Tanzania tunaliona hili la Corona, tunajipanga?

kashibaba

Senior Member
Nov 26, 2019
191
269
Wadau salaam kwenu,

Naamini sote tunaliona hili la Corona Virus kusambaa nchi nyingi sasa na China wenzetu wanaendelea kuona vifo vikiongezeka, na tayari imetangazwa kuwa ni Janga la Dunia. Naelewa Wizara ya Afya wana kitengo cha magonjwa ya mlipuko/ dharura, tumejipangaje kudhibiti hali hii ikiwa hata dawa za tiba still hakuna kwa sasa?

Wengine wamezuia watu wao kwenda China au mashirika ya ndege yao kizuia kwenda China, sis tunajipangaje kama taifa?

Tunaomba Mungu atunusuru na jambo hili kama alivotunusuru kwenye magonjwa mengine ya mlipuko, wito tu kwa Wizara ya Afya lioneni hili kwa uzito uliopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kenya wamejitoa akili wameruhusu ndege ya China iendelee kusomba wachina kuwaleta Kenya na Wakenya waende China. Tujiandae na janga kutokea kwa majirani.
 
Kenya wamejitoa akili wameruhusu ndege ya China iendelee kusomba wachina kuwaleta Kenya na Wakenya waende China. Tujiandae na janga kutokea kwa majirani.
Unasema Kenya?
Tanzania pia wameruhusu kuingia watalii toka China, kuna thread humu tayari.
 
Yaani wakenya ndio naona wameamuwa kabisa kuingiza huu ugonjwa afrika mashariki .Hawa ndugu zetu ndio watakao tuuwa ,na tuseme ukweli huu ugonjwa ukiingia hapa nchini hali ya maisha itakuwa ngumu Mara mia tatu na ilivyo sasa, kama mtu ukizuiliwa usiende kariakoo kufanya biashara zako ,wewe unategemea utaishi vp .Na maisha ya watanzania wengi hutegemea kipato cha kila siku .Tena wengi kipato chetu hutegemea mkusanyiko wa watu ,mfano kariakoo ,na kwenye machimbo mbali mbali ya migodi .Watanzania wachache sana huweka akiba ,kwa ajili ya matatizo kama haya yanapojitokeza .Huu ugonjwa ukiingia tutakufa kwa njaa na kwa ugonjwa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo hii naihofia sana kuingia toka Zanzibar sababu tayari ipo huku imeingia tangu last week. Tunakula pweza na ngisi tuuuu
 
As much as I want to believe that COVID-19 is a global threat, I also think that the traditional media is exaggerating things
 
National Guideline of Clinical Management and Infection Prevention and Control of Novel Corona Virus.
 

Attachments

  • Corona Guideline-Tanzania.pdf
    1.1 MB · Views: 1
Back
Top Bottom