Hakuna namna yoyote ya kupata maendeleo bila kuwa na uongozi bora! nasema hivi nikiwa sina maana ya kwamba uongozi uliopo si bora! Lakini mwaka na miaka ambayo tutapata kiongozi amabaye atatusaidia kuyafanya haya;
1. kuimarisha mifumo yetu ya kiuongozi. yaani Serikali, mahakama na bunge kila muhimiri uwe na mipaka yake na uwe na uwezo wa kuidai hata pale inapo onekana kuingiliwa!
2. Kuwepo na mipango/ marengo ya miaka mingi ya taifa. ambayo hakuna raisi wala kiongozi yeyote atakaye weza kuyabadiri na hili litajwe na liwe wazi kwenye katiba. na mihimili yote ya serikali ifanye kazi ya kuyalinda malengo hayo yatekelezeke. mfano kwa kutokuwepo kwa malengo ya pamoja kama taifa anaweza akaja raisi mwingine 2020 akaanza kazi yake kwa kuuza ndege zote hizo mpya akijiegemeza kwenye sababu ya ndege hizo kuingiza hasara! angalia yaliyotokea kwenye mchakato wa katiba; taifa lilitumia pesa nyingi kuandaa rasmu, ikajadiliwa na bunge kwa pesa nyingi lakini kwasababu wazo hilo halikulindwa na katiba kwa kuwekewa kinga ya kutokubadilishwa sasahivi mchakato umesimama kama siyo kuisha kabisa. Kulikuwa na ujenzi wa bandari bagamoyo sasa hivi sijui!!! kama maendeleo tukiyataka kwa kila kiongozi anayeingia kuanzisha mambo yake mwenyewe ukweli nitasubiri sana!
Angalieni namna elimu yetu ilivyo kwenye umajaribio kwa wakati huu! anaingia huyu anapanga yake, mara anakuja mwingine anaweka yake pia
Angalieni kwenye kilimo. slogan zime kuwa nyingi hata haieleweki tunakwenda wapi!
kwenye biashara the same!
3. kuwepo na utashi wa dhati wa kuwasaidia wananchi na nchi kwa ujumla! Najrlibu kujiuliza mara nyingi haya malekebisho yanayofanywa kwenye katiba yetu yana lengo la dhati la kumsaidia mwananchi? Binafsi naona siyo kweli! kuna mapungufu mengi kwenye katiba ambayo kwa hakika yanahitaji marekebisho, hasa nikijiegemeza kwenye msemo wa 'msema kweli ni mpenzi wa Mungu aliye hai'
A. Ukweli rais kuhusika kwa namna yoyote kuweka viongozi wa mhimiri mwingine kama mahakama, kunaifanya mahakama kutokuwa huru hili kwa kiongozi mwenye hofu ya Mungu linatakiwa kufanyiwa marekebisho.
B. Ukweli rais kuwa kiongozi ama mwenyekiti wa chama fulani, siyo sawa! kunakuwa na mwingiliano usio wa lazima wa shughuli za serikali za za chama. kwanini tusione sababu ya kumpunguzia rais mzigo huo usio wa lazima? na hili lipo ili kulinda uhai wa chama kimoja! kweli kabisa hili jambo siyo sawa!
C. Rais kuteua ama kuhusika kuweka viongozi wa Tume ya uchaguzi! Jamani hili jambo siyo sawa! hakuna namna yoyote ambayo inaweza kuifanya tume hii iwe huru! JAMANI TUSEME UKWELI JUU YA HILI. Hili jambo hatakama miaka itaenda hatakama nitakufa kabra ya marekebisho ya jambo hili, nitakufa nikijua ya kuwa siyo sawa kabisa!
D. Hivi kweli kabisa wakurugenzi na wakuu wa mikoa ambao ni wateule wa raisi na mwenyekiti wa chama fulani cha siasa kuhusika kama wasimamizi wa uchaguzi ni sawa!!!
NB: yapo mengi yanayohitaji marekebisho lakini cha ajabu hakuna kiongozi mwenye utashi wa dhati wa kurekebisha. Maombi yangu, natamani Mungu atupe kiongozi ambaye atasimama kwa dhati kabisa aone sababu ya kutenda haki, hatakama akiongoza kwa miaka 2 tu! awake mambo sawa vinyongo, na uonevu vitakuwa vimeisha ndani ya nchi yetu!
Machache yangu ni hayo.