Tanzania ni sawa na Kichwa cha mwendawazimu

Mzalendo80

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
2,508
1,338
Kwa matukio yanayotekea katika nchi yetu inaonyesha wazi kuwa nchi ipo kwenye matatizo kuanzia wananchi mpaka haoa tunaowaita viongozi. Usome usisome ili mradi ukiwa mjanja basi utapata tenda zote , wengi wao hao wakandarasi ni wajanja janja, wamedanganya elimu zao, wanasiasa wengi wamedanganya elimu zao, wafanyakazi wengi wao walio serikalini wamedanganya elimu zao hakuna wakumuwajibisha wenzake, wote wapo sawa.

Hatuwezi kupata maendeleo tukiwa sisi wenyewe wananchi ndio kikwazo cha hayo maendeleo, kila uchaguzi ukija bado tunawapigia wanasiasa wa kichina (Fake) elimu zao za kuunga unga halafu tutegeme maendeleo katika Taifa letu.

Kama barabara zingekuwa zinaanguka kama magorofa ni barabara ngapi zingekuwa zimeshaua watanzania kama magorofa feki yavouwa katika kuporomoka au kuanguka?

Wakuu wengi wa wilaya na mikoa ni vihiyo, wengi wao hawana uwezo wa kuongoza au kuleta maendeleo katika hizo sehemu. Wapo wapo tu tena kimaslai ya mtu fulani au kulipana fadhila. Wakuu wa wilaya na Mikoa wengi ni wanajeshi waliostaafu wasio na uwezo wowote wa kielimu na hata hao walio na elimu bado hawajastaarabika.

Tanzania imekuwa ni kichwa cha mwendawazimu kila mtu anataka kujaribia mkasi wake au wembe kunyolea. Kisa mmoja wao alijaribu na kufanikiwa basi ameonyesha njia kwa wendawazimu wenzake
 
Back
Top Bottom