Tanzania na Uganda zaanza mchakato wa ujenzi wa bomba la Mafuta

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Tanzania na Uganda zimeanza mchakato wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka katika nchi ya Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kugharimu dola za Kimarekani bilioni nne.

Makubaliano ya kujengwa kwa mradi huo yalifikiwa na marais wa nchi hizo Dr,John Magufuli wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda walipokutana jijini Arusha wakati wa kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mawaziri wa sekta zinazohusiana na nishati,makatibu wakuu na watendaji wa ngazi mbalimbali wa nchi za Tanzania na Uganda wamekutana jijini Arusha na kusaini makubaliano ya kuanza kwa mchakato ambao waziri wa nishati wa Uganda Bi.Irine Liuloni amesema mradi huo utaongeza chachu ya uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki .

Aidha viongozi hao wamesema kitakachofuata baada ya hatua hiyo ni taratibu za ndani za serikali za Tanzania na Uganda na kwamba mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya kimataifa ya uchimbaji wa mafuta ya total unatarajiwa kuanza mapema mwanzoni mwa mwaka 2017.

Kama mradi huo utakamilika na kuanza uzalishaji unatarajiwa kuongeza fursa za kiuchumi na ajira kwa wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Chanzo: ITV
 
Guuuud mchakato uende faster tuanze kuinjoy mapema matunda ya kuwa na Rais kama Magufuli.
 
Uganda wajanja sana waliona Kenya wanamafuta hivo mteja wao wa karibu wa kuwahiwa ni tanzania
 
Wewe hauna Akili hata kinachopangwa kujengwa ni nini na kwani kinapangwa kujengwa haujui, ni bora uulize kwanza ili uasidiwe klk kuandika mambo ambyo hata mtoto wa darasa la nne hawezi kuandika kama ulivyoandika!
 
Mbona umekuwa mkali badala ya kumuelewesha kuwa sio kwamba Uganda wanatuuzia mafuta bali wanatumia ardhi yetu kusafirishia mafuta yao kwenda nje na mafuta hayo ni ghafi,tunachofaidika sisi ni kuongezeka kwa Foreign Direct Investment ,Tozo la kodi ,pamoja na ajira kwetu sisi.hata hivyo iwapo itajengwa refinery plant itatusaidia pia kutokuagiza mafuta kutoka nje badala yake tutanunua mafuta kutoka kwa hawa jirani zetu,so inawezekana pia yupo sahihi.
 
Tanzania na Uganda zimeanza mchakato wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka katika nchi ya Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kugharimu dola za Kimarekani bilioni nne.

Makubaliano ya kujengwa kwa mradi huo yalifikiwa na marais wa nchi hizo Dr,John Magufuli wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda walipokutana jijini Arusha wakati wa kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mawaziri wa sekta zinazohusiana na nishati,makatibu wakuu na watendaji wa ngazi mbalimbali wa nchi za Tanzania na Uganda wamekutana jijini Arusha na kusaini makubaliano ya kuanza kwa mchakato ambao waziri wa nishati wa Uganda Bi.Irine Liuloni amesema mradi huo utaongeza chachu ya uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki .

Aidha viongozi hao wamesema kitakachofuata baada ya hatua hiyo ni taratibu za ndani za serikali za Tanzania na Uganda na kwamba mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya kimataifa ya uchimbaji wa mafuta ya total unatarajiwa kuanza mapema mwanzoni mwa mwaka 2017.

Kama mradi huo utakamilika na kuanza uzalishaji unatarajiwa kuongeza fursa za kiuchumi na ajira kwa wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Chanzo: ITV
Uganda wajanja sana waliona Kenya wanamafuta hivo mteja wao wa karibu wa kuwahiwa ni tanzania
Mbona Tanzania inatarajia kupata mafuta yake...kutoka bonde la Kilombero
images

Swala: Hopes of oil find in Kilombero Basin high
 
Tanzania na Uganda zimeanza mchakato wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka katika nchi ya Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kugharimu dola za Kimarekani bilioni nne.

Makubaliano ya kujengwa kwa mradi huo yalifikiwa na marais wa nchi hizo Dr,John Magufuli wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda walipokutana jijini Arusha wakati wa kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mawaziri wa sekta zinazohusiana na nishati,makatibu wakuu na watendaji wa ngazi mbalimbali wa nchi za Tanzania na Uganda wamekutana jijini Arusha na kusaini makubaliano ya kuanza kwa mchakato ambao waziri wa nishati wa Uganda Bi.Irine Liuloni amesema mradi huo utaongeza chachu ya uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki .

Aidha viongozi hao wamesema kitakachofuata baada ya hatua hiyo ni taratibu za ndani za serikali za Tanzania na Uganda na kwamba mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya kimataifa ya uchimbaji wa mafuta ya total unatarajiwa kuanza mapema mwanzoni mwa mwaka 2017.

Kama mradi huo utakamilika na kuanza uzalishaji unatarajiwa kuongeza fursa za kiuchumi na ajira kwa wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Chanzo: ITV

Rudi hapa December 2016, unaweza kuwa na hoja tófauti.
 
Huko Kilombero hata kama hayo mafuta yapo hizo 540 million barells wanazozisema ni kidogo sana kwenye biashara ya mafuta.
Itazame vizuri taarifa..
''an independent petroleum advisory firm — has completed the review of the resource potential of the basin, located within the Kilosa-Kilombero licence and discovered that potential of oil in two horizons: Kito Basal Sandstone and Kito Sequence 1 Sandstone''
Hii ni sehemu tu ya license.
Tanzania%20overview.png
 
Mbona umekuwa mkali badala ya kumuelewesha kuwa sio kwamba Uganda wanatuuzia mafuta bali wanatumia ardhi yetu kusafirishia mafuta yao kwenda nje na mafuta hayo ni ghafi,tunachofaidika sisi ni kuongezeka kwa Foreign Direct Investment ,Tozo la kodi ,pamoja na ajira kwetu sisi.hata hivyo iwapo itajengwa refinery plant itatusaidia pia kutokuagiza mafuta kutoka nje badala yake tutanunua mafuta kutoka kwa hawa jirani zetu,so inawezekana pia yupo sahihi.
uyo hanaga busara jamaaaa,....mtu wa kelele nyingi then no points
 
Back
Top Bottom