Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,325
- 152,136
Tatizo la ujenzi hoela ni matokeo ya Wizara ya Ardhi na Manispaa za miji na majiji kushindwa kutimiza majukumu yao kutokana na sababu mbalimbali.
Moja ya sababu bila shaka ni kukosekana kwa kitengo maalumu cha kudhibiti ujenzi holela ambacho kingekuwa na bajeti yake maalumu ya kuendesha shughuli zake kama vile kusimamia sheria za ardhi na mipango miji,kuzuia ujenzi holela,kutoa elimu kwa umma juu ujenzi sahihi wa makazi,upimaji wa ardhi n.k
Kitengo cha ardhi katika Wizara ya Ardhi,Idara za Ardhi na Mipango miji katika Halamshauri zote nchini zivunjwe na badala yake majukumu yake yafanywe na Agency hii itakayokuwa na matawi na ofisi zake nchi nzima.
Kama wazo hili kitaalamu litaonekana haliwezekani/halitekelezeki,basi Agency hii ipewe majukumu ya kusimamia na kudhibiti utendaji kazi wa vitengo/idara zinazohusika na maswala ya ardhi na mipango miji katika Halmashauri zote nchini pamoja na kitengo cha Ardhi kilichopo wizara ya ardhi kama ambavyo Taasisi kama EWURA inavyodhibiti na kusimamia maswala ya maji na nishati nchini.
Swala la kusimamia sheria za ardhi na mipango miji linahitaji chombo maalumu kitakachokuwa kinatengewa bajeti yake maalumu ya kuendesha shughuli zake kwani hili ni eneo nyeti sana na linalogusa maisha ya watu kama jinsi tunavyoshuhudia sasa.
Najua kuna watu watakuja na hoja ya gharama lakini naomba niwaulize hili zoezi la bomoabomoa linatumia gharama kiasi gani ukiachilia mbali kuathiri maisha ya watanzania masikini?
Tukubali,wizara ya ardhi na Halamashauri zote nchini kazi ya kusimamia sheria za ardhi na mipango miji imewashinda na tunahitaji kuwa na chombo maalumu katika eneo hili kwani bomoabomoa bila udhibiti maalumu kwa siku za usoni ni kazi bure kama ilivyokuwa katika zoezi la kuhamishia watu huko Mabwepande ambao walirudi tena mabondeni kwasababu ya kukosekana kwa udhibiti na ufuatiliaji wa makazi mapya kwa waliopewa viwanja.
Halamashauri zetu bajeti zake ni ndogo sana huku zikiwa na shughuli nyingi pamoja na vitengo/idara lukuki zinazotegemea bajeti hiyo ndogo ambayo hatahivyo wakati mwingine hupokea fedha pungufu na zile zilizoombwa katika bajeti.

Last edited: