maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Hivi sasa Tanzania iko ndani ya vita ya ajabu ya pande tatu. Kuna Clouds Tv wanaolalamikia kitendo cha mkuu wa mkoa Paul Makonda kuwavamia usiku akiwa na polisi na wanaodaiwa ni wanajeshi au TISS, uongozi wa Clouds umefungua kesi mahakamani.
Kuna upande wa pili wa waziri wa habari, sanaa na utamaduni Nape Nnauye aliyelaani kitendo hicho na hata kuunda tume ya watu watano kuchunguza tukio hilo. Waziri kasema hilo la kunajisi tasnia ya habari likimshinda atajiuzulu.
Upande wa tatu ni ule wa Rais wa JMT aliyewateua Makonda na Nape na rafiki wa Clouds kama alivyo Makonda. Yeye anamhimiza Makonda achape kazi maana yeye ndiye aliyemweka hapo alipo. Ana maana kwamba hana mpango wa kumwajibisha, na haoni kama alifanya kosa kuivamia Clouds ila kosa ni kwa wale wakazi wa Dar wanaomwandama kwenye mitandao.
Cha muhimu ni kwamba lazima mshindi apatikane katika jambo hili na lazima mshindi awe mmoja. Je ni nani atakayeshinda wenzie? Tuupe wakati nafasi.