Tanzania ni nchi ya chama kimoja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ni nchi ya chama kimoja?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kitalolo, Jan 7, 2011.

 1. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikijiuliza ikiwa Tanzania ni nchi ya chama kimoja ni vizuri watanzania tukajulishwa rasmi ikiwa tumeruhusu au kusajili vyama vingi na haviruhusiwi kuendesha shughuli zake au kushiriki kama vyama vya siasi katika utendaji wa majukumu yanayovipasa vyama vya siasa iwapi dhana ya vyama vingi hapo?
  nimeangalia sana ikiwa shughuli fulani ni ya ccm wao wana haki ya kufanya chochote wakisema wanaandama kumpongeza kiongozi wao aliyeteuliwa kugombea nafasi fulani kwao ni ruksa lakini wapinzani wakitaka kuandamana kwaajili ya shughuli kama hiyo basi wao wataambiwa inaonekana kutatokea uvunjaji wa amani hivyo maandamano hayo si halali.
  naona kwamfano nguvu iliyotumika kuyazima maandamano ya Arusha ingeweza kutumika nusu au robo ya nguvu hiyo kuyalinda na yangemalizika kwa amani bila ya kupoteza maisha wala kutumia mabomu na magari ambayo yemetumika na inamaana wametumia gharama kubwa sana kuzima maandamano badala ya kutumia gharama kidogo kuyaongoza na yangeisha kwa amani. nimeona hata idadi ya polisi waliokuwepo arusha na ambao bado wapo ni wengi sana na wengi sio wenyeji wa hapa inamaana waliletwa kwa operation maalumu huko kote walipoletwa kuna gharama zilitumika kuwasafirisha na kuna gharama kubwa sana inatumika kuwaweka arusha kwa oparation hiyo achilia mbali gharama zilizotumika hata kuwahudumia majeruhi.
  nijaribu kuiaghalia gharama hiyo iliyotumika kuleta madhara ingeweza kubadilishwa kwa kulipia ada za vyuo vya ualimu, kununua madawa hospitali , kupunguza deni la dowans ambalo limebeshwa wananchi kwa kuongeza bei za umeme, ujenzi wa barabara za manispaa ya arusha ambazo ni mbovu kuliko za baadhi ya zilizoko vijiji kuongeza vitanda kwenye ward ya mount meru hosp. wakati nikitafakari hayo najaribu pia kutafsiri aina ya viongozi au watawala tulio nao je huwa wanaona upande wa pili wa shilingi?
  je kama hawataki vyama vingi kwanini wasivifute tu na inchi yetu ikabaki kuwa ya chama kimoja kinachosema wanailinda amani ya nchi hii na kwamba amani hiyo inavurugwa na vyama vya upinzani? pia kama unaweza kuandaa uchaguzi kwa gharama kubwa na kuwaambia wananchi kuwa uchaguzi ni wa vyama vingi iweje uchakachue matokeo na kutangaza matokeo kinyemela? ni heri kuwa na chama kimoja uchaguzi ukiisha kimeshinda tunaendelea na mambo yetu.
  kuna watu wameathirika kwenye biashara zao kwa vile tu wameingia kwenye vyama vinavyoitwa nya upinzani najiuliza hivi ni vyama vya uopinzani au ni vyama vya kisiasa? je siku sisiemu ikiondoka kwenye uongozi itabaki kuwa chama cha siasa au chama cha upinzani? kwanini kama umekwisha anzisha mfumo wa vyama vingi usitoe uhuru kwa wananchi wa kuabudu kwenye hivyo vyama vyao? kama hatuna uhuru huo hakuna haja ya kutangaza kuwa nchi hii ina mfumo wa vyama vingi. kuna shuhuda nyi ngi zitakuja hapa kuashiria kwa mwenendo huu hatuna haja ya kujitangazia kuwa tua vyama vingi katika nchi hii. maana hata sasa ujanja unaotumiwa na sisiemu ni kutangaza kuwa vyama vingine vya siasa ni vyama vya upinzania ni ni vyama vya fujo na kwamba viongozi wao ni watu wa fujo tu kitu mabacho sio cha kweli ikiwa serekali inajua kuwa vyama hivyo ni kama kile cha mungiki je kwa kutumia mamlaka iliyonayo kwanini isivifute? na nchi ikawa na amani na salama ?
  kwanini tunajidanganya kwamba tuna vyma vingi wakati tunataka chama kimoja? pengine mtanipa mwanga ili nami nione umuhimu au nafasi ya vyama vingi vya siasa TAnzania.

  naomba kutoa hoja
   
Loading...