Tanzania ya Magufuli na Kenya ya Kenyatta ziko katika Vita Baridi?

Rulleger

Member
Aug 29, 2015
84
60
Ni ukweli kuwa uhusiano wetu na Kenya haujawahi kuwa wa "mahaba" (tukitumia msemo wa Lowassa). Tumekuwa tukivumiliana kwa maslahi ya kiuchumi tangu enzi za mwalimu. Hata hivyo tangu awamu ya tano ianze uhusiano wetu na Kenya unatia mashaka na ni vema tukaongelea jambo hili objectively.

Mambo yalianza na Magufuli kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM. Ikaelezwa viongozi wa serikali ya Kenya walipata hofu kwa vile Magufuli ana urafiki na kiongozi wa upinzani.

Likaja suala la njia ya Bomba la Mafuta. Magufuli akaongea na Mseveni na kukawa na uwezekano mkubwa kuwa Uganda itachagua njia ya Tanzania badala ya Kenya. Suala hili halikuifurahisha Kenya hata kidogo. Kwa sababu ya ushindani wa njia ya bomba la mafuta wakati fulani waziri mmoja wa kenya na maafisa wake walizuiliwa uwanja wa ndege Tanga.

Jambo jingine la kuchekesha ambalo wakenya waliandika ni wakati wa mkutano wa marais wa EA ambapo Magufuli aliongea ki-luo mbele ya Kenyatta. Media ya Kenya ikachukulia ni kejeli kwa Kenyatta kwa vile rafiki wa Magufuli ni M-luo.

Tukio jingine dogo ni la binti wa rafiki mkubwa wa Magufuli kusema kuwa Olduvai Gorge iko Kenya. Media ya Tanzania ikalipuka kwa kulaani. Hii inatokana na historia ya Kenya kuitangaza Kilimanjaro kuwa iko kwao.

Katika mtazamo huohuo juzi wakati anafungua Daraja la Nyerere (Kigamboni) Rais Magufuli aliwasha moto mwingine kwenye media ya Kenya kwa kusema "wale wanodhani kila jambo jema liko kwao wameanza kuandika...walisema Kilimanjaro ni yao, Olduvai Gorge ni yao, n.k" . sasa hivi hii kauli iko katika headings za media za Kenya: "Magufuli fires shots...", "Magufuli hates Kenya with a passion"...n.k

Posts za wakenya kwenye blogs na online newspapers sio positive kama mwanzo wakati Magufuli kaingia madarakani. Watu wanatutukana. Wanauliza tuna nini zaidi ya Kiswahili na hili daraja la Kigamboni. Wanaona serikali ya Magufuli imedhamiria kuifanya Tanzania iwe Juu ya Kenya.

Kuna umuhimu viongozi wetu kwa makusudi wafanye bidii ya kuondoa hii hali ya vita ya maneno. Ile tabasamu Magufuli na Kenyatta wanaonyesha wakikutana iwe pia tabasamu kati ya watu wetu na media zetu.
 
ma bado, hadi waombe poa
 
Tanzania na Kenya zote ni nchi masikini.
Lengo la Tanzania kamwe sio kuwa mbele ya Kenya, hakuna ufahari kumpita masikini mwenzako.
Tunahitaji kuondoa hiyo mindset, social media zisitutoe kwenye Lengo..

NOTE: So far kinachotokea bado hakina hadhi ya kuitwa " vita baridi "
 
Wakenya ni watu wa ligi siku zote.

Kenya kunafukuta kila siku, hawako stable - imara. Si wamoja. Linapotokea suala na sisi wanarukia kuandika kwani kiasi fulani ndio huwaletea hisia za ukenya - umoja. Nje ya hapo ni uluo, ukikuyu, ukamba, utaita na mambo ya aina hiyo

Achana nao hao, msisahau, bado wanatamani ardhi yetu. Yao haiwatoshi

Tuna kila kitu, suala la muhmu ni kujipanga na kuweka utaifa na maadili mbele
 
Tanzania na Kenya zote ni nchi masikini.
Lengo la Tanzania kamwe sio kuwa mbele ya Kenya, hakuna ufahari kumpita masikini mwenzako.
Tunahitaji kuondoa hiyo mindset, social media zisitutoe kwenye Lengo..

NOTE: So far kinachotokea bado hakina hadhi ya kuitwa " vita baridi "

Tanzania ni nchi masikini ya daraja la mwisho kiuchumi wakati Kenya ni nchi ya uchumi wa daraja la pili. Kwahiyo Kenya wanatuzidi tusijidanganye tupambane tu kuwapiku uwezo tunao.
 
Lakini JPM as a president hakutakiwa kuongea yale mambo ya Kilimanjaro na Olduvai Gorge pale, ilikuwa inatosha kuwaachia mawaziri wapige vijembe, yeye angeendelea kuzungumzia daraja tu

Na hiyo ndio sifa ya upande wa pili wa Magufuli, kwamba hajiandai anakwenda kutoa speech gani na kwa parameters zipi, na kupenda kupigiwa makofi sana basi madadi humpanda na kumtoa nje ya mstari!
 
Hapa Kazi Tu...

Kama wanapata kichefuchefu watafune malimao. Walipata dezo miaka 10 ya Kikwete sasa miaka mitano ya JPM tunawakamata na miaka mitano mingine ni kuwafunika vibaya. Sio daraja na bomba tu, hata bajeti tumenza na asilimia 40 purely on development. Makusanyo yanaongezeka pia
 
Lakini JPM as a president hakutakiwa kuongea yale mambo ya Kilimanjaro na Olduvai Gorge pale, ilikuwa inatosha kuwaachia mawaziri wapige vijembe, yeye angeendelea kuzungumzia daraja tu
......hapo nakupa like, lakini si unajua kwenye chama chetu vijembe havikwepeki!!, sijui hata nani alianzisha mtindo wa vijembe, mm huwa nauona unawafaa watu wenye uwezo mdogo kifikra!!! Mh yy apige kazi, maana hapa ni kazi tu, yy yuko juu sana vijembe wapige kina Kisendeka! Baba Magu aendelee kupiga vijembe kwa kupiga kazi, naamini hapo msumari umeshawaingia, lakini wakenya hawajawahi kutupenda hasa katika nyanja za maendeleo hata hivyo!!! kwani alitaja au wamejishtukia tu!!!#HapaKaziTu, Viva Magu! Tutafika, Inshallah!!!
 
Haya mbona ya kawaida sana. Mbona kuna kipindi Watanzania walifukuzwa Kenya tukawaita manyangau lakini mambo yalienda vizuri tu? Cha msingi tupambane kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kujitangaza sisi wenyewe kimataifa! Balozi zetu ni za kutumbuliwa maana hawatutangazi ipasavyo!
 
Kawaida kiutendaji ama kimaamuzi huwezi wafurahisha watu wote. Wacha wapige mayowe wacha wayaone wenyewe.

But " ushaona wapi mtu anasukuma gari akiwa ndani" by lusungo wa JF
 
Lakini JPM as a president hakutakiwa kuongea yale mambo ya Kilimanjaro na Olduvai Gorge pale, ilikuwa inatosha kuwaachia mawaziri wapige vijembe, yeye angeendelea kuzungumzia daraja tu
Mkuu, JPJM alichofanya no sahihi kabisa jamaa hawa walikuwa wamezoa kutuchukulia kama mazezeta vile, nchi inakuwa na ubavu WA kutangaza vivutio vya kitalii vya Tanzania na kudai vipo nchini mwao hii ni hujuma kubwa lakini kutokana na upofu wetu sisi hilo hatulioni -Mabalozi wetu wanaona matangazo hayo kwenye media za magharibi wanakaa kimya badala ya kuichukulia Kenya hatua kali kisheria sambamba na kutoa a press release kwenye media za magharibi kukanusha vikali ulaghai WA Kenya.

Kwa bahati mbaya Balozi zetu zimelala usingizi - Tanzania kama nchi tunapashwa kubadirika kifikira na tuwe aggressive tuachane na masuala ya kuwa as a meek as a lamb - traits zetu hizo zimetu cost sana kimaendeleo, ndio maana majirani zetu utuchukulia for a RIDE.
 
Tanzania ni nchi masikini ya daraja la mwisho kiuchumi wakati Kenya ni nchi ya uchumi wa daraja la pili. Kwahiyo Kenya wanatuzidi tusijidanganye tupambane tu kuwapiku uwezo tunao.
achana na data za kupikwa za IMF kenya ni kama Tanzania tu interms watu wanavyoishi
 
Back
Top Bottom