Tanzania na Upinzani Kanjanja

Tanzania na Upinzani Kanjanja

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2017
Posts
403
Reaction score
211
Tangia uongozi wa awamu ya tano uingine madarakani; mengi yameanza kuonekana kuhusu uhalisia wa upinzani wa taifa hili. Upinzani katika nchi hii umekosa muelekeo ya nini wanakitaka na kukisimamia. Hoja za msingi wananchi walizozitarajia kutoka kwao zimeyeyuka.

Hususani hoja ya kupiga vita rushwa na ufisadi, kutowajibika na uzembe kwa serikali na mengineyo. Wananchi wanataka kuona upinzani uliosimama kwa kupigania haki zao na kujenga hoja za maendeleo ya taifa hili.

Wananchi wanataka rasilimali za taifa hili zisaidie kunufaisha taifa hili sio kuibiwa na wageni. Wapinzani wamekuwa na utamaduni wa kukosoa kauli za rais na watendaji wake bila kuja na hoja mbadala. Kiufupi upinzani katika taifa hili umekuwa hauna dira wala muelekeo wa nini hasa wanaona mbadala katika kuleta maendeleo ya taifa hili.

Kuna hoja wanasimamia kusema CCM imeongoza miaka 50 lakini hakuna maendeleo. Hivi hawa jamaaa wanaelewa tumetoka wapi. Mi niwakumbushe kidogo tu; miaka ya 1970's usafiri ulikuwaje Tanzania. Ulikuwa unasafiri siku ngapi kutoka Dar hadi Songea ama Arusha.

Pili; idadi ya wasomi walikuwa wangapi na sasa wako wangapi; vipi kuhusu maendeleo ya miji na mikoa ilikuwaje kulinganisha na sasa (najua kuna watu humu wanapicha ya Dar es Salaam miaka ya 1970's, maybe wakiwawekea mtaweza kuelewa tuliko toka). Vipi kuhusu upatikanaji wa nishati ya maji na umeme ilikuwaje ukilinganisha na sasa.

Kama hoja ni hii, swali ni kwamba upinzani unaleta hoja ipi mbadala ya kupaisha taifa hili katika maendeleo ya haraka kiasi wanachoota wao? Ili upinzani wa Tanzania usionekane kanjaja naomba wadau mtuambie tu; ni vitu gani mtakavyoleta kwa muda mfupi tufikie hayo maendeleo mnayosema CCM imeyashindwa kwa muda wa miaka hamsini?

Naomba kuwasilisha.
 
Yaani wewe jamaa mweupe sana yaani social services na basic needs ambazo ni haki kwa wananchi ndio unaisifia serikali?? Ulitaka nani ajenge lami ?? Ulitaka nani ajenge shule hizo?? ni basic needs kma vile baba kumpeleka mtoto shule au kumnunulia chakula hivyo sio kitu cha kuboast ongeleeni vitu ambavyo vitaivusha nchi kutoka kwenye umaskini mfano kilimo na uchumi sio mnashangilia barabara mwaka wa 50 huu ni aibu kwa kijana msomi kma ww
 
Hata kujibu upuuzi unaonekana nawe ni zaidi ya mpuuzi.
Kma upinzani hauna hoja ya maana je umeshawahi kupitia hata hotuba ya KUB kwa wizara mbali mbali pale bungeni???

Je umewahi pitia ilani ya uchaguzi chadema 2015-2020

JE umesoma bajeti kivuli yoyote toka umeanza kufuatilia siasa

Tuanzie hapo kwanza
 
Yaani wewe jamaa mweupe sana yaani social services na basic needs ambazo ni haki kwa wananchi ndio unaisifia serikali?? Ulitaka nani ajenge lami ?? Ulitaka nani ajenge shule hizo?? ni basic needs kma vile baba kumpeleka mtoto shule au kumnunulia chakula hivyo sio kitu cha kuboast ongeleeni vitu ambavyo vitaivusha nchi kutoka kwenye umaskini mfano kilimo na uchumi sio mnashangilia barabara mwaka wa 50 huu ni aibu kwa kijana msomi kma ww

Kiongozi unajua multiplier effects ya kuimarika kwa usafiri katika taifa? Hayo maendeleo ya kilimo yatawezekana bila miundombinu ya barabara.

Watu wanahitaji wakizarisha bidhaa za kilimo zifike katika masoko sasa watafikishaje bila miundombinu ya barabara.

Pili; tuna different aspect of development; including social development, political development, human development and economic development na hivi vyote vina mahusiano ya moja kwa moja na kuimarika kwa huduma za jamii na miundombinu.

Mi nazani ungeenda kwenye swali langu la awali katika mada, ungejibu lile ingekuwa poa sana.
 
kwa kweli inasikitsha,kama sasa hivi resources zote zinazopelekwa Mwanza,hakuna hata kupaza sauti kwamba mkuu anakosea,wapinzani wote waliohama,taifa halitawasamehe kamwe.
 
kwa kweli inasikitsha,kama sasa hivi resources zote zinazopelekwa Mwanza,hakuna hata kupaza sauti kwamba mkuu anakosea,wapinzani wote waliohama,taifa halitawasamehe kamwe.
Kwani ni rasilimali kiasi gani zinaelekezwa Dodoma mbona hatusemi. Kiasi gani cha pesa kinaelekezwa kanda za kusini katika kuanza kuimarisha South Corridor?
 
Sasa hivi kuna hoja ya kuporomoka kwa uchumi. Wapinzani wangekuwa wanauwezo wa kulisemea hili kwa namna ambayo italiwekawa wazi kwa wananchi, nadhani wangepata support, kwa sababu wananchi wanaona ugumu wa maisha unavyoongezeka kwa kasi. Lakini sasa hivi wapinzani wako sokoni tu wanasubili kununuliwa.
 
Kwani ni rasilimali kiasi gani zinaelekezwa Dodoma mbona hatusemi. Kiasi gani cha pesa kinaelekezwa kanda za kusini katika kuanza kuimarisha South Corridor?

mie sijui aisee,kungekuwa na balance ya kutumia hizo resources,tusingekua na manung'niko,mkuu keki ya taifa ni yetu sote
 
Sasa hivi kuna hoja ya kuporomoka kwa uchumi. Wapinzani wangekuwa wanauwezo wa kulisemea hili kwa namna ambayo italiwekawa wazi kwa wananchi, nadhani wangepata support, kwa sababu wananchi wanaona ugumu wa maisha unavyoongezeka kwa kasi. Lakini sasa hivi wapinzani wako sokoni tu wanasubili kununuliwa.
Hiyo hoja ni mzuri lakini unabidi uitengeneze kitaalam zaidi. Kwa kuporomoka kwa uchumi (economic recession and depression) zina indicator muhimu ambazo zisipofanyiwa kazi zinaweza kuharibu uchumi. Wanasiasa wetu nao ni shida sometime.
 
Kiongozi unajua multiplier effects ya kuimarika kwa usafiri katika taifa? Hayo maendeleo ya kilimo yatawezekana bila miundombinu ya barabara. Watu wanahitaji wakizarisha bidhaa za kilimo zifike katika masoko sasa watafikishaje bila miundombinu ya barabara. Pili; tuna different aspect of development; including social development, political development, human development and economic development na hivi vyote vina mahusiano ya moja kwa moja na kuimarika kwa huduma za jamii na miundombinu. Mi nazani ungeenda kwenye swali langu la awali katika mada, ungejibu lile ingekuwa poa sana.
Nlikuuliza haya hukujibu bado hujajibu ili twende kwenye mada

Kma upinzani hauna hoja ya maana je

umeshawahi kupitia hata hotuba ya KUB kwa wizara mbali mbali pale bungeni???

Je umewahi pitia ilani ya uchaguzi chadema 2015-2020

JE umesoma bajeti kivuli yoyote toka umeanza kufuatilia siasa

Tuanzie hapo kwanza
 
Kiongozi unajua multiplier effects ya kuimarika kwa usafiri katika taifa? Hayo maendeleo ya kilimo yatawezekana bila miundombinu ya barabara. Watu wanahitaji wakizarisha bidhaa za kilimo zifike katika masoko sasa watafikishaje bila miundombinu ya barabara. Pili; tuna different aspect of development; including social development, political development, human development and economic development na hivi vyote vina mahusiano ya moja kwa moja na kuimarika kwa huduma za jamii na miundombinu. Mi nazani ungeenda kwenye swali langu la awali katika mada, ungejibu lile ingekuwa poa sana.
Najua impact ya miundombinu ila sikutegemea ndio uyaseme kma mafanikio ya CCM kwa sababu hizo ni basic needs mfano hospitali barabara maji ulinzi n.k hayo ni lazima serikali iyafanye maana bila hayo wananchi hawawezi survive so sitegemei useme ni achievement ya CCM kwa miaka 50 sababu ni WAJIBU WA SERIKALI

ila mafanikio halisi ni kubadilisha wellbeing ya wananchi politicaly economically na socially sasa huongelei kuwa kwa miaka 50 sasa watanzania wanasurvive chini ya dollar 2 kwa siku 3...... huongelei zaidi ya nusu ya watanzania ni maskini haswaaaaa.... Huongelei zaidi ya nusu ya watanzania wanashindia milo miwili kwa cku haya ndio yakuongelea kma mafanikio na failure ya ccm sio shule hospitali na barabara maana hizo NI MAJOR ROLES ZA SERIKALI NA NI HAKI KWA MWANANCHI

ahsante
 
Nlikuuliza haya hukujibu bado hujajibu ili twende kwenye mada

Kma upinzani hauna hoja ya maana je

umeshawahi kupitia hata hotuba ya KUB kwa wizara mbali mbali pale bungeni???

Je umewahi pitia ilani ya uchaguzi chadema 2015-2020

JE umesoma bajeti kivuli yoyote toka umeanza kufuatilia siasa

Tuanzie hapo kwanza
Kiongozi hoja mbadala za kibajeti kisekta na kijumla wake huwa nazifuatilia sana. Mimi ni mfuasi wa kufuatilia bajeti kwa kuwa ikipitishwa either inamadhara ama faida kwa shughuli zangu za kiujasiliamali. Katika bajeti nyingi za upinzani zinazosomwa bungeni kuanzia bajeti ya 2016/2017 na 2017/2018 sijaona mikakati mbadala ya kuimarisha sekta inayotolewa na vyama vya upinzania. Zaidi ya kukosoa pale palipo na changamoto. Bajeti mbadala inatakiwa kueleza changamoto na nini chama pinzani kingefanya kuimarisha sekta katika taifa hili. Nilifuatilia bajeti kivuli ya Fedha na Mipango mwaka 2017/2018 nikasema tuna kazi. Nakuomba wewe ipitie kiundani uone.
 
Najua impact ya miundombinu ila sikutegemea ndio uyaseme kma mafanikio ya CCM kwa sababu hizo ni basic needs mfano hospitali barabara maji ulinzi n.k hayo ni lazima serikali iyafanye maana bila hayo wananchi hawawezi survive so sitegemei useme ni achievement ya CCM kwa miaka 50 sababu ni WAJIBU WA SERIKALI

ila mafanikio halisi ni kubadilisha wellbeing ya wananchi politicaly economically na socially sasa huongelei kuwa kwa miaka 50 sasa watanzania wanasurvive chini ya dollar 2 kwa siku 3...... huongelei zaidi ya nusu ya watanzania ni maskini haswaaaaa.... Huongelei zaidi ya nusu ya watanzania wanashindia milo miwili kwa cku haya ndio yakuongelea kma mafanikio na failure ya ccm sio shule hospitali na barabara maana hizo NI MAJOR ROLES ZA SERIKALI NA NI HAKI KWA MWANANCHI

ahsante
Nakuambia kiongozi, kuhusu politically, economically and socially serikali ya CCM imefanikiwa kuleta umoja wa kitaifa unaoleta tija katika kuendeleza mafanikio unayoyaona ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa sasa. Wastani wa kipato cha mtu mmoja umekuwa ukiongezeka siku hadi siku. Uwezo wa wananchi kumiliki ardhi iliyorasimi kwa shughuli za uchumi unaimarika. Kwa sasa idadi kubwa ya ardhi vijijini inapimwa na kupewa hati za kimila.
 
Kiongozi hoja mbadala za kibajeti kisekta na kijumla wake huwa nazifuatilia sana. Mimi ni mfuasi wa kufuatilia bajeti kwa kuwa ikipitishwa either inamadhara ama faida kwa shughuli zangu za kiujasiliamali. Katika bajeti nyingi za upinzani zinazosomwa bungeni kuanzia bajeti ya 2016/2017 na 2017/2018 sijaona mikakati mbadala ya kuimarisha sekta inayotolewa na vyama vya upinzania. Zaidi ya kukosoa pale palipo na changamoto. Bajeti mbadala inatakiwa kueleza changamoto na nini chama pinzani kingefanya kuimarisha sekta katika taifa hili. Nilifuatilia bajeti kivuli ya Fedha na Mipango mwaka 2017/2018 nikasema tuna kazi. Nakuomba wewe ipitie kiundani uone.
Ina maana hata hukuona suggestion ya upinzani ya bajeti kupunguzwa ukubwa ili itekelezeke 100%?? Hyo hukuiona

Hukuona suggestion kuhusu vyanzo vipya vitatu kma source of income kufund bajeti as proposed na halima mdee kwenye bajeti kivuli???

Je unazungumziaje hayo mapendekezo mawili ya upinzani je yalikuwa hayana tija..... Tuanzie hapo kwanza
 
Nakuambia kiongozi, kuhusu politically, economically and socially serikali ya CCM imefanikiwa kuleta umoja wa kitaifa unaoleta tija katika kuendeleza mafanikio unayoyaona ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa sasa. Wastani wa kipato cha mtu mmoja umekuwa ukiongezeka siku hadi siku. Uwezo wa wananchi kumiliki ardhi iliyorasimi kwa shughuli za uchumi unaimarika. Kwa sasa idadi kubwa ya ardhi vijijini inapimwa na kupewa hati za kimila.
Whatever ila nachojua bado watanzania zaidi ya 70% wanategemea kilimo na kilimo kipo ICU sasa huoni mnawamaliza hao??

Je huoni kma CCM wangeweka bajeti kubwa wizara ya kilimo pia maji na umwagiliaji ili kuboost agriculture na kupotezea kwanza mabombardier na viwanja bubu vya ndege kma kile cha chato huoni mngeokoa hawa watanzania zaidi ya million 30 ambao kwa namna moja ama nyingine wanategemea kilimo kma source of income hasa wanaoishi vijijini???

Je hapo lawama haziendi kwa CCM kwa sera zao mbovu na vipaumbele vibovu???
 
wengu hawajua nini maana ya upinzani:
upinzani sio uadui
upinzani sio ugomvi
upinzani ni njia mbadala..
Watanzania ni wamoja..kuwachukia watu kwa kuwa wapinzani ni kufilisika..
 
Wale mnaoona upinzani uchwara kama ninyi ni watanzania kwa nini msianzishe huo upinzani imara?Kama ninyi mnaogopa tu hata kuanzisha vyama "imara" vya upinzani mnapataje nguvu ya kukosoa hawa wenzetu waliojitahidi hadi kuilazimisha CCM kucheza muziki isioupenda?

Kama ninyi mnaoukosoa upinzani mpo huko huko upinzani mf.akina Cheyo na Lipumba,ni wazi mmekuwepo huko miaka mingi,ni kwa nini hadi leo mmeshindwa kutekeleza mbachokifikiria hadi mkakubalika?

Kama mnaokosoa hivi mko CCM, kwa nini msipendekeze vyama hivi vifutwe au muwe wakweli tu kuwa mlivianzisha ili kudanganyia wakubwa wa dunia ili kila mtu ajue aweze kuwa kama Mzee Cheyo na Mrema?Si muwaambie ukweli akina Lissu ili wasikomae kupita kiasi hadi kuwa target ya wauaji wasiojulikana?

Mnaosema hivi, je mnaamini kwamba kuna watu wamezaliwa kuwa wapinzani tu na wengine watawala tu?Kama mnadhani hivyo basi hiyo ni imani potofu na inashiria tatizo kubwa zaidi zaidi la kifikra kuliko kuwepo upinzani uchwara wenyewe
 
Nani aliwaambia kuna upinzani TZ?mbona mnakuwa wagumu sana kuelewa kuwa mnachezewa picha?
 
Back
Top Bottom