Tanzania na Sera za Vyama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania na Sera za Vyama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by cabhatica, Oct 6, 2010.

 1. cabhatica

  cabhatica JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 1,074
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, kila chama cha siasa kinaparamia jukwaa kunadi sera za chama husika.[/FONT]

  [FONT=&quot]Huwa napata shida nikifikiria tutakapofika mahali kama uingereza au marekani ambapo kila baada ya kipindi kifupi nchi inakamatwa na chama tofauti.[/FONT]

  [FONT=&quot]Sera za vyama jinsi ambavyo hazishabihiani, itakuwa hivi kwa Tanzania: leo elimu na afya bure, kesho wananchi wachangie elimu na afya, kesho kutwa bure, mtondo kuchangia…. Leo tunajenga kiwanda cha silaha, kesho ujenzi haujakamilika unasitishwa na chama kingine. Leo magari ya serikali ni hardtop kesho mashangingi. Kesho kutwa hardtop. Leo tuna mikoa na wakuu wa mikoa, kesho majimbo na magavana, keshokutwa mikoa…. Leo tuna wizara ishirini, kesho wizara kumi, keshokutwa wizara thelathini…. Leo kipaumbele ni elimu, kabla hilo halijafanikiwa kesho kipaumbele ni kilimo, keshokutwa ni utalii hata kama kilimo hakijafanikiwa, mtondogoo ni uwekezaji, au nishati au maji nk…..Huu ni wendawazimu!!!!![/FONT]

  [FONT=&quot]Jambo ninalotaka wana-jamiiforum wachangie ni hili: Kwanini kama taifa tusiwe na SERA ZA TAIFA halafu kila chama cha siasa kikaratibu mikakati yake ya kutekeleza sera hizo badala ya kila chama kuwa na sera zake? [/FONT]

  [FONT=&quot]Hili litatufanya watanzania kuwa na malengo ya pamoja (common goals) na hivyo kuwafanya wapiga kura kuweza kulinganisha mikakati ya vyama mbalimbali kuona ni ipi inatekelezeka ili kufikia malengo yetu kwa haraka na kwa urahisi zaidi hivyo kukipa ridhaa ya kuongoza…..?[/FONT]

  [FONT=&quot]Naomba kutoa hoja![/FONT]
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  naunga mkono hoja yako, hayo yoote yangefanyika na chama tawala kama wangekubali kukosolewa na kuona upinzani ni ndugu badala ya kumwona kama ni adui mkubwa. Hapa tz haijawai tokea ndugu mpaka tuone kunamabadiliko badala ya kuiona ccm tuu na makamba wake! Yaani nasikitika ni kama chama chetu kimeuzwa na wengi wanaona kama chadema ndo mkombozi! ccm ya Nyerere ni tofauti saana na ccm ya leo hii. Unawanadi mafisadi kuwa ni watu safi si kuwa nawashutumu, hapana ila kesi zao zipo mahakamani haina haja ya kuwanadi kwa mbwembwe! Tamalize kwanza matabaka ya walionacho na wasionacho. ndipo tuyafanye hayo unayopendekeza. MUNGU IBARIKI TANZANIA!!
   
Loading...