Tanzania rejects EAC proposed land reforms


Wewe kweli Zero. Kwa hiyo kigezo cha kukubali proposal kiwe ni kwamba wengine wamekubali za kwako? mimi nadhani kila proposal inaangaliwa kwa merit yake. Kama proposal za TZ zingekuwa haziangalii maslahi yao, wangezikataa. Pengine wanazikubali kwa sababu either zinaangalia maslahi yao vizuri au zina compromize ambazo wao wako tayari kuishi nazo; unavyoiweka ni kama vile wanazikubali kwa sababu wanaipenda Tanzania.

Na kukubali kwao proposal za TZ kamwe haina maana TZ ikubali kila proposal kwa sababu tu kwamba zake zimekubaliwa.
 
Mpendwa Mr. Zero; wewe ni mTanzania au ni mKenya?
maneno yako yanaonyesha kuwa wewe sio mTanzania.

Hallow Mzee mimi ni born and bled Tanzania. Si unaona kiswanglish kinavyopanda sawasawa? Ila wapuuzi kama kina Peasant ndiyo wananikera.

Mimi siyo kuwa nasupport EAC, I would rather go for SADC . Tatizo ni pale tu tunapopinga agenda kwa kudai wenzetu wana agenda ya siri. Hivi tangu jumuia imeanza sisi tumetoa agenda gani ya kutunufaisha? Agenda kubwa zote; FTA, Federation, Free movement of people, Land reform n.k. yote yanaelekea kuwanufaisha wenzetu. Sasa kama sisi hatuna cha kunufaika kwa nini bado tunang’ang’ania huko badala ya kutumia pesa zetu kwenye sehemu zenye faida zaidi??

May be federation itatusaidia kupata watu wenye akili ya kunegotiate kwenye mikataba kuliko hawa mafisadi wanaoangalia matumbo yao tu halafu wakienda kwenye jumuia wanajifanya wanauchungu na nchi. Kama kweli wangekuwa na uchungu na nchi Mwanza na Shinyanga sasa hivi zingekuwa kama Johannesburg.
 
I support Tanzanians for rejecting the Proposed Land Reforms.

IN Tanzania LAnd is Public Owned.

Jamani watanzania tuanzisheni movement kuhakikisha hii issue inaenea kila mahali Tanzania. Kila Mtanzania inatakiwa apinge hili balaa la wageni kuja kumiliki.

Tushirikiane mambo mengine
 
I too am very proud of the position taken by TZ. Asante Mr Aboud.

Private ownership of land could threaten national security in the long run. Shit can happen where a global corporation (say with a Kenyan partner, for example) buys massive land in TZ. People are expelled and you can’t do shit about it 'cause they own the land. You try to expel them; they take you to the world court (because of some MOU agreement with the World Trade Organization!). That is re-colonization through globalization...

IMF, WTO, (and the likes) are always pushing for land reforms that lead to privatization. Thanks our ancestors, Bongo bado kidogo tunakauzalendo.

You lease the land from the government kisha unachukulia mkopo au ukipauza (pawe na kakibanda, off course) unalipa capital gain tax yao, mambo yanaisha. But, the land remains a Govt property. What is wrong with that?

Tena sikuhizi wameongeza miaka ya kukodi, toka 33 mpaka 99 years!
 


Mkuu Zero,

Hapa ninaungana na wewe kwa nini tunaendelea kupoteza muda wa kujadili hii intergration? Hata hivyo wakati wa maoni sehemu kubwa ya watanzania waliikataa.

Ninatofautiana na wewe kama kweli tunaweza kuwasaidia kwenye hili suala la ardhi. Ni gumu kuliko unavyoweza kufikiria. Sehemu kubwa za vurugu za Kenya ni ardhi. Na hii alieharibu ni Kenyatta na washirika wake mara tu baada ya uhuru walijimegea ardhi. Waulize waliofika kenya uone jinsi watu walivyo hozi ardhi. Sio leo wala kesho watakubali kugawia watu wasio na ardhi.

Nionavyo mimi hawa ndugu zetu wanataka kutumia hii intergration kama sehemu moja wapo ya kupunguza matatizo yao ya ardhi. Tutakaporuhusu watu kusafiri na kuhozi ardhi Tanzania basi wote wenye matatizo na ardhi kwenye hizo nchi watakimbilia TZ. Hii inamaanisha kwa kiasi kikubwa tatizo la ardhi kwao litapungua. Si unajua "kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi".

Labda nikuulize swali moja ndugu yangu Zero hebu tuambie faida moja tu wewe unaikosa kwa sababu hauko na ushirika na Kenya et la, na pindi hii intergration ikikubaliwa utaipata. Nitafurahi kuijua.

Njimba
 
Wakuu kabla ya kukataa jambo lolote ni vyema kwanza kutafuta msingi wa kukataa jambo lenyewe.

Bw/Bibi Ngongo (whichever), asante kwa mchango wako, ila huenda ulikosa kuchangia katika mjadala mzito wa Jumuiya ya Afrika mashariki ambao mpaka leo bado unaendelea. Msingi wa suala linaloongelewa hapa uko katika thread hii, Soma kwa makini, nadhani utapata mchango mzuri kabisa wa kuendeleza mjadala huu.


Asante tena.
Sasa kwa mlolongo wote huo wa matatizo ya ardhi kwa wenzetu, ni Mtanzania gani mwenye akili zake timamu atakuwa tayari kuungana nao katika kufanya ardhi iwe mali huru?
 
with the east african community there are issues that need be addressed first b4 we think we can renew the integration successfully ask
1.whether the break of the 1977 of community was it caused by among other factors the diversity in policies and then

2.whether this time diversity is not there

3.then whether self interest in the member countries exist or not

Then try to answer the issues in view of the current situation in the community.


note: when sane people have decided to launch a community,why do they look behind...where our presidents in 2001 forced and by whom
 


= Maybe?



...
 
Tanzania tuache kupinga hoja zifanyike research tupoteze mda mwingi maofisin let peolple go deep making researches iwe authority tunapokuwa tunaargue,ni kweli kwwnini na sisi tusiwe na mapendekezo yetu alafu ndo yakujadiliwa.unless otherwise tutaendelea kuonekana mabogus ktk jumuiya
 

Ajabu kabisa,inamaana mzee kweli kabisa hujasikia proposal na ajenda ya WaTZ?
Hivi ni upi msimamo wa kilinga na uvivu wa kufikiri kati ya hii

Kkushindwa kuona msimamo wazi wa jamii yako(ukosoaji pofu) V/s kutoa proposal mbadala wa ule usiouunga mkono(hata kama unajifanya hauuoni)?

FYI:WaTZ tunajua tunachotaka na hatupendi kuburuzwa katika hili
 
...seems humu ukiwa for federation wananchi wanakuita sio mtanzania,ukiwa una support Nkunda/Kagame sio Mtanzania,hii phony nationalism sijui watu wametoa wapi na ni hatari kweli kweli maana any extremism ya kuwaona wengine kama foreigners kwenye debate ndogo ndogo kama hizi nafikiri is beyond stupidity,sikatai kucheza na ardhi is a dangerous territory na ningependa iendelee kuwa mali ya Public kama ilivyo sasa ili kuzuia yaliyotokea kenya na kwingineko lakini jamani kwanini vitu kama passport/ID ambayo itasaidia free movements kwa wote kuanzia watalii,wafanyabiashara,goods& services na wananchi,nafikiri hii arrogance & disruption tunayoweka sasa itakuja kutu cost more kuliko tunavyofikiria,ndio majority ya watanzania hawataki Fed lakini kumbuka in History not always majority wanakuwa right....angalia sheria za marekani za kibaguzi kuanzia ndoa,elimu mpaka voting rights majority walikuwa wanasupport huo upuuzi,lakini 1948 california high court kwa mara ya kwanza ikapiga chini sheria ya kukataza mweusi na mweupe kuoana ingawaje majority walikuwa wanapinga ndoa za namna hiyo,anyway tuache kuitana majina humu la sivyo tutawaachia mjadili wenyewe
 
Hebu tupime mabaya na mazuri katika hii EAC, Kwa mtazamo wangu mabaya yanazidi mazuri na ndio sitaki kwenda hata mbali kwenye hayo mazuri, kwani mabaya machache ni tosha kumzindua Mtanzania yoyote akili.
Wasituzingue hawa akina Kamau, hawa watu wana matatizo kibao ambayo endapo tutaungana nao jamii yetu itazidiwa na itakuwa na shida kubwa. Nenda kule Kibera kaangalie mwananchi wa kawaida anaishi vipi? Viwango vya ujambazi,ukahaba na kadhalika umekithiri, hii yote ni kutokana na kuwepo kwa pengo kubwa la uwiano katika jamii yao, fananisha kibera na mji wowote Tanzania utapata picha kamili jinsi miji na mitaa ya Bongo itakavyobadilika pindi hio uncontrolled movenments of people itapitishwa. Tuna value zetu lazima tuzilinde, Bongo hata ukimkuta masikini kijijini lakini atakukarimu na sio rahisi ukakuta mtu ameuwawa na bado watu wanampita kama kwamba yule aliyekufa ni Kuku!
Kuuwana kwao ni jambo la kawaida, angalia jinsi wameuwana baada ya uchaguzi, Kisa ni ethnic proud nonsense waliyonayo hawa Wakenya!
Kenya, Uganda and Rwanda/Burundi they all have one thing in common 'Violent nature' kutokana na ethnics proud zao ambapo wakituletea huku hatutaweza kumudu hio hali. Angalia wakimbizi wao wakija mikoa kama Kagera jinsi wanavyoleta ushenzi wao.
Jambo jengine ARDHI, taratibu zao za ardhi ni mbovu, ndio ukaona kwa Mkenya wa kawaida ataishia kukodi na ndio wamoena hii itawapa mwanya wa kuvamia Ardhi ya Tanzania (hii sio siri)
Angalia hivi sasa kuna Bogus Marriage kibao zinafanyika Bongo, wanaume wa kikenya, Waganda, Wazambia, Wanaijeria, Wakaburu na Wachina wote wamekuja na mtindo wa kuwaowa dada zetu ili tu wapate makaratasi, kuendesha biashara na kununua maeneo, Serikali yetu bado imelala kwa hili na dada zetu hawajui Motive za hawa jamaa!! Mungu ibariki Tanzania.
 

Nakubaliana na wewe asilimia miamoja nakitu kingine lazima ukumbukee nikwamba, matatizo katika nchizote za Afrika yameanza katika migogoro ya ardhi. Juzi tu wakenya wame kimbizana kilammoja anamwambia mwenzake ondoka katika ardhi yetu rudi kwenu huko...Sasa Nyerere alipo tangaza kwamba ardhi ni mali ya serikali alifanya kitu cha msingi sana ndio maana watu tuliweza kwenda lila maali na "inter-marriges" ziliondoa sehemu kubwa ya ukabila. Kwahiyo hizi pamoja na nyingine nyingi za ha wenzetu kutafuta suluhu ya matatiozo yao ya ardhi ambayo yana jumuisha chakula haswa kwa Burundi na Rwanda, iabidi tulipinge sana!!!! Naomba tuanzishe mjadala nadhani mmoja ulikuwepo kuchambua swala la mafanikio Tanzania itapata kwa kujiunga na EA. Naomba viongozi wetu wote na wwananchi wapinge "land reforums". South Korea na nchi nyingine zina matatizohaya haya wana saini mikataba kila maali kutafuta sehemu za kupanda mazao kulisha watu wao. Watakua wana "export" hataama tuna njaa namna gani. Na hii itaua matarajio ya wafanya biashara wadogo wadogo wanaao uza chakula kwenye nchi jirani. We need to kill this stupid idea!!!!!!!!
 

Mzee, sina maana ya kuwasaidia ardhi yetu. Bali kuwasaidia katika land reform kutokana na matatizo tuliyaona.
 


Wewe acha **** hapa, leta point zako. Ulitaka nijiite nani. Mbona wewe hukutumia jina lako. Usijifanye kuwa na akili kwa elimu ya kujiendeleza.

Mimi sijasema kigezo unachokitumia wewe. Point yangu ni kwamba kama hatuna maslahi huko kwa nini tunang'ang'ania. Tusubiri wakati muafaka ndiyo tujiunge badala ya kupoteza pesa zetu bure. Hizo pesa zingeumika kujenga shule au barabara.

Mambo ya jumuiya ni ku-compromise. Halafu jiulize, kwa nini proposal zetu zina maslahi kwao wakati za kwao hazina maslahi kwetu???

Kama tumeshalijua tatizo kwa nini tusilifanyie kazi kwanza kabla ya kwenda mbele? 2013 siyo mbali. Sasa itakuwaje tuwe na Federation ambayo watu wake hawana uhuru wa kusafiri, kuuza na kufanya kazi mahali wanapopataka.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hebu jaribu kuchunguza athari ya kutumia ID kama njia ya kwenda nchi moja kutoka nyingine!!
Hivi at any one pint umewahi kusikia Mkenya akisifia sheria za ajira zinazohusiana na foreigners za Tz!! They always say Tz has very strict rules ila unajua ni wakenya wangapi wako Tz wakipata ajira na kulipwa vizuri pamoja na sheria zetu kuwa ngumu?? If that is possible then tujue kwamba ikifikia hatua ya kutumia IDs kama hati za kusafiria things will be worse!
 
 
Hakuna feasibility study yeyote iliyofanyika (sina taarifa kama ipo-ni ujinga wangu) kuhusu uanzishwaji wa EA Federation ! Fikiria kurekebisha mifumo yote-gharama zake ni kubwa kiasi gani-mfano elimu syllabus mpya?, passports/ID mpya kwa watu mil 100!(japo sio wote wana passports au kipande-IDs,nk. Ikumbukwe uunganishaji wa mifumo lazima kuna vigezo-sasa kenya serikali haijatulia baada ya uchaguzi ulioamuliwa kwa ukabila, uganada bado mkurya Kony anasumbua, Burundi taabu tupu, Rwnada akna mama ndo wametawala kwenye nguzo za kisiasa ! Hakuna platform iliyoandaliwa tayari kuunganisha mifumo hii, sasa hapo hiyo EA federation itasimama wapi? Tufanye mambo kisayansi ilie vizazi vijavyo vione kulikuwa kuna matayarisho, sio tulipuke kwa taamaa za watu kutaka ardhi na madini ya wenzao!
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…