Jana wakati naangalia Taarifa ya habari niliona wabunge wakihoji ni lini serikali itapeleka mikataba bungeni.
nilijiuliza mengi nikajiuliza hivi kuipeleka mikataba bungeni tutatatua matatizo ya mikataba?
ni rahisi sana kuona kama naunga mkono serikali lakini jifanye kama hujui ninaipinga au naiunga mkono unisikilize kwanza uelewe ninallolisema alafau ndio ulihukumu.
kwangu mimi ninaona tanzania ikiwa tunachukulia mambo kirahisi na kila mmoja akijaribu kutafuta ugali wake huku akidai matatizo tuliyonayo ni kwa yeye kutoshirikishwa. hivi kweli hili ndilo tatizo letu?
kwanza kabisa najiuliza ni mambo mangapi yamepita bungeni na bado yanatoka huko mambo ni yaleyale. nakumbuka kuna wakati niliwahi kusikia waziri akiliambia bunge kuwa alienda kusaini mkataba wa madini ulaya kwa kuwa tungepoteza kiasi fulani cha fedha na bunge lilikubaliana na waziri huyo.
niliwahi kuandika katika mtandao huu wa kijamii kuwa bunge letu ndio mzigo namba moja. mimi ninaamini kama bunge lingekuwa makini kwa majukumu waliyopewa ya kusiamamia na kushauri serikali tusingekuwa na serikali zinazofanya vibaya.
lakini kama msimamizi mwenyewe hajui wajibu wake na hatimizi maana hawezi kutimiza asilolijua unategemea serikali ifanye nini kama sio bahati nasibu, ikifanya vizuri haya aikifanya vibaya haya.
kwanza huwezi kufanya kazi ya kusiamia na kushauri bila utaalamu, sasa bunge utaalamu linaupate?
tujikite katika swala la mikataba hii, hivi bunge lina utaalamu gani wa kupitia mikata kama sio watu kutumia madaraka tuliyowapa badala ya kuweka utaratibu mzuri bali wanataka kujilundikia kila kitu na mambo wasiyaweza na kufanya ubabaishaji ndani unaoligahrimu taifa.
tatizo linalotuingiza katika mikataba mibovu ni nini? je ni corruption? je ni utaalamu wa watu kujua mbinu na vigezo vya kimikataba ili kulitetea taifa na kuweka vipengele vizuri katika mikataba?
hivi wengi wetu tumekuwa tukisikiliza bunge, mtu anasimama kuchangia hoja muhimu anachokifanya ni kutaja majina ya vijiji na kata kwenye jimbo lake na huyo ndiye anayepigiwa makofi na wabunge wenzake. hivi tunadhani tunaweza kuondoa mikataba mibovu kwa kusema tuipitishe bungeni? hawa wana utaalamu gani?
sasa kama ushauri wenyewe unaotolewa na bunge juu ya mikataba ndio huo wa kutaka wao ambao wanaunda kamati ambazo upo uwezekano wa kukuta mwaka fulani kuna taaluma haikuingia bungeni kutokana na wanaoingia wanatumia vigezo tofauti. watafika huko wataunda kamati mfano kamati imejaa walimu tu eti inaletewa mkataba wa madini kuupitia na wanaona wakiipitia wao ndio kutaondoa tatizo la mikataba mibovu?
hoja yangu ni hili tatizo haliko kwa bunge tu, sote katika jamii hatukai kujitafakari na kuangalia kila wetu mimi kama mimi au sisi kama sisi wajibu wetu katika taifa hili ni upi.
sote tunabaki kutazama wengine na kudhani tukichukua majukumu ya wengine ndio mambo yatakwenda vizuri. hivi kwa kufikiri hivyo je tunakuwa sahihi au bado tunaendeleza ubabaishaji?