uanzilishwaji wake marekani sababu walioko sasa hivi sio wazawa wa kule wazawa ni wahindi wekundu ambao sijui hata kama bado wapo ambapo walipelekwa wazungu wakorofi kama adhabu na waafrika walioelimika ili wasiwaelimishe waafrika wengine ndio wakalitengeneza taifa la Marekani linaloonekana leo.hata marekani yenyewe sio nchi moja ni muunganiko wa majimbo*
Na kwa Tanzania wanaoishi hapa sasa hivi sio wazawa wa eneo hili ni kutokana na vita vya kupanua makoloni ndio ikawa watu wanatafuta mahali pa kujificha na kupata hifadhi ndio ikawa kila mtu anafikia kwake ndio maana nchi ina makabila zaidi ya 120 ikawa makabila yote yanamila tofauti na desturi nyingine baada ya uhuru na kuathiriana kwa lugha ili ipatikane moja ndio kikaja kiswahili kwa kuiba na kuchanganya maneno ya makabila mbalimbali ikapitishwa sera ya ujamaa ili kuyaunganisha sababu makabila 120 kuyaunganisha hivi hivi ingekuwa tatizo ambapo ndioa maana hadi leo watu wanajitahidi kuuhama ujamaa lakini bado tunautumia rafiki,jirani,yako ni ndugu yako.
kitu ambacho zinatofautiana ni Marekani imeundwa na wazungu wakorofi ambao walishindikana uingereza ( kikawaida mwizi anaekuibia kila siku anaakili na mipango mizuri kukuzidi) na waafrika walioelimika na Tanzania inaundwa na makabila ya wapiganaji waoga waliokuwa wanatafuta mahali pa kujificha wapate malazi.
Nahisi ndio maana kila kitu tunapuuzia mambo ya msingi kidogo tu tunaacha,umeme unakatika bila taarifa tuko kimya,watu wanaiba mahela mengi ya serikali ambao ndio sisi tuko kimya,watu wanadanganywa na kupelekwa mahakamani kesi inavuma miezi miwili tunapuuzia ,Dk kateswa watu wamesubiri arudi amechukua mwezi kimya watu wameshapuuzia, ishu za kagoda,Dowans,Richmond,Radar,Ndege ya Rais,Epa *watanzia hawana stori nazo tena sasa hivi wanawaza uamsho na kuchomwa makanisa nayo kidogo itapita, Balali kaonekana baada ya kusemekana alifariki kitambo nani amejali tena karudi na ishu za kisiasa anatabiri kifo cha CHADEMA,Hii ni kutokana na taifa ni la waoga na watu wa kukimbia ukweli na kujificha ili mambo yapite turudi na ndio maana kila anaepata madaraka anataka kula kwanza sababu anandugu zake wengi hawana kazi wanamtegemea na hawana kazi anafikiria kwanza mizigo yake na sio kazi yake na jina.