Tanzania na serikali inayoyeyuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania na serikali inayoyeyuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'ong'onsela, Feb 4, 2012.

 1. N

  Ng'ong'onsela New Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ndo Tanzania yetu jamani,sina hakika kama viongozi wazuri na wenye nia njema na nchi wamekwisha mpaka hawa waliopo wandelee kutesa kiasi hiki.Wamekua na dharau kwa sababu bado wanaendelea kuongoza kwa mazoea kwani kila mtu anaweza kuthibitisha,hivi wakati watu wanakufa kwa sababu ya mgomo wa madaktari mkuu wa nchi alikua amekwenda wapi? kipi kilikua bora kwake pamoja na serikari yake kushughulikia maisha kwanza ya watanzani au kwenda kwenye huo mkutano? hii ni dharau ya moja kwa moja kutoka kwa rais wetu.
  Pili tazama majibu ya waziri mkuu kwa madaktari pamoja na ya katibu mkuu wa wizara ya afya..jamani hawa bado wanaongoza nchi kwa mazoea wanasahau kua hatma yao ipo mikononi mwetu hii ni lazima tuwajibishe jamani.
  Haya naomba niingie kwenye mada yangu ,ikiwa tunakumbuka vizuri sakata la Jairo na nia njema ambayo waziri mkuu aliionesha bungeni na mbele ya wananchi kuhusu uamuzi ambao angeuchukua bila hata kusita ni kumfukuza mara moja,kwakua madaraka yako kwa rais aliahidi kumfikishia taarifa rais ili achukue hatua dhidi ya Jairo lakini tukumbuke kauli ya waziri mkuu ndio ilikua kauli ya serikali rais tulikua tunamsubiri tu kuadhimia hilo mara moja...
  Cha ajabu rais hakufanya hivyo mara moja..alifanya baada ya kuona watu wanalisemea sana..Haya sasa hili la juzi kuhusu posho WAZIRI MKUU ALISEMA RAIS AMEKUBALI LAKINI BAADAYE TAARIFA IKATOKA IKULU KUA RAIS HAJAIDHINISHA HILO!
  KAMA HAWA VIONGOZI WAMESHINDWA KUONGOZANA WAO WAWILI WATAWEZAJE KUTUONGOZA WANANCHI WOTE?

   
 2. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Tatizo lililopo ni kwamba maamuzi mengi hivi sasa miongoni mwa viongozi wetu ni ya kisiasa zaidi kuliko ya kimantiki.
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
   
Loading...