Tanzania na matumizi ya Kiingereza

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,660
1,801
"Nimehazwa' kuandika kipande hiki kutokana na mjadala unaoendelea hivi sasa juu ya weledi wa rais Magufuli wa kuzungumza Kiingereza.

Kuna wale walioona alichokisema katika mkutano wa EAC ni aibu kubwa. Mimi ni mtetezi wa matumizi ya Kiswahili, ila pia natambua Kiingereza bado ni muhimu kwa Tanzania. Kwa sasa, ni muhimu viongozi wetu wajue vizuri lugha zote mbili hizo.

Kwa kweli katika hali ya kawaida kusingekuwa na sababu yeyote ya viongozi wetu kuona wana lazima ya kuzungumza Kiingereza. Ila kwa vile hatukufanya lolote kukikuza Kiswahili tangu tupate uhuru, ni kweli kuwa hadi sasa msomi wa kweli ni yule anayejua Kiingereza. Hadi sasa bado haiwezekani kusoma kwa Kiswahili tu na kuwa msomi. Ili tufikie daraja hili ingebidi tangu kupata uhuru tungeanzisha mkakati wa kweli wa kufasiri vitabu vyote muhimu vinavyotambulika duniani, ikiwa vya sayansi au literature kwenye lugha ya Kiswahili.

Hadi hapo siku tutakapoweza kusoma Illiad ya Homer, Great Expectations ya Charles Dickens, Virgin Soil ya Ivan Sergeyevich Turgenev....au hata Lolita cha Vladmir Nabokov, kwa Kiswahili......hapo ndipo Kiingereza hakitakuwa na maana, na mtu angekuwa msomi wa kweli kweli hata kama hajui neno moja la Kiingereza au lugha nyingine.

Kwa hivi sasa kwa kweli mtu kutojua Kiingereza kunaleta maswali mengi juu ya taaluma yake. Hata kama tukisema kutokujua kuzungumza lugha hakumaanishi kutokuwa msomi. Hilo si kwa nchi kama Tanzania.

Hilo linaweza kuwa kweli kwa nchi kama za Kiarabu, Iran, Korea nk. Kwa sababu hawa tayari wana hazina kubwa ya vitabu vilivyofasiriwa katika lugha zao kiasi mtu anaweza kusomea udaktari mpaka akawa mpasua moyo, kwa Kiarabu tu. Iran nilikutana na wanasayansi wanaotengeneza safina ya kwenda anga za nje, na wengi walikuwa hawajui neno moja la lugha ya Kigeni.
Wenzetu hawa walitambua kabisa tangu mwanzo kwamba bila ya ku-'izalendosha' elimu haitawezekana kupata wataalamu wa kufikiria mambo mapya.

Kwa mfano Waarabu kuanzia miaka ya hamsini wamekuwa na kituo kikubwa Misri cha kufasiri vitabu kutoka lugha zote za taaluma: Kiingereza, Kirusi, Kifaransa, Kihispaniola nk kwenda kwenye Kiarabu. Juhudi zao zilileta tija kuanzia miaka ya sabini wakati nchi nyingi za Kiarabu zilipoanza kutumia mtaala wa Kiarabu kitupu.

Kazi hii ya kufasiri vitabu ilitakiwa tuianze tangu wakati tulipopata uhuru. Hii ni kazi inayochukua karne nzima ndiyo tija iwe imeiva. Kwa bahati nzuri hata miaka 50 tangu kuanza kazi hiyo matokeo yanaweza kuonekana, kama kwa Waarabu na Waajemi; ambao bado wana miaka mingine 30-40 hivi ya ku- catch up.

Ila sisi kila kukicha ni kusema tu na kupiga domo. Hata Nyerere ambaye alikuwa na nia nzuri, ila hakuwa na ufahamu kuwa ili ku-zalendosha mtaala inabidi kwa kweli kuwa na serious government mkakati wa kufasiri vitabu, tena mkakati wa muda mrefu.

haiwezekani ufanye 'ilani' tu na kesho iwe!
Ukisoma maendeleo ya Ulaya hadi kufikia 'industrial revolution' mnamo karne ya 17, utaona kuanzia mwaka 1444 ambapo Johannes Gutenberg alipovumbua mashine ya kwanza ya kuchapisha vitabu, waliongeza kasi ya kufasiri vitabu vya Kiyunani na Kiarabu na kuvitia kwenye lugha zao. Hii ndiyo iliyopelekea Wazungu kuendelea na hatimaye kuyashinda mataifa yote kielimu. Tunajifnza nini katika hili? Kwamba ugurishaji wa taaluma na maarifa hautatimia ila kwanza kwa kufanya kazi kubwa ya kufasiri vitabu katika lugha yenu. Kuna tafiti nyingi zimefanywa na kugundua ili akili iweze kuvumbua ni lazima i process information katika lugha yake ambayo ndiyo anayoizungumza kwa muda mrefu wa maisha yake na ndiyo anayoitumia katika kufikiria na katika ndoto.

Kwa sababu elimu siyo shule. Elimu ni ile unayoishi nayo wakati wowote ule. Kazi ya shule ni kuelekeza tu mfumo wa kufikiria. Vinginevyo tutakuwa na 'wasomi' wa kurudiarudia tu yale yanayovumbuliwa na wengine, mithili ya kasuku.
 
Hivi kiingereza kina makosa gani? Au kiingereza kimewakosea nini watanzania? Mbona inaonekana kinabezwa sana kanakwamba ni lugha isiyotakikana miongoni mwetu???

Sera ya lugha inasema kiswahili ni lugha ya taifa, lugha ya taifa ni lugha inayotakiwa kutumika katika matumizi yote ya kila siku ya shughuli za serikali na zile za wananchi binafsi, ni lugha halali ya kuwasiliana baina ya watu wa kutoka makabila mbalimbali na kuwaunganisha watu. Hata hivyo kwa mujibu wa sera ya lugha ya Tanzania Kiingereza na kiswahili ni lugha rasmi. Maana ya lugha rasmi ni lugha inayotakiwa kutumika kwenye maofisi na shughuli rasmi za kiserikali. Kwa maana hiyo katika shughuli rasmi za kiserikali na maofisini lugha zinazotakiwa kutumika ni mbili ama kiswahili au kiingereza na ndiyo maana unapoomba kazi maofisini huwa interview hufanyika kwa kiingereza hii ni kwa sababu ni muhimu kwa mfanyakazi kujua lugha hizi mbili ambazo ndizo lugha rasmi, kiswahili wengi wanakijua lakini kiingereza imeonekana ni tatizo sana!!!

Kwa maoni yangu kujifunza kiingereza siyo kuutukuza uingereza bali ni jambo la muhimu kwa mtumishi na kiongozi wa umma!!! Tuache mawazo potofu kwa mfano mfanyakazi wa benki asipojua kiingereza akaja mteja asiyejua kiswahili ana mhudumiaje? Mahakamani hasa mahakama ya hakimu mkazi, wilaya, mahakama kuu lugha zinazotumika ni kiswahili na kiingereza. Mahakama ya Rufani lugha inayotumika ni kiingereza pekee. Kiujumla siyo sahihi kukibeza kiingereza kana kwamba hakina umuhimu na kama swala ni kuutukuza uingereza kwa kutumia kiingereza basi tumeanza kuutukuza kuanzia kwenye sera yetu ya lugha kwa kukifanya kuwa sehemu ya lugha rasmi! Kwanini haikuwa kichina? Au kifaransa?. Kiingereza ni lugha rasmi hapa nchini!!!

Kiingereza kimetufaa na kinaendelea kutufaa? Wawekezaji wanakuja Tanzania wanawasiliana nasi kwa kiingereza, viongozi wetu wanaenda nje wanaongea hiyo lugha. Watanzania wengi wapo nje ya nchi wanafanya kazi kwa kutumia kiingereza! Leo hii kiingereza ni lugha ya kufundishia watoto wetu kuanzia sekondari hadi chuo kikuu! Hatuoni haya? Nani atainuka kukisemea kiingereza? Siyo kwa vile viongozi wetu fulani hawakijui ndiyo tusahau fadhila za lugha hii! Ni ajabu sasa kila mtu anajifanya mtetezi wa kiswahili wakati hata kiswahili chenyewe hatukijui vyema!

Siyo jambo la kushabikia kuona kiongozi mkubwa hajui lugha hii huu ni mojawapo wa udhaifu kwa viongozi. Ushauri wangu wamtafute tu Rasi Simba wajifunze lugha ni juhudi zako tu na mazoezi yako!

Tukienzi kiswahili lakini tusisahau umuhimu wa kiingereza.

Siku njema!
 
Hii ndo nchi pekee ambayo kwenye milango ya shule za kata yamebandikwa mabango "NO ENGLISH NO SERVICE" wakati huo huo kwenye ofisini ya kule kuelekea kivukoni pamewekwa bango "WITH ENGLISH NO SERVICE".
 
Sioni kama kuna umuhimu wowote wa Mtanzania kuongea English,Kama Watanzania wangelijua umuhimu wa kiswahili wangelikitikuza sana,sema bahati mbaya watanzania ni majuha bado wanataka kutegemea Lugha za watu wakati lugha kiswahili inadhaminiwa dunia nzima...
 
Juzi wakati nimeweka topic ya Rais wa Vietnam kutumia lugha yake ya nyumbani kuhutubia 'ugenini' kuna mdau mmoja humu simkumbuki vizuri lakini alitoa hoja ya msingi sana ambayo na wewe mleta mada umeigusia.

Kwamba wale wanaozungumza lugha zao hata wanaposafiri nje ni wale ambao wamesoma masomo yao yote kuanzia 'vidudu' hadi huko juu.Nadhani kila mtu anapata jibu hapo na tunaweza kufunga mjadala huu
 
Mkuu umeongea la maana sana. Nakubaliana nawe kwa asilimia 100!!

Kinachoendelea sasa inaonyesha mfumo mbaya wa elimu yetu. Wapiga kelele wengi humu ni waathirika wa huu mfumo ... haiwezekani kwenye mfumo mzuri wa elimu kijana akasoma lugha kuanzia darasa la 3 mpaka chuo kikuu halafu ashindwe kuimudu sawasawa. Mbona Kenya wanatumia Kiswahili lakini hawana tatizo kama letu ukija kwenye lugha ya Kingereza!!? Kuna watu watadai Wakenya hawaongei Kiswahili kama sisi ......... hiyo siyo kweli. Ukiwa nje ya nchi ukikuta Wakenya wako pamoja au kwenye bar utakuta muda mwingi wanatumia Kiswahili tu. Angalia hata kwenye team zao utakuta wakiwawanapeana maelekezo wao kwa wao yanafanywa kwa Kiswahili. Ukienda Zimbabwe, Botswana au Malawi huwezi ukawakuta wanatumia Kingereza wakiwa wao kwa wao ......... wanatumia lugha zao kama sisi tunavyotumia Kiswahili lakini Kingereza cho kiko juu kuliko sisi!!

Inawaezekana kabisa kujifunza lugha zaidi ya moja shuleni na zote ukazimaster vizuri tu. Angalia watu waliosomea elimu zao za juu kama Urusi, China au Germany, kwa nini huwa wanajifunza hizo lugha kwa muda mfupi na kuweza kuzitumia sawasawa sometime kuliko hata Kingereza walichojifunza kwa zaidi ya miaka 10!!?

Nafikiri ni muda tu tukubali kuwa kupata walimu wa Kingereza nje watusaidie ...... wenyewe hatujitoshelezi!!
 
Sioni kama kuna umuhimu wowote wa Mtanzania kuongea English,Kama Watanzania wangelijua umuhimu wa kiswahili wangelikitikuza sana,sema bahati mbaya watanzania ni majuha bado wanataka kutegemea Lugha za watu wakati lugha kiswahili inadhaminiwa dunia nzima...

Nafikiri hoja ya msingi kwa sasa ni kwa nini sisi tunashindwa kuimaster lugha inayotumika kutufundishia kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu!? Kama serikali ingekuwa imechagua Kiswahili kama lugha pekee ya Taifa na kila kitu kikafundishwa kwa Kiswahili nafikiri tusingekuwa na issue ya kujadili leo. Tatizo serikali imekosea hapo na bado pia imefail kwenye Kingereza walichokichagua. Ethiopia wanatumia lugha yao .......... naona matunda ya nini wanafanya taratibu yanaanza kuonekana!!

Kwa hiyo unaposema huoni umuhimu wa Mtanzania kuongea English ungekuwa uko sawa kama tungechagua Kiswahili over English!! Kwa vile tumechagua lugha mbili basi ni lazima tuhakikishe tunazimudu sawasawa ..... vinginevyo tutakuwa tunafail kama Taifa!!

Ka sasa Kingereza kinapewa nafasi kubwa sana katika serikali na taasisi zote ....... ndiyo maana kila mtu anajitahidi kumsomesha mtoto wake kwenye English meadium schools!!

Sidhani kama kuna mtu anadai kuwa Kingereza ni superior kwa Kiswahili bali ni kwa nini sisi tunashindwa kukimudu Kingereza wakati ndiyo lugha tunaoitumia kushishiwa na kupata kazi serikalini!!?
 
Mr. Zero,

..watu wamejenga chuki na kiingereza kwasababu hawakijui au kimewashinda.

..wanaochukia kiingereza wananikumbusha waliokuwa wanachuki somo la HISABATI wakati niko shuleni.

..mwanafunzi anapokuwa halimudu somo Fulani Mara nyingi hujenga chuki na somo hilo. Hiyo yote ni hali ya kukata tamaa.

..kuna umuhimu mkubwa kwa taifa kuwekeza ktk kupata waalimu wazuri wa kiingereza ili vijana wetu waimudu lugha hii.
 
Mkuu umeongea la maana sana. Nakubaliana nawe kwa asilimia 100!!

Kinachoendelea sasa inaonyesha mfumo mbaya wa elimu yetu. Wapiga kelele wengi humu ni waathirika wa huu mfumo ... haiwezekani kwenye mfumo mzuri wa elimu kijana akasoma lugha kuanzia darasa la 3 mpaka chuo kikuu halafu ashindwe kuimudu sawasawa. Mbona Kenya wanatumia Kiswahili lakini hawana tatizo kama letu ukija kwenye lugha ya Kingereza!!? Kuna watu watadai Wakenya hawaongei Kiswahili kama sisi ......... hiyo siyo kweli. Ukiwa nje ya nchi ukikuta Wakenya wako pamoja au kwenye bar utakuta muda mwingi wanatumia Kiswahili tu. Angalia hata kwenye team zao utakuta wakiwawanapeana maelekezo wao kwa wao yanafanywa kwa Kiswahili. Ukienda Zimbabwe, Botswana au Malawi huwezi ukawakuta wanatumia Kingereza wakiwa wao kwa wao ......... wanatumia lugha zao kama sisi tunavyotumia Kiswahili lakini Kingereza cho kiko juu kuliko sisi!!

Inawaezekana kabisa kujifunza lugha zaidi ya moja shuleni na zote ukazimaster vizuri tu. Angalia watu waliosomea elimu zao za juu kama Urusi, China au Germany, kwa nini huwa wanajifunza hizo lugha kwa muda mfupi na kuweza kuzitumia sawasawa sometime kuliko hata Kingereza walichojifunza kwa zaidi ya miaka 10!!?

Nafikiri ni muda tu tukubali kuwa kupata walimu wa Kingereza nje watusaidie ...... wenyewe hatujitoshelezi!!

Mimi mjadala wa lugha ya kiingereza huwa siupendi hata kidogo. Badala ya kuzungumza tatizo watu wanaanza kuchekana eti huyu hajui kuzungumza kiingereza sijui nini, yaani watanzania kwa kweli wana inferiority complex kubwa sana kuhusu kiingereza. You know what, watanzania wengi wanaamini kuwa mtu mwenye elimu ni yule anayezungumza kiingereza na kwamba eti ni aibu kwa kiongozi kutojua lugha hii. Mimi nimeona vijana wengi wakiwemo pia watu wazima wanaona aibu kuzungumza kiingereza...akizungumza broken English yaani utaona mtu amesinyaa kwa aibu na hofu ya kuchekwa. Ninavyoelewa mimi kiingereza ni lugha kama ilivyo kwa lugha nyingine ingawa kwa hakika ni vizuri mtu kujifunza kiingereza kwani ni lugha ya kimataifa na ni kwa business .
Yaani kwangu kiingereza ni sawa na Kipare, mimi nikiongea Kipare ambacho ni broken kwanini nichekwe wakati siyo lugha yangu? Hii Kasumba ya watanzania kuhusu kiingereza ndiyo iliyowafanya wakati Fulani watu wengi nchini mwetu kuwapeleka watoto wao kusoma huko Uganda na Kenya. Yaani wakiwa Kenya watoto wengi walikuwa wanajua kuongea kiingereza lakini knowledge yao in general kwa masomo mengi ilikuwa duni kabisa.

Of course watu wa zamani waliopiga umande wanajua vizuri kuongea na kuandika kiingereza. Hii inatokana na namna shule zilivyokuwa zimeandaliwa. Mimi nakumbuka wakati wangu kiingereza tulikuwa tunaanza kujifunza kuanzia darasa la tatu na ikifika darasa la tano masomo yote yalikuwa ni kwa kiingereza. Kulikuwa na mashindano ya insha za kiingereza na debates. nakumbuka topic maarufu za debates wakati ule kama 'village life is better than town life', 'a day school is better than a boarding school'. Basi vijana, wavulana kwa wasichana, walikuwa wanajimwaga kushiriki debates hizo.

Mimi nakumbuka siku moja au mbili kabla ya debate tulikuwa tunazama kwenye dictionary kutafuta maneno magumu ya kiingereza wenyewe tukiita 'mabombastic' ili tuje tuwakoge wenzetu wakati wa debate.

Halafu kulikuwa na vitabu vingi vya hadithi na hata Radio Tanzania (au TBC) wakati huo ilikuwa na kipindi cha kiingereza saa tatu au saa nne asubuhi. Basi tunakusanyika kwenye darasa na kiredio cha shule cha mbao kikiwa mbele kusikiliza 'series za thousand miles to Tanga' na kadhalika.

Haya basi, mtu ukichaguliwa kwenda sekondari (na wakati huo shule zinatoa mtu mmoja au wawili sana sana wanne na ile inayotoa wanafunzi wanane ilikuwa ni kiboko) mwezi mmoja kabla ya shule za sekondari hazijafunguliwa nyie wa form one mnawahishwa mwezi mmoja na kazi yenu ni moja tu kusoma kiingereza kuanzia asubuhi mpaka usiku. Yaani nyie kazi yenu ni moja tu kusoma kiingereza kila kitu kuhusu English na vitabu vya hadhithi vya English. Nakumbuka mimi wakati wangu kwa mwezi huo mmoja nilisoma vitabu vya hadithi vya kiingereza vitapavyo 70 hivi mpaka mwalimu akanipa zawadi ya kitabu. Yaani vitabu vya hadithi in English vilikuwa vimejaa library kubwa ya shule na kila stream ya form one ilikuwa na library yake ndogo. Kwa hiyo mtu unaazima kitabu ukimaliza unarudisha na kupata kingine. Vitabu vya hadithi fupi na hadithi ndefu kama 'King Solomon mines' na kadhalika.

Halafu, shule za sekondari nazo zilikuwa na mashindano yake ya debates, basi nakwambia hapo ilikuwa ni shida...Mimi nikiwa form one tulikuwa tunawasikiliza watemi wa Form SIX wanamwaga English mtu unashangaa.

Sasa basi na sisi enzi zetu kuwaonyesha watu kuwa tunajua English tunabeba novel zetu zile za James Hadley Chase kama 'This is for Real', ' A Coffin From Hong Kong'; 'Why pick on me?' na kadhalika...kulikuwa pia na novel za waandishi wengine kama 'The Guns of Navarone', 'The Day of the Jackal' ya Frederick Forsith bila kusahau novel ambayo ilikuwa ni best seller na ambayo mpaka sasa ninayo ingawa imechakaa ya 'The Godfather' ya Mario Puzzo '. Yaani kizazi cha wakati ule kilikuwa ni cha kusoma.

Ila sasa mambo yamebadilika, hiki ni kizazi cha digitali yaani Dot.Com yaani ni shida kazi yao ni mambo ya kompyuta, smart phone na kadhalika. Yaani hata message zinavyotumwa via smart phone ni shida yaani utapata taabu kusoma message zao sijui wanatumia lugha gani mara wamechanganya namba na maneno. Yaani vijana wa siku hizi ni smart hata kama hana smart phone yaani kwao ku-operate siyo shida. Vijana wa leo wana uzuri wao, kwa hakika.

Tatizo la kiingereza liko wapi na limeanzia wapi ni mjadala mzito. namna gani turejeshe standard nzuri ya English nao ni mjadala mzito.
 
Nafikiri hoja ya msingi kwa sasa ni kwa nini sisi tunashindwa kuimaster lugha inayotumika kutufundishia kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu!? Kama serikali ingekuwa imechagua Kiswahili kama lugha pekee ya Taifa na kila kitu kikafundishwa kwa Kiswahili nafikiri tusingekuwa na issue ya kujadili leo. Tatizo serikali imekosea hapo na bado pia imefail kwenye Kingereza walichokichagua. Ethiopia wanatumia lugha yao .......... naona matunda ya nini wanafanya taratibu yanaanza kuonekana!!

Kwa hiyo unaposema huoni umuhimu wa Mtanzania kuongea English ungekuwa uko sawa kama tungechagua Kiswahili over English!! Kwa vile tumechagua lugha mbili basi ni lazima tuhakikishe tunazimudu sawasawa ..... vinginevyo tutakuwa tunafail kama Taifa!!

Bado sioni umuhimu wa lugha ya kiingeza katika jamii ya kitanzania,Kingereza ni sawa na lugha yoyote ile duniani,Wajurumani hawaongei kingereza,wafaransa hawaongei kingereza.....nk

Ka sasa Kingereza kinapewa nafasi kubwa sana katika serikali na taasisi zote ....... ndiyo maana kila mtu anajitahidi kumsomesha mtoto wake kwenye English meadium schools!!

Sidhani kama kuna mtu anadai kuwa Kingereza ni superior kwa Kiswahili bali ni kwa nini sisi tunashindwa kukimudu Kingereza wakati ndiyo lugha tunaoitumia kushishiwa na kupata kazi serikalini!!?

Kaka uko sawa,Kama Ethiopia imechagua kusomesha raia wake kwa lugha yao,basi ujue Waithiopia sio majuha kama watanzania,Amharic lugha Taifa la Ethiopia,nani anazungumza lugha ya Amharic?,,Ni waithipia tu wanaozungumza hiyo lugha,Nani anazungumza kiswahili?nchi ngapi za Afrika zinazunguza kiswahili?Je kiswahili kinajulikana vipi kimataifa..

Kiswahili ni lugha kubwa inayojulikana Dunia nzima,lugha inayosomeswa katika vyuo vikuuu duniani kote,kuna vipindi vya watoto katika nchi fulani za ulaya vinafundisha watoto kiswahili

Kwa ufupi watanzania wamebarikiwa kuwa na hii lugha lakini, watanzania bado hawajajua umuhimu wa lugha ya kiswahili,waswahili wanasema "kwenye miti hakuna wajenzi",bado tunang'ang'ania lugha za kigeni,watanzania wanaona wakizungumza kingereza wanajiona wako juu,ujuha!!!

Nchi zote zilizoendele duniani zinawasomesha raia wao kwa lugha zao za "local language",sio lugha za kigeni,tafiti zinaonyesha watoto wanakuwa wanafahamu somo analosomshwa kirahisi kama atafundishwa kwa lugha yake aliozalowa nayo...
 
Sioni kama kuna umuhimu wowote wa Mtanzania kuongea English,Kama Watanzania wangelijua umuhimu wa kiswahili wangelikitikuza sana,sema bahati mbaya watanzania ni majuha bado wanataka kutegemea Lugha za watu wakati lugha kiswahili inadhaminiwa dunia nzima...
Mkuu majuha ukiwemo na wewe?
 
Mkuu majuha ukiwemo na wewe?
Kama ningekuwa juha kama wewe singeliandika niliyoandika,,nani kakwambia kama mimi mtanzania....Nashangaa bado mnang'anga'ania lugha za watu wakati yenu mnayo,mnaona mkiongea kingereza ndio mko juu.Kingereza ni lugha kam lugha nyeninge yoyote ile.

Kwa taarifa yako China hawaongei kingereza na wamepiga hatua kimaendeleo,Wafanransa ndio hivyo hivyo,kwa ufupi nchi zote zilizoemdelea zinafunza raia wake kwa Lugha yao,,,,Angalia Ethiopia inavyopiga hatua.....,Juha mkubwa wewe
 
So Tanzania nayo ndiyo China?
 
So Tanzania nayo ndiyo China?

Nilidhani katika mjadala huu wangeshiriki watu serious, wenye maono, elimu na weledi na pengine 'exposure'......Ah, lakini Tanzania ni Tanzania. Mjadala kama huu watu wanakuja na mawazo ya akili za samaki.
Suala la lugha, kama tusipolitatua hivi sasa, bye bye maendeleo ya kweli. Nimesema, sijaona nchi iliyoendelea kiviwanda na uvumbuzi iliyotumia lugha ya watu wengine. Na kama iko hiyo itakuwa 'exception' si rule. Hii si inaishiria wazi kuwa lazima tujitoe mhanga kwa vyovyote vile tufikie mahali tunaweza kutumia lugha yetu kwa masomo yote? Sijasema leo au kesho twaweza kufanya hivyo. Nilisema hii ni safari ndefu na nikasikitika kwamba kwa nini hatukuianza tangu tulipopata uhuru, saa hii tungekuwa half-way. Na wala sijasema tusijifunze lugha nyingine, na siyo Kiingereza tu. Watu wengi wako 'so obssessed' na Kiingereza kana kwamba ndiyo lugha pekee ya taaluma. Hawajui kama kuna Kifaransa- ambacho hadi karne ya 18 ndicho kilichokuwa kinaongoza duniani kama lugha ya elimu na ustaarabu. Pengine katika uhai wetu Ki-Mandarin (Kichina) kitakuwa ndicho kinachosomwa zaidi!
Sasa kitu gani cha kupinga hapo?
 
TUTUMIE KISWAHILI ILI TUKITANGAZE DUNIANI,.....
TUWE PROUD NA KISWAHILI
 
Laiti ningeweza kusema Tanzania itumie kiswahili kama inavyojinadi ni lugha ya Taifa .........ukifanya kazi na wajerumani hata kiingereza chako ulichojifunza hakitakusaidia wao wanaongea lugha yao basi na kila kitu wanachotumia na kutoka kwao.......vile hawaelewi kiingereza hata ungeongea kiswahili ingekuwa bora zaidi maana ungetangaza TZ
 
Watu wengi wako 'so obssessed' na Kiingereza kana kwamba ndiyo lugha pekee ya taaluma.
Unaona? Ili na wewe uonekane umo imekubidi utumie neno la Kiingereza...bahati mbaya ni kwamba umeonesha mapungufu yale yale tunayoyapigia kelele, hatuna neno obssessed katika hiyo lugha, neno sahihi ni obsessed. Hizo lugha zote ulizozitaja hakuna lililo na umuhimu duniani kama Kiingereza na zilishasalimu amri zamani sana . Sijali hebu zingatia sababu hizi;
  1. English is the world's Business & Finance Language
  2. English is the Unofficial Language of the Internet!
  3. English is the Language of Travel
  4. English is the original language of most Scientific Books & Literature
  5. English is the most versatile and sophisticated Language in the world.
  6. English is the dominant language of movie industry...Hollywood blockbusters!
  7. English is the ladder to the Big Stage worldwide – One's Gotta Sing in English!
 
Back
Top Bottom