Tanzania ni mwenyeji wa mkutano wa mawaziri wa Sekta zaMazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwaAfrika (SADC)

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atafungua mkutano wa Mawaziri wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC) Jijini Arusha.

Mkutano huo unatanguliwa na ule wa makatibu wakuu na watendaji wa wizara za Maliasili, Utalii na Mazingira kutoka nchi za SADC ambao unafunguliwa leo Oktoba 21, 2019 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Aloyce Nzuki amesema jana kuwa mkutano huo utajadili mwenendo wa hali ya mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa na hali ya utalii na misitu katika nchi za SADC.

Dk Nzuki amesema mkutano huo wa kisekta ndani ya SADC, pia utajadili juu ya utekelezaji wa mikakati ya hifadhi na usimamizi wa mazingira na kupitia mikakati na miongozo juu ya masuala hayo katika kutekeleza majukumu ya kila nchi ndani ya SADC.

Amesema mkutano wa Mawaziri wa sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii utatanguliwa na mikutano ya wataalamu wa sekta ya wanyamapori na mkutano wa makatibu wakuu wa sekta za mazingira, maliasili na utalii utakaoanza leo Jumatatu Oktoba 21 hadi 24, 2019

Dk Nzuki amesema mikutano hiyo miwili itajadili na kuandaa mapendekezo yatakayowasilishwa katika kikao cha mawaziri kitakachofanyika Ijumaa Oktoba 25, 2019 kwa uamuzi na maelekezo.

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda wa Wizara ya Mambo ya Nje, Agness Kayola aliliambia Mwananchi kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 wanachama wa SADC wanaotekeleza mkakati wa SADC kuhusu usimamizi wa sheria na vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori.

Alisema mkutano huo ni muhimu kwa Tanzania kama mwenyekiti wa jumuiya hiyo.
 
Back
Top Bottom