Tanzania kwanini isitangaze rasmi lugha ya 3 ya taifa?

Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,327
1,681
Wanajf hamjambo!
Kama swali hapo ambalo huwa najiuliza mara kwa mara , Leo nimeona niwaletee tujadili kidogo kama inafaa au haifai with ground reasons.

Ukifika South Africa wao wana lugha kama nane officially recognized baadhi ni kizulu, kisuthu, Xhosa, Afrikana, English, nk .

Ukifika katika ile wanaozaliana kama sangara wao wana English, Yoruba, Hausa, IBO nk zote ni officially recognized national language huko kwenye mji MKUBWA wenye msongamano wa magari Na wengi wa madereva wasio Na nidhamu.

Huko DR Congo kuna Lingala, Kikongo, Manyema , kifaransa nk ni officially recognized Language.

Je hapa Tz kwanini Lugha ya tatu isitambuliwe kuwa lugha 3 ambayo ndiyo lugha ya kiasili inayotumiwa na watz wengi na pia Watanzania wasio wa kabila hiyo wanaifahamu asilimia kubwa Na hata humu JF mtu akisema ngosha unaelewa tu.

Kwanini kisukuma kisiongezwe kiwe lugha ya tatu ya taifa letu? Tafadhali MAENDELEO haya Vyama!
 
Kiasilia itakataa Tz kuwa na lugha ya tatu hasa eti kisukuma(kwa ground reasons zip?) .kiswahili chenyewe sio lugha ya maofisini ...kweny katiba bado haijajumuishwa kuwa officially pia kisheria inapotokea utata kama wanatumia lugha ya kiswahili sheria iko wazi lugha ya kutumika kuondoa utata au kuelewa zaidi ni english ..hapa nazungumzia kuna neno kwa kiswahili likitumika linakuwa na maana nzito kuliko kwa kingereza pia ivo ivo kwa english...mkuu lugha ya tatu bongo bado sana !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja Kisukuma kiwe lugha rasmi ya taifa maana hata Mh. Rais wetu siku moja moja huwa anatupia Kisukuma kwenye hotuba zake na sisi wananchi wanyenyekevu kwake tunamuelewa sana. Wabheja sana..
 
Hizo nchi ulizozitaja hawana lugha moja unayowaunganisha kama sisi ndio maana wakachagua lugha ambazo zinaongelewa na wengi ndio ziwe lugha rasmi.
 
Dawa zinatakiwa zimezwe kwa umakini sana..
Tanzania ni nchi iliyo na makabila mengi sana hivyo ukifanya hivyo makabila mengine yatatutumka nayenyewe kutaka hivyo..haistahiri kuwa lugha ya taifa kwanza sidhani kama inajitosheleza kimsamiati niambie kompyuta inaitwaje kwa hiyo lugha,pia calculator,rimoti je.?
Mkuu italeta mtafaruku usio mantiki bora tuendelee na tz yetu maana ikitambuliwa mtataka pia iwe lugha ya kufundishia
 
Mkuu jamaa kabakza mitano,akija mdengereko wadengereko watawaza hayo hayo.Mkuu sie tunataka ibaki moja wewe unataka Watanzania waongezewe mzigo mwingine?Tuumalize kwanza umasikini na na huu ujinga unaoongezeka kila siku,hayo mengine hayana tija kwa Taifa Hata tukiwa na lugha 52 rasmi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom