Tanzania tuitakayo miaka 25 ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania tuitakayo miaka 25 ijayo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Dec 16, 2011.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Ili nchi ya Tanzania iendelee na kupiga hatua kubwa ya maendeleo ni lazima haya yafuatayo yatokee.
  1. Lazima tuwe na katiba mpya itakayotengenezwa kisayansi na kushirikisha makundi yote ya jamii na kuunda tume huru za kukusanya maoni, na kutengeneza katiba, tume huru ya uchaguzi mahakama huru, bunge huru, na serikali isitokane na wabunge.

  2. Vyombo vya habari lazima vianze kuajiri wasome wenye mkusanyiko wa elimu mbali mbali.
  3. Tubadili mitaala yetu ya elimu ili iendane na dunia ya sasa.

  4. Msomo ya sayansi pamoja na mishahara inayotokana na wahitimu wa sayansi ipande na masomo yao yazingatiwe kuanzia shule za msingi.

  5. Tuheshimu na kuwatambua wagunduzi wa ndani na wafanyabiashara wabunifu wasio iba wala kubebwa na mfumo wa wezi.

  6. Viongzoi lazima wapatikane kwa historia zao za utendaji na maisha yao katika jamii.

  7. wananchi waelimishwe jinsi ya kuchagua wawakilishi wanaojali maslahi ya mpiga kura sio maslahi yao binafsi.

  8. Wananchi waelimishwe madhara ya kushabikia mafisadi hasa pale wanapoishi na fedha za wizi na wananchi kuwaona mashujaa

  9. Taasisi za dini ziache kukumbatia wezi, mafisadi kwa kisingizio chochote kile kwani hali hii inadhoufisha wanoishi kwa kutenda mema na kumtumainia Mungu.

  10. Katiba iweke wazi kiongozi hatalipiwa matibabu nje ya nchi mpaka idhibitike kuwa huduma husika au ugonjwa husika hauna wataalamu nchini.

  11. Wananchi wasimchague kiongozi ambaye hatumii huduma zilizopo jimboni mwake kama hospitali, shule, na huduma mbali mbali za jamii.

  12. Wananchi waruhusiwe kupiga kura za maoni dhidi ya viongozi wao kila miaka miwili na nusu, na kiongozi akionekana hafai atolewe.

  13. Tupunguze ukubwa wa bunge kwa kuhakikisha hakuna mkoa unatoa zaidi ya wabunge nne na mikoa iwe ya kudumu ndani ya katiba ili kuondoa mwanya wa wanasiasa kuigawanywa kila wakijisikia.

  14. Kuongeza ushiriki wa madiwani kwani wako karibu zaidi ya wananchi.

  15. Kuhakikisha tunauza bidhaa badala ya malighafi. Hakuna nchi imeendelea kwa kuuza malighafi.

  16. Sheria zetu za uwekezaji kwa wageni tuziangalie upya ili ziweze kumnufaisha mwananchi, na wawekezaji wote lazima wawe wale wanaokuja kutumia malighafi ili kuzalisha hapa nchini, badala ya sheria za sasa za wao kufanya Tanzania shamba la bibi.

  17. Kukuza uzalendo na kuchukia wanaoiua nchi.

  Ni mimi Chief Mkwawa wa Kalenga
   
Loading...