DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 409
- 343
Wanabodi,
Walio ughaibuni wana msemo mmoja ambao nita unukuu kwa Kiingereza, "If you want anything done right, do it yourself". Uchambuzi mfupi wa msemo huu unaweza kuashiria mambo mengi lakini chenye umuhimu kabisa ni kwamba katika juhudi zote za kuishi vizuri na wanao tuzunguka, fahamu kwamba ambaye anatakiwa kuwa na machungu zaidi kuhusu maendeleo yetu ni sisi wenyewe.
Nitaendelea kuelezea kuhusu mada hii kwa kusema kwamba, shamrashamra za kupata uhuru mwaka 1963 zili badilika na kuwa kilio miaka kadhaa iliyopita tulipo gundua kwamba ukoloni unaweza kujirudia kwa njia nyingine ambayo inaitwa "Neo-colonialism". Je, neo-colonialism ni nini?. Tafsiri ya neno hili kwa Kiingereza ni: The use of economic, political, cultural or other pressures to control or influence other countries, especially former dependencies. Tanzania iliyo tawaliwa na waingereza na wajerumani leo hii imepiga hatua kubwa kimaendeleo. Swali ambalo ni muhimu kujiuliza ni kama mwenendo wa nchi katika kipindi hiki na rasilimali watu vina ashiria kwamba maendeleo haya ni kutokana na jasho letu wenyewe.
Unaweza kusema kwamba haijalishi maendeleo yameletwa na nani ili mradi watanzania wana nufaika lakini siku zote, serikali pamoja na vyombo vyake vyote havitakiwi kutegemea shirika au nchi yoyote bila kuwa na mipango wa kujifunza au kubuni ujuzi wowote. Inawezekana kabisa kuwa na watanzania wenye malengo mazuri na wenye fikra na uwezo wa hali ya juu katika suala zima la kuchambua changamoto tulizonazo kwa kina na baada ya hapo kuwa na suluhisho tofauti tofauti lakini kushindwa kwetu kujiamini na kushindwa kutumikia maendeleo yetu ni baadhi ya sababu zinazo tufanya tuendelee kuwa tegemezi.
Tukitazama teuzi mbalimbali zinazofanywa na rais, viapo vya viongozi katika wadhifa tofauti tofauti, na idadi ya watu "wanao husika moja kwa moja" katika maamuzi ya serikali, utagundua kwamba, idara ya rasilimali watu serikalini sio imara. Huhitaji kutazama mbali ili kuelewa kwamba bunge la Tanzania kwa muda mrefu sasa halina mchango wowote unaoweza kuwa na tija katika uendeshaji wa serikali. Vile vile vijana wanao husika moja kwa moja na vyama vya siasa bado hawaja onyesha ukomavu na wala hawaoni umuhimu wa kufanya shughuli zao kwa umakini katika suala zima la kuwa saidia watanzania.
Katika hatua hii, ni vyema kufahamu kwamba siku zote, maendeleo yatakayo ivusha Tanzania kutoka nchi ya dunia ya tatu na kuifanya iwe nchi ya dunia ya pili yana hitaji taasisi zilizo imara na rasilimali watu wanao jituma na kuendesha shughuli zao vizuri na bila kufuatiliwa. Mila na desturi zetu za ustaarabu, uadilifu na utu wema zidumu katika suala zima la kutafuta maendeleo ya nchi yetu pendwa Tanzania.
Tafakari,
Jummah Kareem