Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,555
- 41,064
Majanga ya kiasili yanatajwa ni miongoni mwa matukio ambayo ni vigumu sana kujikinga nayo kwa 100%, kwa sababu mengi hutokea katika scale kubwa na hivyo kuwanyima watu sehemu ya kukimbilia.
Hata hivyo, mataifa mbalimbali, yakipatwa na majanga hayo, hujitahidi kuyatumia majanga hayo kama msingi wa kujilinda dhidi ya mengine ya namna hiyo endapo yakitokea tena. Katila kufikia hilo, mambo mbalimbali hufanyika, kama vile:
1) Kuangalia maeneo mengine yaliyo prone kwa janga kama lililotokea.
2) Kutengeneza mifumo thabiti ya predictions na uokoaji kama endapo yakitokea tena eneo jingine.
Je, sisi Tanzania, majanga ya awali yamekuwa yanatufunza chochote?
Landslide iliwahi kutokea miaka ya nyuma huko Same. Watu walipoteza maisha na mali. Landslide kubwa na mbaya zaidi ilitokea huko Uganda, tulishuhudia na tukaenda kutoa pole kwa hawa majirani zetu.
Kwa upande wetu Tanzania, janga lile lile lililokuwa limetokea Same, limetokea Hanang, tena kwa scale kubwa zaidi. Watu wamepoteza maisha na mali, na uwezo wetu wa uokozi bado upo duni vilevile kama ilivyokuwa wakati ule, na mipango yetu ya makazi imeendelea kuwa holela vile vile kama ilivyokuwa siku hizo za nyuma.
Angalia miji kama Mwanza. Fikiria siku likitokea hata tetemeko dogo la ardhi, jinsi yale mawe makubwa yasiyo na mzizi yaliyo juu ya vilima, yatakapoporomoka kushuka chini.
Ifikirie pia Dodoma, mji mkuu uliobuniwa na wanasiasa bila ya kuwashirikisha wataalam. Dodoma ipo kwenye Rift Valley, hizi ni deep rooted structures ambazo zinalifanya eneo la Dodoma kuwa earthquake prone. Wanasiasa waliposhituliwa kuwa eneo ni hatari kwa matetemeko, CDA wakati huo ikatoa mwongozo kuwa majengo yote ya ghorofa Dodoma, yasizidi ghorofa 3. Leo maelekezo hayo yamepuuzwa au yamefutwa kimyakimya, na inaonekana unaweza kujenga jengo la urefu wowote. Tena jengo la Waziri mkuu lipo juu mlimani, juu ya mawe, labda wanataka likitokea tetemeko, yeye awafikie wahanga wengine kwa kutokea juu.
Watawala na wapanga mipango na miji yetu, sijui ni kwa kukosa maarifa, kukosa akili, au ni kwa uzembe au kwa kupuuza, hawajui kuwa maafa makubwa ya matetemeko ya ardhi, hasa epicenter inapokuwa nchi kavu, yanasababishwa na majengo marefu.
Hii nchi, kama watu wataendelea kupeana vyeo kwa kuangalia ni nani chawa wa Rais, ni nani chawa wa CCM, au ni nani kada mzuri wa CCM, hakika hakuna mahali popote au eneo lolote tutakalofanikiwa.
Poleni sana wafiwa na waathirika wote wa landslide ya Hanang. Lakini inasikitisha zaidi kwa sababu tuna mazingira yanayopalilia majanga mengi ya aina hiyo na aina nyingine kuendelea kutokea katika miaka ijayo.