Tanzania na Maendeleo: Muelekeo Mpya na JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania na Maendeleo: Muelekeo Mpya na JK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by CAIN, Oct 18, 2010.

 1. C

  CAIN Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza napenda kumpongeza rais wetu Mh. J Kikwete kwa nia na dhamira yake ya kuifanya Tanzania kuwa na maendeleo ya kweli pamoja na kuiwezesha na kuendeleza amani iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwl. J Nyerere.
  Pili nimewiwa niandike mada hii kwa kuwa kipindi tulichonacho na muelekeo ni kwenda kwenye uchaguzi mkuu ambapo tutafanya maamuzi ya nani apewe dhamana ya kuiongoza nchi hii. Maamuzi tutakayofanya ndiyo yatakayofanya mustakabali wa nchi yetu uwe ama wa AMANI NA KULETA MAENDELEO au MACHAFUKO NA MVURUGANO.
  Ni kipindi muhimu sana kwa Taifa letu kwani kosa dogo tutakalofanya hapo Oktoba 31, laweza tugharimu kama sio miaka 5 basi mingine mingi ijayo. Ni vema wananchi wenzangu tukakipigia chama ambacho NIA na MALENGO yake ni kuendelea kuifanya Tanzania kuwa na AMANI na hivyo kufikia malengo ya Maendeleo.
  Nasema hivi kwa kuwa katika mchakato mzima wa kampeni unaoendelea hivi sasa nchini, kumekuwepo kwa sera za chuki na hasira zinazotolewa na baadhi ya vyama vya siasa eti kwa kuwa tu vinakichukia chama tawala CCM na kuona kama hakijafanya lolote kwa wananchi na Taifa la Tanzania. Hebu tupime ni mambo mangapi ambayo serikali ikiongozwa na CCM imeyafanya. Hivi leo mtu unasafiri kwa barabara tena ya lami toka Mtwara hadi Mwanza, wananchi wa Shinyanga waliokuwa na shida ya maji sasa wanafurahia huduma hiyo, hospitali nyingi zilizojengwa kila mahali nchini, idadi kubwa ya shule za msingi zilizojengwa chini ya serikali inayoongozwa na CCM, na mambo mengine mengi...
  Mipango zaidi, soma Tanzania - Projects & Programs

  Pia soma mipango ya kimaendeleo inayokamilika chini ya Tanroads hapa: Completed Projects

  Napenda kuwaasa wananchi wenzangu kujitokeza kwa wingi hiyo Oktoba 31 na kukipigia kura chama na mgombea ambaye kwa sera za chama chake, Tanzania itafikia malengo yake iliyojiwekea. Tusifanye majaribio ya kumpeleka mtu Ikulu ambaye hata uongozi mdogo wa kanisa ulimshinda sasa itakuwa kwa nchi???
  Kumbukeni Usia wa Baba wa taifa pale aliposema IKulu sio mahali pa Majaribio..


  Nawakilisha Oktoba 31
   

  Attached Files:

 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mtabadilisha ID's we lakini ukweli unabaki pale pale na mnafahamu hilo. Ndiyo maana kila kukicha hamuishi kuji-identify na new pen names just to try hoodwink members kwamba JK ana support na watanzania walio wengi.
   
 3. ZLATAN

  ZLATAN Senior Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Cain, umenifurahisha ndg yangu, hawa jamaa wagumu sana kuelewa, wao na slaa.......... Slaa na wao, tuendelea kuwaelimisha, nna imani ipo siku wataelewa, na si mbali ila ni oktoba 31.
   
Loading...