Tanzania Vs Egypt | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Vs Egypt

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kamanzi, Feb 1, 2011.

 1. k

  kamanzi Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kwa wale wanaoshuhudia mapinduzi yanayoendelea pale Egypt watakubaliana na mchanganuo ninaokwenda kuuelezea hapa chini. Kwa kifupi matukio yanayoendelea nchini Misri yanaonyesha kuwa Tanzania na Egypt kuna mambo yanayofanana sana ila reactions zetu ni tofauti:

  MAMBO YANAYOFANANA:

  . Jumla ya watu wanaoshindwa kupata ajira katika nchi hizi mbili inazidi kuongezeka
  .Mfumuko wa bei za bidhaa na huduma za jamii umekuwa mkubwa haswa kwa kuzingatia ukubwa wa mfumuko mkuu wa bei (inflation)
  . Kama Tanzania ilivyoanza na mwana mapinduzi Nyerere, Misri nao walikuwa na Nasser.

  TOFAUTI KUBWA BAINA YA NCHI HIZI MBILI:
  1. Uhuru wa habari: japo Tanzania tunajigamba tuna uhuru wa habari, Misri imeonyesha kuwa nao zaidi. Sahau habari ya kutimuliwa El-Jazira na kuondolewa kwa mitandao ya kijamii kama facebook, bila ya Misri kuruhusu 24 hours coverage ya matukio, kusingekuwa na maandamano. Kule kuwepo kwa coverage kuliwafanya mapolisi na hata wanajeshi kutenda kwa taadhari maana walijua dunia inawatazama. Kama katika mauaji ya Arusha kungekuwapo na BBC, CNN, Al-JAzeera na wengineo, CCM isingeweza kuruhusu mauaji ya kinyama vile.

  2. Polisi wanajua kazi yao Misri: Nafahamu polisi wanachukiwa Misri na duniani kote. NAfahamu pia wamisri waliwafukuzilia mbali mwanzoni mwa uprising. Lakini tumejifunza nini? Mara tu baada ya polisi kuondoka, wizi na matukio ya kihalifu yaliongezeka Misri nzima. Fananisha na Arusha ambapo walipokuwepo polisi mauaji na fujo vilitokea ilhali walipoondoka, amani na utulivu vilitawala. KWa kifupi polisi Tanzania ndio majambazi wenyewe.

  3: Wanajeshi wa Misri wanajua kazi yao: TAngu polisi wa wakimbie mitaa Misri (japo sasa wamerudi) wanajeshi wameingia mtaani. Lakini wanajeshi hawa wanachofanya ni kulinda maeneo rasmi ya serikali na sio kuingilia siasa. Watu wamewapenda na kuwakumbatia maana wanajua mipaka yao ya kazi. Fananisha na Tanzania ambapo mnajimu mkuu wa jeshi aliita press conference kabla ya kupigwa kura Tanzania akisema "lazima watanzania wakubali matokeo". Hii inaonyesha si tu jeshi la Tanzania linaingilia siasa za nchi, bali ni kibaraka wa CCM

  4. Dini haichanganywi na siasa nchini Misri: Kumbuka kuwa Hosni Mubarak ni muislamu pure. Lakini punde alipoonekana ni fisadi na dictator, wakristo kwa waislamu nchini Misri walijiunga kwa pamoja kutaka kumtupilia mbali. Fananisha na Tanzania ambapo Fisadi Kikwete anaendelea kupata support ya waislamu karibu wote kisa tu ni muislamu mwenzao. Waislamu wanadanganyika kuwa ufisadi wa Kikwete haupingiki kisa tu ni muislamu mwenzao. Wasichojua ni kwamba Kikwete anawatumia kwa faida yake mwenyewe. Hivi ndugu zangu waislamu mnafahamu kuwa Sheikh Mkuu anachaguliwa kwa kupandikizwa na TISS kwa ushauri wa CCM. Nyie endeleeni kulala

  5. Mafisadi Misri wanaanza kuhama: Kutokana na uprising, watoto wa Mubarak pamoja na mafisadi wengine wote wameshakimbia nchi ya Misri. Fananisha na Tanzia ambapo akina Rostam, Lowassa, Chenge na wengineo bado wanakula bata wakisubiri share yao ya DOWANS.

  6. Katika kupambana na ufisadi, vyama vya kisiasa na makundi ya kijamii Misri wameungana: Fananisha na Tanzania ambapo CUF, NCCR, TLP, Zitto Kabwe na wengineo wapo upande wa CCM na ufisadi ili kuipinga CHADEMA chama pekee cha Mapinduzi nchini Tanzania.

  Tunajifunza nini katika yote haya? Nini muafaka wa Tanzania? Na ninani atakataa nikisema Tanzania imelaaniwa?
   
 2. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  yeah, nimekusoma mkuu.
   
 3. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,228
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono...ila angalizo langu naliweka upande wa kucomment with reference to dini....mbali na hapo pengine umemulika vyema!
   
 4. n

  niweze JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Vitu ni vile vile. Mubaraka amekaa madarakani miaka 30 na CCM imekaa madarakani miaka 50...Yupi mbaya hapa? Ni bora kuishi Egypt then. Wananchi wa sehemu hizi zote hawana uhuru wa kupiga kura na kila wanapo kwenda kupiga kura wanakuta kitu kinaitwa NEC chombo cha kuchakachua kina badilisha matokeo. Ukiangalia ajira za vijana katika nchi hizi mbili utaona huko Egypt hakuna kazi kama Tanzania, wanafunzi wanalala wakisoma kwa bidiii ili elimu iwaokoe kimaisha na familia zao vijijini wakati Rostam anasuka mipango ya kuwakata shoka kwa kusuka deal za kuua uchumi wa Taifa. Mikataba inasukwa na viwanda vinataifishwa na kuuzwa kwa wawekezaji kumbe ni hao hao wakina JK/Lowasa/Mkapa hio hio CCM. Uchumi utajengwa vipi wakati wao wanataka vya bure? Matatizo ya Mubarak yanafanana kabisa na ya Kikwete hapa Tanzania. Tunacho kifanya ni kumpa fundisho mwezi huu JK/Pinda kwamba Watanzania wote tunakwenda mitaani kushikana mikono kwa amani na tunataka waondoke madarakani.
   
 5. P

  Pokola JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kipenga kikilia tutampeleka mfalme Golgota, tukamsulubishe. Kachangia sana sisi kuwa mashokoa kama tulivyo.:sick:
   
Loading...