Wallaahu mustaan, lakini fitna imeshavuruga akili na mitazamo ya viongozi wetu.
Punde tu mtu yeyote mwenye kuhoji au kusema ukweli ataadhibiwa sio kwa kubandikwa "ugaidi" tu bali ataitwa "mhaini".
Punde si punde Taifa letu litakamilika kugawika kimitazamo baina ya upande mmoja: waislamu wa kweli (ambao wanaikubali Shariah kwa mujibu wa Qurani na Sunna kuwa ni mfumo kamili wa kimaisha na kiutawala katika kila nyanja ya maisha, na kwa hiyo ni haki kwa nchi za waislamu kuitumia kama system, sio lazima hapa kwetu) upande mwengine: Wasiokuwa waislamu (kundi kubwa la wale wasio waislamu wa kweli/wanafiki (yaani secularists muslims:- kwa maana nafasi ya Sharia, Qur-ani na Sunna imeunganishwa katika nguzo ya kwanza ya uislmau-Shahada, na muislmau ambaye anavibeza, kuvifumbia macho au kuvikataa vitu hivyo, shahada yake huporomoka na kubakia kuwa mshirikina au mnafiki kama nilivyosema); au wenye imani nyenginezo zisizokuwa za kiislmau kwa mfano wakristo, na makafiri (wenye kuuchukia uislamu kwa kuuona kama kizingiti kwa matamanio yao machafu ya ulimwengu na walimwengu).
Hivi ndio kusema waislamu wa kweli waTanzania ndo magaidi au wahaini kwa kusema hivi?? Hivi ndio kusema wasiokuwa waislamu waTanzania ndio wana mapenzi sana na nchi yetu kuliko sisi? Huu ni upumbavu na matusi yasiweza kustahamilika maana sote vitovu vyetu vimezikwa katika ardhi hii ya Tanzania na kwa hiyo ni ardhi takatifu kwetu sote. Masuala ya ndani ya nyumba na kitaifa kama ufisadi, tuyaangalie kwa mapana na marefu yake, na vilevile masuala ya nje na kimataifa kama ugaidi tuyaangalia kwa mapana na marefu yake. TUSIBURUZANE....
Wasomali mwanzo wake ni mapigano wenyewe kwa wenyewe, na Al-Shabab imeibuka kutokana ndani ya "Baraza la Mahkama" lililotawala kiislamu (Shariah) kwa salama na amani nchini Somalia kwa kipindi kifupi cha miezi kama 9 mnamo 2006 kama sikosei, kipindi kilichokuwa na chenye neema na baraka ambao hakukuwa na mlio wa bunduki. Hii ilichafuliwa "kigaidi" na uvamizi wa Ethiopia uliofanywa chini ya remote control ya mabwana zao wa Magharibi kuuondosha utawala wa kiislmau uliokuwa unaanza kunawiri. Uvamizi ule wa kigaidi ndio uliogawa kundi la mahakama into 1) Waliokubali kuuza uislamu kwa bei chee ya kumoderate, kusecularise, demokrasi na utumbo utumbo wa mifumo mengine pamoja navo (serikali ya sasa) 2) Waliokataa kuuuza uislamu kwa bei hizo na kuamua kuurudisha hata kama italazimika kupigana jihadi (Hili ndio kundi la Al-Shabab). Kwa kifupi ni wenyewe kwa wenyewe. Nani asiyeweza ku-guess hapa kwamba Zionists, Marekani na washirika wao wata-support kundi gani hapa na kundi lipi watalibandika jina la "Magaidi" na parapaganda nyenginezo za kuwapaka matope wakati watazamaji wenye kufuata mkumbo wapooooo?
Miongoni mwa wenye kufuata mkumbo mpaka sasa: Swali linakuja!!!
Uganda ilishambuliwa na Al-Shabab kwasababu ya kushiriki kwao katika kufuata mkumbo kivitendo, Burundi wameonywa na Al-Shabab kwa kufuata kwao mkumbo kivitendo. Kenya wameanzwa kudokolewa dokolewa kwasababu ya kuvuka mipaka katika kufuata mkumbo kivitendo, maana hapana shaka mazungumzo na jirani yangewezekana. je sisi tumefanya nini ?????????????? hata Al-Shabab watushambulie??????? Au ndio katika kujaribu kuwapaka matope kidiplomasia kwamba wao kazi yao ni kushambulia na kuua tuu bila sababu yeyote ile achilia mbali sababu za msingi??