Kwa bahati mbaya sana mi si muhumini wa utumiaji mbaya wa rasilimali za nchi, inawezekana lengo la mwalimu na timu yake lilikuwa sahihi soon after independence, ikiwa ni ishara kuwa sasa tuko huru!dhana na mantiki ya mwenge kwa miaka ya sitini na sabibi hadi themanini katikatika ilikuwa sawa lakini dhana ya sasa si dhana ya kuserve madhumuni ya mwenge!raiti tungekuwa na watu wenye uwezo wa kungamua mambo nadhani tungekaa chini, tukafanya kitu kinaitwa cost and benefit analyis then tukaja na jibu la kweli kama gharama tunayotumia kukimbiza mwenge nchi nzima ni sawa na faida tunayoipata.
,
mwenge ulikutumika kuhimiza uzalendo, kuhimiza uwajibikaji, kueneza ujumbe juu ya athari za rushwa, lakini tunapokaa leo na kuhubiri mwenge mantiki yake ni nini make rushwa inaongezeka, ufisadi ndo wimbo na kanisa la matajiri kwa sasa wanaojiita wanasiasa ambao kipindi cha mwalimu ilikuwa ni ajabu kuona mwanasiasa ni tajiri, angalia uzalendo uko wapi?kila siku unashuka, angalia matumizi ya nchi yanakuwa makubwa kuliko mapato hadi tunakopa kulipa mishahara< mikataba ya nchi imekuwa siri kubwa hali wadau wa mikataba ni wananchi wenyewe!,
,.
ubabe umeongezeka kodi zetu zinatumika na hakuna mtu anayeruhusiwa kuhoji, tumeona kwenye mtikisiko wa uchumi, ambao waziri wetu wa fedha bwa mkulo aliuhakikishia umma kuwa Tanzania hatutaathirika lakini kinachoendelea mi nadhani watanzania wanaweza kusema hata waliosoma political science wanalijua hili, ninachotaka kusema ni pale serikali ilitoa stimulus package kwa makampuni fulani ili yasifirisike lakini wabunge walipohoji serikali ilisema ni siri ingawa ni pesa za wanachi zilitumika!
,
tunazo rekodi nyingi zinazoonesha kuwa hatuna haja ya kuendelea kuushikiria mwenge sema tungetafuta njia mbadala ya kufikisha ujumbe uliolengwa kusambazwa kwenye mbio za mwenge!kwani tuna wanafunzi wengi hawana madarasa ya kutosha, hamna walimu, hamna vitendea kazi, hamna madawati ya kutosha, hospitali nyingi na zahanati za serikali zimebaki na panadol, nadhani hii ni kukosa dira ya ukweli, tumekosa mtu wa kudefine njia sahihi ya nchi hii, tumebaki na wanafiki, wabinafsi, na mafisadi, waliona sifa za utawala 100% na kukosa sifa za uongozi 100%
.
tufike hatua tuamue wenyewe na tuseme kuwa tumechoka kuburuzwa na tumechoka na matumizi mamabya ya rasilimali za nchi hii!changa kimaendeleo ila kubwa kiumri.
naomba niishie hapa.