Tanzania, Madini na Gas

Tanzania, Madini na Gas

Zero One Two

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2007
Posts
9,346
Reaction score
3,033
Geita, Tabora, Shinyanga na baadhi ya maeneo ya Tanzania yenye neema za madini moja wapo ni hizo tajwa hapo awali, Tabora ( Nzega ) ki ujumla ni mkoa ulio nyuma sana kimaendeleo, na ni mkoa wenye madini sijui ni ki vipi madini yatokayo pale yanavyo nufaisha hiyo mkoa.

Hali kadhalika Mkoa wa Geita pamoja na Shinyanga maendeleo ya maeneo haya si mazuri, ingawa kuna uchimbaji mkubwa wa madini tena ya kutosha, wa kufanya maeneo hayo na Tanzania nzima kwa ujumla kunufaika.

Leo hii nasikia kwamba Gas itayo chimbwa Mtwara ni kwa manufaa ya Tanzania nzima ki ujumla, sipingini na hili, ila kama madini yameshindwa kuwa nufaisha wana wa Tabora, Shinyanga na Geita je? Yali wanufaisha vipi wana wa Mtwara. Simaanishi vya Mtwara vibaki Mtwara na Tabora vibaki Tabora, la hasha napingana na kauli ya kusema Gas itainufaisha Tanzania nzima na wasiwasi hata Mtwara wanaweza kua kama Tabora, Geita na Shinyanga.

Kwanza kabisa tusitegemee muwekezaji atae chimba gas kwa kuinufaisha Tanzani ( Muwekezaji atapeleka kwao atakacho kivuna Tanzania kwa manufaa ya nchi yake, tusitegemee watao chimba Gas kwamba wana mapenzi na sisi na wanafanya ivyo ili tunufaike sisi, wale wapo kwa ajiri ya nchi zao .

Kitu kingine hakuna ajira tutazopata kutokana na hiyo miradi na hata zikiwepo ni ajira uchwara, kwani jamaa wanakuja na wataalamu wao. Japo sasa ivi kuna baadhi ya kampuni kama BG na Schlumbeger zinachukua watanzanzia na kwenda kuwapa training japo ni kwa uchache sana ukilinganisha na ukubwa wa mradi.

Kutokana na haya nafikiri Nchi kama yetu inabidi itulie na kutofanya tamaa katika mambo ambayo yakikosewa madhara yake ni makubwa sana hapo badae, kwanini nchi iingie kwenye miradi mingi kwa wakati mmoja na ina ulazima gani hiyo miradi kwa Tanzani hii ya Leo?

Nafikiri Gas ya Mtwara ichimbwe huko huko na vinu vyake viwe huko huko. Kama wananchi wa Mtwara wanavyo pendekeza, japo naona Serikali imeanza kuleta zengwe kwa kusema gas nyingi ipo kwenye kina kirefu cha bahari na si Mtwara. Utumiaji mzuri wa hizi mali zetu, tulitakiwa kua na wataalamu wa kutosha na kuhakikisha more than 60% wataalamu tena wazalendo wanatoka kwetu, leo hii hata wakiamua kutuibia ni rahisi sana, maana hatuna utaalamu wala uzoefu juu ya hili jambo.

Kwa pamoja tuungane tuhakikishe Gas inakua na manufaa kwa Mtwara na Tanzania nzima kwa ujumla.
 
Naunga mkono maandamano ya mtwara maana hakuna siku MaCCM na serikali yake wakafanya jambo kama hilo.Wameshindwa kulinda twiga waliopakiwa kwenye Dege la Kijeshi huko Arusha halafu Gamba Lukuvi eti tusizungumzie EPA wala Wanyama tuzungumzie Gesi!!!!!!!!Kwanza nauunga mkono chadema kwenye sera yao ya utawala wa Majimbo ili kila jimbo lidhibiti lasilimali kwa manufaa ya wenyeji wake lakini bila ubaguzi wa Ajira na Matumizi na kama kuna Jimbo ni Masikini Lichangiwe na majimbo mengine sio kuibia watu kwa kisingizio cha Tanzania Nzima!!Mbona uchagani kuna maendeleo kuliko sehemu zingine kwani wao ndio wanatoa kodi kubwa kuliko Wamachinga????Go Mtwara msirudi nyuma hata waje majenerali wa Jeshi
 
utaungaje mkono takataka ya matapishi kama hii? akili gani kusema gas isiletwe, tumeshaanza kujenga bomba kwa hela ya mkopo kubwa sana, mabomba yalishanunuliwa na tulishaingia mkataba na wajenzi. hatuwezi kuvunja mkataba, tutawalipa mipesa mingi na hatujaanza hata kurudisha mkopo kwa wachina....kwanini hamkuanza kulalama kabla bomba halijaanza kujengwa? kwa akili zenu wakistopisha sasaivi kuna faida au hasara?
 
Back
Top Bottom