Tanzania ya Inayotegemewa ni baada ya Miaka 10

Kinaeleweka

Senior Member
Nov 10, 2014
145
104
Salaam Aleykum! Tumsifu Yesu Kristo!

Ndugu zanguni,mie nikiwa mzalendo na mpenda amani wa Tanzania kwa tabia zetu zilivyo basi nachelea kusema Maendeleo ya kweli ya Tanzania ni baada ya miaka 20 ijayo kutokana na sababu zifuatazo:

1.Ujinga, Tatizo hili bado lipo miongoni mwa Watanzania na hivo kushindwa kutambua nini viongozi tuliowapa dhamana ya kulinda rasilimali zetu wanafanya.

Nashukuru uwepo wa shule za kata kwani ingawa zinazalisha div.zero na four nyingi zaidi lakini zinapunguza hili tatizo la Ujinga kwa kiasi kikubwa na hasa vijijini.

2.Umeme,tunashukuru jitihadi zinazoendelea kufanywa na wabunge mbalimbali kuhakikisha umeme unawafikia Mwananchi.Ni kupitia huu Umeme ndipo waliopo vijijini wataendelea kutambua madudu wayafanyayo viongozi waliowapa dhamana kupitia Luninga zao na hivo kutofanya makosa ktk uchaguzi wa chama na kiongozi anayefaa.

3.Mahudhurio ya Jeshi kabla ya kujiunga na Vyuo.
Hili pia linazidi kuwaimarisha vijana na kuwaondolea uwoga pindi wanapotaka kudai haki zao za msingi Kwa kufuata sheria bila kutishwa.Hali ambayo Ni tofauti sana na sasa.

4.Kujitambua.Hii pia itaongezeka sana baada ya miaka 10,tofauti na sasa.Kujitambua hapa inamaanisha ni ufahamu wa maamuzi sahihi ya kuchukuliwa inapobidi.Kwa mfano umuhimu wa kwenda kupiga kura,kumwajibisha kiongozi anayeenda tofauti na katiba n.k.

5.Katiba,Ikiwa ndo dira ya taifa lolote lile inapaswa kujari maslahi ya nchi na wananchi wake.

Katiba inayopendekezwa ni Kwa manufaa ya wachache na ambayo Ni Mafisadi.Ainiingii akilini kiongozi na mwananchi mpenda Taifa lako ukaipigia debe katiba ambayo haipendi kuona Viongozi wake Wanawajibishwa na tena wasio na kikomo cha uongozi.
Hili pia tumelishuhudia Jana tu toka Kwa Mkuu wa nchi namna alivojitahidi kuwalinda Mafisadi wenzake bila aibu yoyote.
Na ndiye anayeipigia debe hii katiba Pendekezwa iweze kupita.Katika hili Watanzania wa miaka 10 ijayo hawataweza kuruhusu ujinga huu.

6.Vifo.
Hakuna mtu yeyote aliye na amani na Furaha anayependa kufa.Lakini waumini wa dini tu naamini kuwa kifo ndo njia pekee ya kivuko cha am a kwenda Kwa Mungu Baba au Kwa shetani.

Hili taifa letu pia liweze kufikia maendeleo na demokrasia ya kweli basi Watanzania wengine tunatatakiwa tufe.

Faida ya kifo hapa Ni pale 5% ya wazee tulionao kwa sasa ikapungua( kutokana na sensa ya watu na makazi ya hivi Karibu ni kuwa 80% Ni vijana, 5% ni wazee na iliyobaki Ni watoto.)
Wazee wengi wamekuwa hawataki kuibadilisha chama cha Mafisadi Kwa madai kuwa Ni cha Nyerere na pengine woga wa mabadiliko.

Kwa hayo yote,baada ya hiyo miaka Mkuu wa nchi hawezi akaleta upumbavu na dharau kama aliouonyesha Jana Kwa Watanzania na akawa na Amani kama alivokuwa anataka.

Bunge litakuwa na nguvu zaidi kusimamia matatizo ya wananchi.

Katiba inayopendekezwa Kwa kuwa ni Kwa manufaa ya wachache Mafisadi haitapita hata kama Watailazimisha sana lakini tutakuja kuipata katiba ambayo itaridhiwa na wote.

Watanzania tutaanza kufanana na raia wa mataifa mengine duniani yaliyoendelea japo kimtazamo wa kidemokrasia katika kudai haki pale unapoonewa.

Nawakilisha pulizii!!
 
Back
Top Bottom