Tanzania ni nchi yenye mali nyingi

Tanzania ni nchi yenye mali nyingi

EDWIN BAJUNGU

New Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
4
Reaction score
3
Amka Tanzania, amka kutoka katika usingizi bandia. Kaeni macho, kuweni chonjo, sasa semeni kuibiwa basi.

Wametuibia sana, wametunyonya sana, wameigeuza Tanzania shamba la bibi. Wametajirika kwa rasilimali zetu.

Ndiyo wametajirika kwa madini yetu, wanyama wetu, malighafi kutoka katika mashamba yetu, mifugo na samaki wetu. Sasa tunasema kuibiwa tena basi.

Madini tutachimba wenyewe, hatukubali tena ulaghai kuwa tuna teknolojia ndogo hatuwezi kuchimba madini wenyewe.

Ulaghai huo hauna nafasi tena kwani wachimbaji wetu wadogo wamefanikiwa kupata madini mengi na makubwa kuliko yaliyowahi kupatikana kupitia wawekezaji wageni.

Wachimbaji wadogo wamelipa kodi vizuri na serikali kupata mapato makubwa kuliko yaliyowahi kupatikana kutoka kwa wawekezaji wageni.

Tanzania ni nchi Tajiri sana, utajiri wetu lazima tuulinde. Lazima wananchi wetu wafaidi utajiri wa nchi yao Tanzania.

Ni muhimu kuulinda utajili wetu usiporwe na wanyonyaji, mafisadi, mabeberu na vibaraka wao.

Ndiyo maana tunamuhitaji Rais John Pombe Magufuli ili atuongoze kulinda na kudhibiti utajiri wetu usiporwe.
 
Tanzania ni nchi tajiri ila yenye viongozi wachumia tumbo akiwemo huyo magu.

Pia ni nchi yenye wajinga wengi kama wewe na ndio maana mali zetu zinaibiwa kizembe.
 
Una habari kuwa makinikia bado yanasafirishwa nje ya nchi kwa kibali cha Magufuli siku hizi? Bado hajatatua tatizo, yapo mengi tu na ameshindwa sana, hata ujenzi wa barabara hatujafikia kiwango cha enzi za Mkapa na Kikwete.
 
[emoji445][emoji1623][emoji442][emoji441]Tanzania Tanzania, nchi yenye mali nyingi watu wengi wa ulaya wanaililia sana.....

Mwenye mashairi ya huu wimbo naomba
 
KISWAHILI huwa ni kigumu aiseh
Mali haina maana nzuri kama ingiita natural resources'
Sasa ukishaiiita natural resources biashara imeisha maana uipeleke kwenye matumizi gharama ni kubwa kuliko resource yenyewe.
Yaan extraction process, exploitation procedures, harnessing activities are more costly than the resources itself. Aiseh maisha haya kama una technology, Capital, unskilled up to specialised labour utabakia unatoa macho tu na resource zako
 
Una habari kuwa makinikia bado yanasafirishwa nje ya nchi kwa kibali cha Magufuli siku hizi? Bado hajatatua tatizo, yapo mengi tu na ameshindwa sana, hata ujenzi wa barabara hatujafikia kiwango cha enzi za Mkapa na Kikwete.
Afadhali ya sasa kuna malipo. Pia serikali ina watu wake kule ndani ya migodi. Magu kaweka watu wanaotoa taarifa tena wengine hata hawajuani ole wako ule taarifa ya uongo.
 
KISWAHILI huwa ni kigumu aiseh
Mali haina maana nzuri kama ingiita natural resources'
Sasa ukishaiiita natural resources biashara imeisha maana uipeleke kwenye matumizi gharama ni kubwa kuliko resource yenyewe.
Yaan extraction process, exploitation procedures, harnessing activities are more costly than the resources itself. Aiseh maisha haya kama una technology, Capital, unskilled up to specialised labour utabakia unatoa macho tu na resource zako
Poor thinking. Libya ilikuwa maskini, mafuta yalipogundulika pakawa keki ya dunia
 
JIWW ANACHOWEZA NI KUPAMBANA NA KUWAKOMOA VIONGOZI WA CHADEMA.

KATIBA SHERIA UTAWALA BORA UTAJILI WA NCHI NK YEYE HAVIJUI.
 
Wewe acha bangi sasa huu uharo wote hapa Tanzania kauleta nani si hicho chama chako cha CCM. unafahamu kama sasa ni miaka 60 tangu CCM waanze kutawala hapa bongo na huyo Magufuli wako anafata muongozo wa CCM. mzee usitulete bla bla hapa
ADUWI NAMBA MOJA WA TANZANIA NI CCM. FULL STOP.
 
Tanzania ni nchi tajiri ila yenye viongozi wachumia tumbo akiwemo huyo magu.

Pia ni nchi yenye wajinga wengi kama wewe na ndio maana mali zetu zinaibiwa kizembe.

Toka umezaliwa mpaka leo umesaidia nn hii Nchi kama sio kulalamika? we ni mzigo kwenye hii Nchi
 
Pole sana. Bahati mbaya inaonekana uelewa wako ni mdogo sana kuhusiana na madini. Ungekuwa na uelewa japo kidogo sana, ningekuambia kwa nini tumepotea njia.

Miaka 5 ijayo, uchimbaji mdogo utakuwa umekoma au unaelekea kukoma. Tukibahatika kuwa hai, utaelewa wakati huo. Na nitakueleza kwa nini umekoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom