Tanzania ndani ya China

Tanzania ndani ya China

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
227
Reaction score
599
Hivi karibuni niliwahi kutembelea jengo moja lililopo katika mji mmoja nchini China. Kitu kilichonishangaza ni kwamba nilijikuta ghafla nimetokezea nchini Tanzania baada ya kuingia ndani ya jengo hilo lenye ghorofa moja.

Hata hivyo niliporudi nje ya jengo nilijikuta tena ndani ya nchi ya China, nikabaki nimepigwa butwaa. Nikajiuliza inamaana huku nako kuna uchawi mpaka nakutana na mapichapicha hayo?

Baada ya kutazama na kuulizia vizuri ndipo nikasimuliwa ukweli wa mambo hayo kama ifuatavyo;

Jengo lipo katika mji wa Changchun-China, ni jengo la makumbusho ya Sanaa za Kimakonde. Ni maarufu kwa jina la Makonde Arts.

Jengo zima chini hadi juu limepambwa kwa vinyago mbali mbali vinavyotengenezwa na wamakonde nchini kwetu Tanzania. Kuta zote zimepambwa kwa picha mbalimbali za utamaduni wa Kitanzania. Kwa kifupi ni kama uko Tanzania ndani ya China.

Unapoingia tu ndani ya jengo unakutana na hotuba za Kiswahili za Rais wa wa awamu ya tatu na ya nne wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Benjamin W. Mkapa pamoja na Mhe. Jakaya M. Kikwete. Pia kuna picha ya Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius K. Nyerere.

Kwakuwa tulikuwa katika ziara ya kitarii tukiwa kundi kubwa la watu kutoka nchi mbalimbali, Watanzania tuliokuwa wa nne tulijiskia furaha sana kwakuwa kila mtu alianza kutuangalia sisi na kutuuliza maswali mengi kuhusu Tanzania.

Jambo hili ni jema sana kwakuwa ni namna ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwetu Tanzania ikizingatiwa kwamba makumbusho hayo yanatembelewa na Maelfu ya watu kutoka nchi mbalimbali.

Kwa upande mwingine nilijisikia vibaya sana kwakuwa sijawahi kutembelea makumbusho kama hayo nchini kwetu Tanzania na sijui kama yapo au hayapo.

Pamoja na kwamba nimeshatembelea chuo cha sanaa Bagamoyo ambapo kazi hiyo ya uchongaji hufanyika, sijawahi kutembelea makumbusho ambako ningeweza kupewa historia ya uchongaji huo na namna unavyofanyika.

Suala la kujifunza kwa viongozi wa serikali yetu ni kwamba, wenzetu wanathamini sana vitu vidogo na kuviongezea thamani.
 
Back
Top Bottom