Tanzania Mabingwa CECAFA

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 23 imetwaa ubingwa wa michuano ya CECAFA kwa kuifunga Burundi kwa mikwaju ya Penalti 6 - 5 baada ya kutoa suluhu ndani ya dakika 90 kwenye uwanja wa Bahir Dar, Ethiopia
 
Wameshinda shindaje,sisi tushazoea atufikagi hata robo,sasa uko fainali mpaka kubeba kombe tumefikaje?
 
Timu anazoziongoza Kim Poulsen huwa zinafanya vizuri...

Huyu mzungu ni kama ameweza kujua namna ya kuwafunza wachezaji wetu...
 
Kweli kabisa yaani akina Lerant Lusajo ndio under 23?
Team zote za under 23 huruhusiwa kuongeza wachezaji 3 waliozidi umri kwa ajili ya kuongeza hamasa na uzoefu kwa wachezaji vijana kwenye mashindano.

Hata kwenye mashindano ya Olympic kule Japan, Dan Alves wa Brazil na umri wake wa miaka 39 alishiriki!
 
Mashindano ya vijana bila kujaza vijeba hutoboi kwa Afrika, Tulikua wenyeji wa Under 17 tukaweka umri sahihi mliona kilicho tokea!! Kwasasa ni nwendo wa vijeba tu hakuna namna.
 
Back
Top Bottom