Tanzania tuache siasa za kizamani na tuwe na siasa endelevu (progressive politics)

PESAYAKO

Member
Sep 14, 2013
33
14
Nimeangalia kwa muda mrefu sana kwenye hili jukwa na pamoja kwenye social media zingine kama Twitter, Facebook, Bloggs nk. Mtindo ni mmoja tu Zitto Kabwe tu kumjadili utazania anatuwekea mkate kila siku asubuhi mezani. Huu ni upumbavu wa hali ya juu badala ya kujadili vitu vya kujenga hoja kama Sera (Policy) tuna kalia kujadili watu. Huu ni ujinga wa hali ya juu naomba ndugu zangu Watanzania tujadili vitu vitavyotuletea maendeleo na sio watu. Hawa watu watakuja wataondoka na watakuja wengine lakini Sera zitadumu na kukumbukwa viza na vizazi kwa kuweka kumbukumbu.
Watanzania tujadili Sera(Policy) za vyama na sio watu na kama hatutabadilika kwa mtaji huu Umaskini hautakwisha. Mtakuja kujuta kwanini mnapoteza muda kwenye kujadili watu wakati bei ya umeme inapanda, bei ya gas ya kupikia juu, umaskini unaongezeka kila kukicha.
Hao wakina Zito ndio nani hao kwani wao ni bora kuliko watoto wetu wanaosoma bila kuwa na vyumba vya madarasa, watoto wanakwenda shule bila kuwa na mavazi mazuri pamoja na viatu, madaftari, wanafunzi wanafeli, watu hawana ajira, walemavu hawana mahitaji, madawa hospitalini hakuna, maji safi ya kunywa hakuna tena hata Dar es Salaam, Watu wanazidi kuwa maskini na wakina mama wajawazito wanakufa kwa kukosa huduma bora.
Huu ni wendawazimu ni muda sasa wa kukaa na kujadili sera bora kwa nchi yetu na siyo kupoteza muda na watu wachache wakati kuna watu wengi wankufa kutoka na matatizo yanayoweza kuzuilika na pia kuna watu wengi wanakosa huduma ambazo zingiweza kupatikana kama msisitizo ungewekwa.
Tuache hizi siasa za kizamani za enzi ya cold war na tuwe na siasa endelevu (Progressive Politics or Progressive Politician) na sio hizi siasa njaa za kujadili majina. Sanasa ni kukifaidisha chama kilicho madarakani maana muda mwingi badala ya wananchi kujadili kama kinatekeleza majukumu sisi wananchi tume ng'ang'ana na kujadili watu.
Watu wapo, watu wataondoka , watu watakuja wapya lakini sera nzuri zitakuwepo na zitadumu na kukumbukwa na vizazi vingi vijavyo.
 
Bora umeliona hlo mkuu kwasababu kuna watu humu wanatoa mapov kila sku kuzungumzia watu utadhan ndio awanao walisha. Watz tunasikitisha sana. Kila sku utaona slaa mara mbowe mara sijui zitto mar mwigulu yaan mpaka inakuwa kero
 
Back
Top Bottom