Tanzania na China zatiliana saini Mikataba 15

Tanzania na China zatiliana saini Mikataba 15

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,521
Ni matunda ya ziara ya Rais wa JMT mh Samia nchini China

Mikataba 15 yo ushirikiano imetiwa saini ikiwa ni pamoja na Tanzania kupewa mkopo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa Mikataba na Hati za Makubaliano ya kimkakati 15 akiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping.

Miongoni mwa mikataba hiyo iliyolenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji wa baina ya nchi hizo mbili umeshuhudia China ikiipunguzia Tanzania sehemu ya deni lake la thamani ya Shilingi Bilioni 31.4.

Miongoni mwa mikataba na makubaliano yaliotiwa saini ni kuhusu mahitaji ya kuwepo na soko kubwa la usafirishaji wa maparachichi kutoka Tanzania kwenda China.

Pia wametia saini Mkataba unaohusu msaada wa RMB milioni 100 za ushirikiano wa kiuchumi na kitaalamu baina ya nchi hizo mbili.

Vile vile, kumetiwa saini makubaliano kuhusu mahitaji ya kuwepo na soko kubwa la Usafirishaji wa Mabondo ya Samaki pamoja na bidhaa nyingine za uvuvi kutoka Tanzania kwenda China.

Aidha, China imetoa mkopo wa thamani ya dola za Kimarekani milioni 56.72 wenye masharti nafuu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar, Terminal II.

China inaongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania. Hadi kufikia Mwezi Oktoba 2022, Jumla ya miradi 1,098 yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 9.6ilisajiliwa katika kituo cha uwekezaji chaTIC.

Miradi hiyo imezalisha ajira 131,718. Uwekezaji huo umefanyika katika sekta za viwanda, kilimo, mawasiliano, madini na uvuvi.

Rais Samia yupo nchini China kwa ziara ya Kiserikali kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais wa nchi hiyo ambapo pia alikutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa China pamoja na Spika wa Bunge la nchi hiyo.

Chanzo: ITV habari
 
Wawalete kwenye miradi ya maji waache ujinga nchi kukosa maji wakati eneo lake Kama 25% ni maji tu
 
Mod unganisha huu uzi na ule mwingine wa Kwanza kuhusu hii
ziara muhimu sana kuliko zote za Raisi wa TZ na sehemu nyingine nyingi duniani ktk taifa la China wakati huu.

Kwanza dunia inakwenda ktk multi power order ikimaanisha hakuta kuwa na Taifa moja au mawili yenye nguvu kubwa sana itakuwa ni zaidi mawili na yenye nguvu zisizopishana sana yakiongozwa na China.

Raisi wa China amechaguliwa majuzi tu kuendelea ktk kiti chake na Raisi wetu amepewa heshima kubwa sana ya kuwa kiongozi wa kwanza kupata mualiko rasmi na Mama najua hakutuangusha hapo kutumia hiyo fursa ya kukutana na mfalme ukiwa wa kwanza kukaribishwa.

Wachina hawajatupa hiyo nafasi sababu wanatupenda ni sababu ya utajiri wetu mkubwa sana wa mali asili na stability yetu na tuombe Mungu atusimimamie kutumia hii fursa kuu kwa maendeleo ya TZ.
 
Back
Top Bottom