Tanzania sasa namba moja kwa utalii

Tanzania sasa namba moja kwa utalii

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Wizara ya Maliasili na Utalii

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kama ilivyoripotiwa na kituo cha utangazaji cha CNN cha nchini Marekani, napenda kutumia fursa hii kuwajulisha kuwa nchi yetu imeendelea kufanya vizuri duniani katika kunadi vivutio vya utalii vilivyoko hapa nchini. Hii inatokana na hatua madhubuti tulizochukua kama nchi, katika suala zima la uhifadhi hasa kwenye ulinzi wa maliasili zetu dhidi ya ujangili ili kuifanya sekta ya utalii iwe nambari moja kwenye ukuzaji uchumi hapa nchini.

Ni uthubutu huo, uliosababisha mafanikio makubwa kwenye mapambano dhidi ya ujangili kwenye hifadhi zetu ambapo kwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo uanzishaji wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), idadi ya wanyamapori waliokuwa hatarini kutoweka sasa inaongezeka hivyo kuwavutia wageni wengi kutembelea hifadhi zetu mara wanaposikia taarifa kuhusu sekta ya utalii ya Tanzania.

Jambo lililosababisha nizungumze na ninyi asubuhi hii ni kuwajulisha kuwa, nchi yetu kutokana na jitihada mbalimbali ambazo tayari tumezionyesha kwenye sekta hii ya utalii kwa ujumla wake; hivi karibuni imetajwa kuwa ya kwanza barani Afrika kwa ubora na mvuto wa kutembelewa na watalii.

Heshima hii kwa taifa letu ni matokeo ya utafiti wa kina uliofanywa na mtandao wa kimataifa wa nchini Uholanzi unaoshughulika na masuala ya utalii unaofahamika kama safaribookings.com, ambao ulitumia takriban miaka miwili kukusanya maoni ya watalii maarufu na wataalamu wa masuala ya maliasili kote duniani, ambao hao walizungumzia uzoefu wao na hali ya sekta ya utalii katika nchi za Afrika, wakieleza wazi juu ya nchi bora kwenye Utalii kwa sasa.

Matokeo hayo yanaonyesha zaidi ya watu 1,000 kutoka nchi 53 walihusishwa kwenye utafiti huo ambao kati ya jumla ya pointi tano za zilizotolewa kwa wastani, Tanzania ilipata pointi 4.8 ambazo ndio alama za juu ikifuatiwa na Botswana yenye pointi 4.75, Kenya 4.66; Zambia 4.58; Afrika Kusini 4.55; Namibia 4.54; Uganda 4.16 na Zimbabwe 4.14.

Sababu zilizotajwa na watafiti hao, kuwa siri ya ushindi wa Tanzania barani Afrika kwenye sekta ya utalii ni utajiri wa maeneo ya hifadhi za wanyamapori ambayo mawili kati yao ni maeneo ya urithi wa dunia yanayotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO; maisha ya asili ya wanyamapori hifadhini Serengeti ambako kwa mwaka zaidi ya wanyama hasa nyumbu milioni mbili huhama kuelekea Mbuga ya Maasai Mara kwa upande wa Kenya kisha kurudi nchini.

Pia uwepo wa maeneo ya malazi ya hadhi tofauti tofauti kwenye maeneo yetu ya vivutio kulingana na uwezo wa mtu kiuchumi, fukwe za kuvutia, uwepo wa wanyamapori wasiopatikana maeneo mengine duniani, Mlima Kilimanjaro ambao ni wa kwanza kwa urefu Afrika na hali ya usalama, amani kisiasa zimetajwa kuwa sababu kuu za mafanikio yetu kwenye sekta ya utalii Afrika.

Aidha matokeo ya utafiti huo yamezitaja hifadhi zetu 10 kati ya 16 zilizopo hapa nchini kuwa chachu nyingine ya ushindi kwakuwa Wanyamapori watano wakubwa mbugani ambao ni Simba, Faru, Tembo, Chui na Nyati wanapatikana kwenye baadhi ya hifadhi hizi ambazo ni Serengeti, Selous, Ngorongoro, Katavi, Tarangire, Ziwa Manyara na Arusha huku Mahale ikitajwa kwa upekee wake wa idadi kubwa ya Chimpanzee.

Watafiti walistaajabishwa zaidi na Tanzania kwasababu ni nchi pekee ambayo kutokana na utajiri wetu wa maliasili, hatuna majira ya mwaka ambayo utalii hauwezekani kabisa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa au majira; tofauti na nchi zingine ambazo kwenye baadhi ya miezi hali huwa mbaya na watalii huacha kuzitembelea mpaka kipindi hicho kipite.

Ni wazi kuwa tunastahili kujipongeza kwa mafanikio haya, kwani nchi tulizoshindanishwa nazo pia zina ubora wake kwa namna mbalimbali kwenye sekta ya utalii, hivyo hatujawa washindi kati ya wabovu bali washindi miongoni mwa washindi hivyo ni mafanikio makubwa ambayo wote tu mashahidi kuwa kutokana na serikali ya awamu ya nne ya CCM kuonyesha nia ya kutumia utalii kukuza uchumi na kufanya kwa vitendo; tumeweza na tunaendelea kusonga mbele.

Tunajifunza nini kwenye suala hili? Hatulewi sifa, tunaendelea kuchapakazi ambapo katika kulithibitisha hili, hivi karibuni tuliwaalika waandaji maarufu wa filamu bora duniani kutoka Hollywood wakachukua picha kwenye hifadhi zetu ili kuandaa tangazo la viwango vya kimataifa ambalo litarushwa kwenye vituo vya televisheni vya mashirika ya kimataifa ya habari ikiwemo CNN ili kuvutia watalii wengi zaidi.

Tangazo hilo ambalo litakamilika na kukabidhiwa kwetu hivi karibuni, litazinduliwa na Mhe. Rais Dk. Jakaya Kikwete, ili lianze kurushwa rasmi kwenye vituo hivyo kote duniani; Watanzania tunachotakiwa kufanya ni kuendelea kuitunza amani iliyopo, kutunza mazingira yanayozunguka hifadhi zetu na ndani ya hifadhi bila kusahau kutoa ushirikiano kwa TAWA na mamlaka zingine juu ya taarifa za majangili ili tuendelee kuwa bora Afrika na duniani.

Lazaro Nyalandu

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.

Dar es Salaam, 19 Mei, 2015

tatizo nyalandu anatafuta sifa hata kwa kudanganya umma

tembo wanazidi kupungua yeye anadai wamefanikiwa kwenye ujangili
 
Hii kazi ya kutoa taarifa angeweza kufanya afisa habari wa wzara au TANAPA au katibu mkuu waziri kutoa taarifa kama hii ni kiherere cha kupitiliza.
 
habari imeanza vizuuuri ila mwishon tu, kama pameharibika, lakin , KUNA ATHAR GANI YA KUWA WA KWANZA, WAKAT MPUNGA UTAISHIA KWA WACHACHE??
 
Sioni juhudi binafsi za nchi kama nchi. Naona zaidi God's favor ya kutujalia maliasili tulizokuwa nazo.
Naona juhudi za international organisations na research centers walizofanya juhudi kubwa kuzipigania na kuijengea uwezo tanapa kuweza kusimamia hizi resources. Kwa waliofanya kazi kwenye hifadhi wanajua michango ya frankfurt zoological societies, jane Goodall institutes, WCS, AWF na jinsi mara kadhaa wamehitilafiana na serikali ya ccm wasivune na kuharibu hifadhi kwa kichaka cha 'maendeleo'.

Leo hii wao ndio wanakuja juu kuwa wamefanikiwa.
 
Mbona tumechelewa kuwa wa kwanza???afu hizi juhudi ni kama watalii ndo wametustua,wizara ililala sana hapa kati.I think Tanzania deserved this recognition from early 2000's.
 
jamhuri ya muungano wa tanzania

wizara ya maliasili na utalii

taarifa kwa vyombo vya habari

kama ilivyoripotiwa na kituo cha utangazaji cha cnn cha nchini marekani, napenda kutumia fursa hii kuwajulisha kuwa nchi yetu imeendelea kufanya vizuri duniani katika kunadi vivutio vya utalii vilivyoko hapa nchini. Hii inatokana na hatua madhubuti tulizochukua kama nchi, katika suala zima la uhifadhi hasa kwenye ulinzi wa maliasili zetu dhidi ya ujangili ili kuifanya sekta ya utalii iwe nambari moja kwenye ukuzaji uchumi hapa nchini.

ni uthubutu huo, uliosababisha mafanikio makubwa kwenye mapambano dhidi ya ujangili kwenye hifadhi zetu ambapo kwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo uanzishaji wa mamlaka ya wanyamapori tanzania (tawa), idadi ya wanyamapori waliokuwa hatarini kutoweka sasa inaongezeka hivyo kuwavutia wageni wengi kutembelea hifadhi zetu mara wanaposikia taarifa kuhusu sekta ya utalii ya tanzania.

Jambo lililosababisha nizungumze na ninyi asubuhi hii ni kuwajulisha kuwa, nchi yetu kutokana na jitihada mbalimbali ambazo tayari tumezionyesha kwenye sekta hii ya utalii kwa ujumla wake; hivi karibuni imetajwa kuwa ya kwanza barani afrika kwa ubora na mvuto wa kutembelewa na watalii.

Heshima hii kwa taifa letu ni matokeo ya utafiti wa kina uliofanywa na mtandao wa kimataifa wa nchini uholanzi unaoshughulika na masuala ya utalii unaofahamika kama safaribookings.com, ambao ulitumia takriban miaka miwili kukusanya maoni ya watalii maarufu na wataalamu wa masuala ya maliasili kote duniani, ambao hao walizungumzia uzoefu wao na hali ya sekta ya utalii katika nchi za afrika, wakieleza wazi juu ya nchi bora kwenye utalii kwa sasa.

Matokeo hayo yanaonyesha zaidi ya watu 1,000 kutoka nchi 53 walihusishwa kwenye utafiti huo ambao kati ya jumla ya pointi tano za zilizotolewa kwa wastani, tanzania ilipata pointi 4.8 ambazo ndio alama za juu ikifuatiwa na botswana yenye pointi 4.75, kenya 4.66; zambia 4.58; afrika kusini 4.55; namibia 4.54; uganda 4.16 na zimbabwe 4.14.

Sababu zilizotajwa na watafiti hao, kuwa siri ya ushindi wa tanzania barani afrika kwenye sekta ya utalii ni utajiri wa maeneo ya hifadhi za wanyamapori ambayo mawili kati yao ni maeneo ya urithi wa dunia yanayotambuliwa na shirika la umoja wa mataifa la unesco; maisha ya asili ya wanyamapori hifadhini serengeti ambako kwa mwaka zaidi ya wanyama hasa nyumbu milioni mbili huhama kuelekea mbuga ya maasai mara kwa upande wa kenya kisha kurudi nchini.

Pia uwepo wa maeneo ya malazi ya hadhi tofauti tofauti kwenye maeneo yetu ya vivutio kulingana na uwezo wa mtu kiuchumi, fukwe za kuvutia, uwepo wa wanyamapori wasiopatikana maeneo mengine duniani, mlima kilimanjaro ambao ni wa kwanza kwa urefu afrika na hali ya usalama, amani kisiasa zimetajwa kuwa sababu kuu za mafanikio yetu kwenye sekta ya utalii afrika.

Aidha matokeo ya utafiti huo yamezitaja hifadhi zetu 10 kati ya 16 zilizopo hapa nchini kuwa chachu nyingine ya ushindi kwakuwa wanyamapori watano wakubwa mbugani ambao ni simba, faru, tembo, chui na nyati wanapatikana kwenye baadhi ya hifadhi hizi ambazo ni serengeti, selous, ngorongoro, katavi, tarangire, ziwa manyara na arusha huku mahale ikitajwa kwa upekee wake wa idadi kubwa ya chimpanzee.

Watafiti walistaajabishwa zaidi na tanzania kwasababu ni nchi pekee ambayo kutokana na utajiri wetu wa maliasili, hatuna majira ya mwaka ambayo utalii hauwezekani kabisa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa au majira; tofauti na nchi zingine ambazo kwenye baadhi ya miezi hali huwa mbaya na watalii huacha kuzitembelea mpaka kipindi hicho kipite.

Ni wazi kuwa tunastahili kujipongeza kwa mafanikio haya, kwani nchi tulizoshindanishwa nazo pia zina ubora wake kwa namna mbalimbali kwenye sekta ya utalii, hivyo hatujawa washindi kati ya wabovu bali washindi miongoni mwa washindi hivyo ni mafanikio makubwa ambayo wote tu mashahidi kuwa kutokana na serikali ya awamu ya nne ya ccm kuonyesha nia ya kutumia utalii kukuza uchumi na kufanya kwa vitendo; tumeweza na tunaendelea kusonga mbele.

Tunajifunza nini kwenye suala hili? Hatulewi sifa, tunaendelea kuchapakazi ambapo katika kulithibitisha hili, hivi karibuni tuliwaalika waandaji maarufu wa filamu bora duniani kutoka hollywood wakachukua picha kwenye hifadhi zetu ili kuandaa tangazo la viwango vya kimataifa ambalo litarushwa kwenye vituo vya televisheni vya mashirika ya kimataifa ya habari ikiwemo cnn ili kuvutia watalii wengi zaidi.

Tangazo hilo ambalo litakamilika na kukabidhiwa kwetu hivi karibuni, litazinduliwa na mhe. Rais dk. Jakaya kikwete, ili lianze kurushwa rasmi kwenye vituo hivyo kote duniani; watanzania tunachotakiwa kufanya ni kuendelea kuitunza amani iliyopo, kutunza mazingira yanayozunguka hifadhi zetu na ndani ya hifadhi bila kusahau kutoa ushirikiano kwa tawa na mamlaka zingine juu ya taarifa za majangili ili tuendelee kuwa bora afrika na duniani.

lazaro nyalandu

waziri wa maliasili na utalii, lazaro nyalandu.

dar es salaam, 19 mei, 2015

safi kabisa! Sasa nitapumua huku nilipo maana kuna majirani walikuwa wananishambulia sana kuwa wao ndio bora! Afadhali ulimwengu umeamua!
 
Tanzania imekuwa ya kwanza kwa sababu ya kuwa na vivutio vingi.jiulizeni tuna vivutio vingi lakini watalii ni wachache hatujilinganishi na Kenya kwa watalii.maana wageni wengi huwa wanaanzia kenya ndio waje huku.Waziri angalia pia swala la park fees imepanda sana.mwaka jana wageni wengi walikatiza safari zao kwa kupanda kwa bei.
 
Kama Mtanzania mzalendo naona ni taarifa nzuri ila bado sijaona connection kati ya ulinzi ulioanza juzijuzi tu na kuongoza kwa utalii kama nchi.
Je watalii walikuwa wangapi na wameongezeka kwa kiasi gani kwasababu ya kuongezeka kwa ulinzi au kuundwa kwa mamlaka ya wanyama pori. Je kuongoza huko kumechangia vipi katika pato la taifa wakati shilingi inazidi kuporomoka. Kwa tulioko kwenye utalii ndo tunaona utalii unazidi kuwa mgumu sijui yeye anapata wapi guts za kutueleza haya.
Hii taarifa mi niliiona kama siku tano zilizo pita lkn kwasababu imefanywa na wazungu basi inabidi tuiabudu wakati tuna watanzania wenzetu wangeweza kufanya haya.
Waziri ametoa hii taarifa kama vile na mhemuko, hajajiandaa kabisaa. Kuna mambo mengi ya msingi yameachwa na hata aina ya uandishi ni ileile tuliyozoea .....
Sina tatito na taarifa mana ni ya wazungu na wala sina tatizo na waziri mwenyewe ila uwasilishaji wake ...... is too low!
 
inafaida gani kwa mtanzania wa kawaida ikiwa wenye kampuni za utalii wengi ni wazungu na wahindi kwa hapa Tanzania
 
Hivi Mapambano gani makubwa yanayoelezwa hapa dhidi ya Ujangiri?

Hivi si ni mwezi uliopita tu imeripotiwa Tembo zaidi ya laki moja wameuwawa hifadhi ya Ruaha na Selous? Huyu Mbeba askari wa Kike Nyarandu aache kujipigia debe kwa kiki ya Utalii, tena ashukuru sana kuchafuka kwa Amani huko Kenya otherwise wimbo ungekuwa ni uleule.

Kwanini utegemee utafiti tena uliofanywa nje ya nchi? Nyie mmefanya lini utafiti ili kugundua hilo?

Hapa Nyarandu anataka kutuambia kama kuwa kwetu namba moja hakuendani na Mapato halisi ya Utalii hapa nchini basi aachie ngazi. Na mbona hajaambatanisha ripoti ya mapato tangu kupata kuwa kwetu namba moja kwenye sekta hii.?

Na hapa inatakiwa ieleweke wazi kwamba Tanzania tunaongoza kwa kuwa na Vivutio vya Utalii lakini tukiongoza kuwa na Huduma duni za Utalii kulinganisha na Nchi zingine na hapa ndipo ulipobase Utafiti huo.

Sisi tunaongoza kwa Vivutio vya Utalii na si Mzingira bora ya Watalii wala Mapato yatokanayo na Sekta hiyo ya Utalii. Kwa mtu mwenyw akili angekuja hapa kujisifu kwa kuongezeka kwa mapato kwenye sekta hiyo ikiambatana na kuboreka kwa Huduma za wanaanchi. Na si kushika kwetu namba moja kwa kuwa na Vivutio vingi vya Utalii huku vikiwa havina manufaa kwa Wananchi.

Hivi hii Serikali itaelimika lini?

BACK TANGANYIKA
 
Sioni juhudi binafsi za nchi kama nchi. Naona zaidi God's favor ya kutujalia maliasili tulizokuwa nazo.
Naona juhudi za international organisations na research centers walizofanya juhudi kubwa kuzipigania na kuijengea uwezo tanapa kuweza kusimamia hizi resources. Kwa waliofanya kazi kwenye hifadhi wanajua michango ya frankfurt zoological societies, jane Goodall institutes, WCS, AWF na jinsi mara kadhaa wamehitilafiana na serikali ya ccm wasivune na kuharibu hifadhi kwa kichaka cha 'maendeleo'.

Leo hii wao ndio wanakuja juu kuwa wamefanikiwa.
Kweli mkuu,ni sir God na baraka zake.Kuna ule mkataba wa kunadi utalii wa Tz na Sunderland FC sijui hawa jamaa wakishuka daraja ktk Epl inakuaje??
 
Back
Top Bottom