Tanzania still does not recognise new Libyan Rulers

Tanzania still does not recognise new Libyan Rulers

Idols of the market place. Tz tupo sewrious na vitu vya ovyo. Gadafi is gone, wanataka arudi ili wamtambue? Viongozi wetu si mchezo
 
Hii ndiyo maana ya kuwa na msimamo. Kama threshhold ya utawala bora bora au muundo wa serikali haijafikiwa basi watawala hao wanabaki kuwa ni kikundi cha wahuni ambao hawana sifa ya kupewa heshima ya kutambuliwa.
 
SERIKALI imesema inaendelea na msimamo wake wa kutoitambua Serikali mpya ya Libya hadi pale itakapotimiza na kukidhi vigezo vinavyotambulika na nchi zote za Umoja wa Afrika (AU) ambavyo vipo kwa mujibu wa Sheria za Kimataifa. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim alisema vipimo au vigezo vinavyotumika kuitambua au kutoitambua Serikali mpya yoyote ni vingi na kwa upande wa AU na Tanzania, Serikali yoyote inayoingia madarakani kwa kuiondoa Serikali halali iliyochaguliwa na wananchi kidemokrasia haitambuliwi.

“Serikali ya Tanzania kwa kuzingatia mchakato mzima wa mabadiliko ya Libya kuanzia vita ilipoanza bila kuihusisha AU, kuzuka kwa mapigano yaliyoihusisha NATO wakisaidiwa na Baraza la Waasi wa Libya (NTC) na kuuawa kikatili kwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi kunaifanya Serikali ya Tanzania kutoitambua NTC,” alisema Maalim.

Alisema Serikali ya Tanzania itaitambua Serikali ya Libya iwapo tu itatekeleza vigezo vya kuunda Serikali ya Mpito itakayowashirikisha wananchi wote wa Libya, kutekeleza Mpango wa Amani wa AU ambao utaitisha uchaguzi huru, haki na kidemokrasia na kuwapo kwa Bunge la uwakilishi na Mahakama huru. “Serikali inapenda kusisitiza mauaji yaliyotokea nchini Libya hatuyaungi mkono na kwamba Serikali hailazimiki kutambua Baraza au Serikali ambayo inakiuka vigezo vilivyoainishwa hapo juu,” alisema.

Habari leo.
 
delusion itawapeleka pabaya hawa viongozi wetu-libya hawana haya ya kutambuliwa na serikali ya ccm maana kwao haina msaada wowote-those big daddies walioitambua wanatosha sana
 
It doesn't make any different ........waitambue wasiitambue haitasaidia CCM na serikali yake kuboresha hali zetu duni za maisha
 
libya haina serikali , hivi jamani mbona hili watu hamulielewi?
 
The Deputy Minister for Foreign Affairs and International Co-operation, Mr Mahadhi Juma Maalim, saidTanzania will not recognise any regime that comes to power through unconstitutional means.-Lakini Waziri pia angetuambia kuwa kama hatutambui serikali zinazoingia katika madaraka kwa mapinduzi kama ya libya,Tulipaswa pia kutozitambua zile ambazo zinabaki madarakani UNCONSTITUTIONALY,The uncontitutional existance in power ndiyo imepelekea hayo ya Libya,angalia Zimbabwe,Angalia Uganda,haiwezekani ukae madarakani Miaka arobaini na miwili ukipinduliwa useme waliokupindua wameingia madarakani Uncostitutionally,wakati wewe hukutana hiyo constitutional waklati wako,huu pia ni unadfiki mkubwa kwa viongozi wetu wengi wa kiafrica.
 
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]


na Edson Kamukara

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]
SERIKALI imeainisha vigezo vitatu ambayo inataka vitekelezwe ili kuweza kulitambua Baraza la Mpito la Waasi (NTC) la nchini Libya, lililomwondoa madarakani kiongozi wa nchi hiyo, Kanali Muammar Gaddafi, mwezi uliyopita.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, alitoa msimamo huo Bungeni jana mjini Dodoma wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF).

Katika maswali yake, mbunge huyo alitaka kujua ni vipimo gani Tanzania inatumia kuitambua au kutoitambua Serikali mpya ya Libya itakayoundwa baada ya kuondolewa kwa hayati Kanali Gaddafi, na kwamba vipimo hivyo vinatumika kwa mapinduzi yoyote ya aina hiyo?
Naibu waziri huyo, alifafanua kuwa vipimo vinavyotumika ni vingi na kwamba katika kesi ya Umoja wa Afrika na Tanzania, serikali yoyote inayoingia madarakani kwa kuiondoa serikali halali iliyochaguliwa na wanachi kidemokrasia, hiyo haitambuliwi na katika hilo aliitolea mfano serikali ya Madagasar iliyopinduliwa mwaka 2009.

“Vigezo vitakavyotumika kuitambua serikali mpya ya Libya ni tofauti na kigezo hicho hapo juu. Vipimo tulivyoweka baada ya mchakato mzima ili tuweze kuitambua NTC ni

- kuunda serikali ya mpito itakayoshirikisha makundi na makabila yote nchini humo.
- kutekeleza mpango wa amani wa Umoja wa Afrika (Road Map) ambao utapelekea kuitishwa kwa uchaguzi huru, haki na kidemokrasia,” alisema.

Katika kipimo cha tatu,
- alisema Tanzania inalitaka baraza hilo katika serikali yake ya mpito kuwa na Bunge la wawakilishi na mahakama huru, huku akisisitiza kuwa haiyaungi mkono mauaji yaliyotokea Libya.


Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF), aliyehoji ni kwanini Tanzania ilikaa kimya wakati Libya ikivamiwa, Naibu waziri huyo alisema serikali ilitoa msimamo wake kuwa haikuafiki jinsi azimio la Umoja wa Mataifa lilivyotekelezwa na majeshi ya NATO.

Kuhusu kwanini serikali haitambui mapinduzi, lakini baada ya serikali mpya kuundwa na wapinduaji hao inageuza msimamo, naibu waziri huyo alisema baada ya waasi kuondoa serikali halali na kuunda mpya inayokidhi vigezo vinavyotakiwa basi Tanzania huendeleza mahusiano na taifa hilo.



[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Wataitambuaje Libya wakati wenyewe hawajitambui? yakwao yanawashinda ya Libya wataweza?
 
Tanzania viongozi wake wanachekesha kweli kweli ...hivi vijamaa utafikiri ni viooongooozi kumbe tabu tubu lol!
 
Kwa mfano,tunaendelea kushika msimamo huo for as long as it takes! What difference does it make? Why we do not want to recognize the choice of libyans while our stand throughtout the decades has been not to mingle with internal affairs of other countries? Did we change of political outlook as far as African politics is concerned?
 
Back
Top Bottom