Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,932
Katika kuielezea nchi ya Tanzania katika maandishi mbalimbali ya kitaaluma na mengineyo, tunasoma kuwa baadhi ya sifa za kuielezea Tanzania, ni kuwa ni nchi ya kidemokrasia. Viongozi wetu, wanapokuwa katika majukwa mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, huitambulisha Tanzania kama nchi inayofuata mfumo wa kidemokrasia. Hata hivyo, hebu tukae pembeni ya misemo hiyo na tuanze kujiuliza kuwa , Je! Tanzania ni nchi ya kidemokrasia?
Nchi inayoendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia ni ile ambayo wananchi wake wote kwa ujumla, kupitia kwa wawakilishi wao, wanahusishwa katika shughuli, maamuzi na mipango ya maendeleo ya maisha yao na nchi kwa ujumla. Katika nchi ambayo kikundi kidogo cha watu, kinafanya maaamuzi juu ya maisha na maendeleio ya nchi, tunaweza kusema kuwa nchi hiyo haiongozwi katika misingi ya kidemokrasia, hata kama vyombo vya kidemokrasia vimo humo.
Ili mfumo wa kidemokrasia uweze kushamiri na kuendeleo, inabidi mawazo ya kidemokrasia yajengeke katika watu wanaohusika. Ni lazima wawe na imani katika demokrasia. Kama watu hawatakuwa na imani katika demokrasia, hawataweza kutekeleza vitendo vya kidemokrasia kwa uhalisi.
Tumekuwa tukisikia misemo mbali mbali ya kupinga demokrasia kutoka kwa midomo ya hao hao wanaosema kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia. Maneno hayo ni kama: 'CCM itatawala milele', 'Vyama vya upinzani ni upepo tu, utapita' na mengine mengi.
Cha kushangaza ni hao hao tuaowaona katika majukwaa hapa nchini na hata nje ya nchi wakiimba wimbo wa demokrasia. Huo ni unafiki. Hawapendi demokrasia iwepo. Hao ni maadui wa demokrasia.
Nchi ya Tanzania ipo katika njia ya kuelekea kupata demokrasia, na njia hiyo ina vikwazo vingi.Kwa Watanzania, wapenda maendeleo na mabadiliko, nabidi tuviruke hivyo vikwazo ili tufike huko tunakotaka. Njia moja pekee ni kuondoa hao wanaokwamisha demokrasia kwa maneno na matendo yao.