda vilivyobinafsishwa kuwa na utendaji unaosuasua. Waziri mwenye dhamana ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, anasema kati ya viwanda 106 vilivyofanyiwa tathimini, viwanda 45 vinafanya kazi, 24 vinasuasua na 37 vimefungwa. Anasema kuna viwanda vingine 35 ambavyo vimebaki ambavyo vitafanyiwa tathimini ili kujua hatma ya viwanda hivyo.

Mpango wa Pili wa Maendeleo Mpango wa kwanza wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2011/12-2015/16 unafikia ukomo mwezi huu wa Juni na kutoa nafasi ya kuanza kwa awamu ya pili. Mpango wa kwanza wa maendeleo umefanikiwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo nishati, miundombinu, huduma za jamii, kilimo, maendeleo ya rasilimali watu pamoja na uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha. Mpango wa pili wa Maendeleo umejikita zaidi katika maendeleo ya uchumi wa viwanda na rasilimali watu.

Akiwasilisha mpango wa pili maendeleo wa miaka mitano Bungeni, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango anasema, kiasi cha Sh trilioni 107 kitatumika kugharamia mpango na miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka 5 ijayo, sawa na wastani wa Sh trilioni 21.4 kila mwaka. Anabainisha kuwa Serikali itachangia Sh trilioni 59 katika mpango huo, sawa na wastani wa Sh trilioni 11.8 kila mwaka ili kufanikisha jambo hilo.

Sekta binafsi inatarajiwa kushiriki kikamilifu ili kufikia azma hiyo. Msingi wa uchumi wa viwanda Mosi, mpango huo umelenga kukuza uchumi na kujenga msingi wa uchumi wa viwanda. Mpango huu utaleta mapinduzi ya kilimo ambayo yatachochea maendeleo ya watu na viwanda. Waziri Mpango anasema hii ni fursa kwa wananchi na wawekezaji binafsi kuchangamkia sekta ya kilimo ambayo pia imekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa na kutoa ajira kwa wananchi wengi zaidi.

Pili, mpango umelenga kufungamanisha maendeleo ya uchumi na maendeleo ya watu. Ili uchumi ukue vizuri ni vema kwenda sambamba na maendeleo ya watu. Mpango huu umelenga kupanua fursa za upatikanaji wa elimu bora kwa watu wote itakayowezesha mwananchi kujiajiri au kuajiriwa. Vilevile, umejikita katika kuimarisha afya za wananchi ikijumuisha huduma za matibabu, usalama wa chakula na upatikanaji wa viini lishe vya mwili, maji safi, mazingira safi ya kuishi na hifadhi ya jamii.

Tatu, Mpango umelenga kujenga mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji kwa kuimarisha mifumo ya kisheria ili iwe rafiki katika kuvutia wawekezaji, ikiwa ni pamoja na kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme, miundombinu ya reli, barabara, bandari, usafiri wa anga na majini pamoja na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama). Nne ni kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa mpango, hatua inayohusisha kutanzua vikwazo vya utekelezaji na kuimarisha usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya mpango.

Kiwanda cha mbolea Mbunge wa Babati Vijijini, Jitu Soni, anapendekeza kuwa ni muhimu Serikali ikawekeza zaidi katika kuendeleza sekta ya kilimo kwa kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea aina ya urea inayotokana na mabaki ya gesi, itakayouzwa kwa bei nafuu. Ili kuzalisha mbolea unahitaji kuwa na phosphate, calcium na madini mengine yanapatikana hapa nchini isipokuwa nitrojen inayotoka nchi za Uarabuni na nchi za Scandinavia.

“Kwa kuwa tunazalisha gesi na imesafirishwa hadi Dar es Salaam, kijengwe kiwanda cha kutengeneza nitrogen itakayotumika kwenye viwanda vya mbolea vitavyozalisha mbolea itakayokidhi viwango na bei rafiki kwa wakulima”, anasisitiza Soni. Aidha, anashauri kuwa pembejeo za kilimo zinazozalishwa na kuuzwa hapa nchini zikiwemo mbegu, zisitozwe kodi kama ilivyo kwa pembejeo za kilimo zinazoingizwa nchini kutoka nchi za nje, jambo ambalo anasema litapunguza bei na litasisimua ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya kilimo.

Uboreshaji miundombinu Anapendekeza uwekezaji mkubwa ufanywe katika miundombinu ya reli ikiwemo ya kati, reli ya kutoka Tanga, Kilimanjaro, Arusha hadi Uganda ambayo pamoja na kusafirisha abiria na mizigo yao, itumike pia kubeba shehena ya saruji na chokaa kwenda nchini humo. Anasema kuwa ili Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano uweze kufanikiwa, ni lazima sheria ya manunuzi ya mwaka 2014 ihuishwe ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali zinazopotea kutokana na kupandishwa kwa bei za bidhaa na huduma zinazohitajika na Serikali ikilinganishwa na bei ya soko.

Anabainisha kuwa sheria hiyo imekuwa kichaka cha kupoteza fedha za Serikali kutokana na vitendo vya rushwa na ufisadi wa baadhi ya watumishi wa umma wasio waaminifu. Vyanzo zaidi vya mapato Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Waitara Mwita Mwikwabe anashauri Serikali itafute ama itengeneze vyanzo vingi vya mapato na kuwaelimisha watu umuhimu wa kulipa kodi. Pamoja na hayo mfumo wa ukusanyaji kodi wabunge wanashauri serikali ihakikishe kila Mtanzania mwenye uwezo wa kulipa kodi alipe.

Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza anaona kwamba kuna ulazima wa Serikali kuboresha mifumo ya kodi na kuangalia upya suala la misamaha ya kodi ili kufunga mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali. Hata kwa yule asiyetoa kodi kwa namna moja au nyingine bado ana jukumu la kuisaidia Serikali kubaini wakwepa kodi kwa kutoa taarifa za wafanyabiashara wasio waaminifu na pia kudai risiti kila wanapofanya manunuzi.

Tatizo la ukwepaji kodi limekuwepo kwa muda mrefu ambapo hivi karibuni baada ya uongozi wa awamu ya tano kuingia madarakani, tumeshuhudia taasisi za Serikali na binafsi zikihusishwa na ukwepaji kodi ikiwemo upitishaji wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam ambapo makontena yalipitishwa bila kulipiwa kodi hivyo kupelekea Taifa kupoteza mapato. Hivyo basi katika mpango huu wa miaka mitano Serikali haina budi kuhakikisha kuwa mianya yote ya ukwepaji kodi inazibwa ili mapato yote ya Serikali yawe yanakusanywa ipasavyo.

Uamuzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanzisha matumizi ya mashine za kielektroniki (EFDs) kwa wafanyabiashara katika biashara zao itasaidia kuhakikisha kuwa Serikali inapata mapato stahiki. Hivyo basi, kama Taifa mpango huu ukitekelezwa vizuri kama ulivyowasilishwa utaleta mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa wananchi kwa kuwaongezea fursa za kuajiriwa na kujiajiri. Mwandishi wa makala haya ni ofisa habari Wizara ya Fedha.

Chanzo: Habarileo
 
Anataka atuhamishe katika mada ya msingi uyu, Jesca amefikaje chuo kikuu?
 
Kalulu unahangaika mno,uzi wa nne kwa asubuhi ya leo ni kusifu na kuabudu tu!
Ngoja nikwambie nilichoona,haiwezekani nyuzi zote hizo na kwa urefu wake uwe umeandika asubuhi!Hii inaonekana ni program maalum uliyokwishaifanya kwa siku kadhaa na leo ndioo unarelease hadithi zako!
Kazana huenda watu wakamsahau Jesca!
 
ASANTE TUMEAMKA......HAKIKA MWENYE ENZI MUNGU ASHUKURIWE!
 
zile bajet za zaid ya 70% matumiz ya kawaida 10% ukarabat 20% mirad ya maendeleo ndo unazozizungumzia.
 
Ujenzi wa viwanda una maana kubwa sana kwa nchi:
1. Kuongeza jira mpya
2. Kuokoa fedha za kigenia ambazo zingetumika kuagiza bidhaa ambazo zingeagizwa nje
3. Matumizi sahihi ya raslimali za ndani - value addtion of natural resources
Lakini,kama bidhaa zitakazotengenezwa na viwanda hivyo ni sawa na bithaa za ndani tu kwenye soko ambazo zimeagizwa nje impact ya viwanda hivi itakuwa ndogo kwa uchumi na manufaa kwa manufaa kwa wananchi
 
Bandiko refu sana lakini ukilisoma kwa umakini ni malengo ya muda mrefu sio leo ama kesho ama mwakani. Ni strategies za miaka kuanzia mitano na kuendelea, na ni ngumu kutekelezeka kwa kuwa mirija bado ni mingi mnooo.

Ni nini haswa kitatumika kiwashirukisha wazawa, sababu tunaongozwa na watu wanaoamini wazawa hawawezi chochote zaidi ya kuuza juice.
Mpango muafaka wa kumeza yote hayo ni kuwapa support wazawa katika project zao ili ziwe endelevu. Mfano bidhaaa ambazo ni za matumizi ya kila siku ya mwanadamu, kutokana na tabia nchi ya kwetu haya ingetosha kabisa kutimilizwa hapa ndani. Soko ni kubwa sana la ndani, tunaongelea watanzania zaidi ya milioni 50. Hatupaswi kufikiria makubwa kwanza ilhali haya madogo tuu ya ndani yametushinda.
 
Viwanda vya kuongozwa na akina jeska havitatusaidia kuondokana na umaskini, wataajiriwa majeska watupu na matokeo kwa taifa yatakuwa sifuri.
Turudi kwenye hili suala la ufisadi wa elimu lililoibuliwa na jeska na baba yake , likitatuliwa hilo ndio tuongelee viwanda.
 
Back
Top Bottom