Tanzania & Siasa: Sera nzuri ndio maendeleo yetu

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Habari Tanzania!

Nimefurahi kuona na kusikia mijadala mingi mitaani, maofisini na sasa mitandaoni watu wakizungumza kuhusu sera za vyama vya siasa namna watakavyo toa huduma endapo wakipewa mamlaka; yaani nimependa namna watu wanavyofunguka akili sana.

Kupitia kusikiliza, kuchambua na kuchagua sera nzuri itachochea maendeleo halisi kwa maeneo husika au jamii; kazi zimamoto hazitakuwepo (maendeleo ya kushtukiza); kuondoa wagombea feki; watu wasiojiweza na wasio na ushawishi kwa jamii watatoweka; siasa itakuwa na manufaa kwa jamii moja kwa moja; tutaweza kuona ahadi za wakati zenye manufaa kiutekelezaji na tutapata maendeleo ya kweli kwa wagombea halisi.

Pia tutaweza kuhoji kwa ufasaha mambo, sera au ahadi walizoahidi kipindi cha kampeni kwa kutaka kuona utekelezaji wake unavyofanyika au ulivyofanyika.

NB:
Nakazia wananchi tuwalazimishe wagombea kupitia majukwaa yote wa vyama vyote vya siasa waseme sera zao za ndani ya nchi na mambo ya nje ya nchi yetu. Tusikubali ubabaishaji.

Karibu.
 
Back
Top Bottom